Saturday, October 29, 2016

Taarifa Kutoka CCM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Ndugu Christopher Ole Sendeka, Msemaji wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa akizungumza kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo tarehe 28/10/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

Ndugu wanahabari,

Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeli, kudhihaki, kukatisha tamaa, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania.

Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na kuichafua taswira ya nchi yetu.

Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni Watanzania. Je ni tamaa ya madaraka tu au mengine? Hakuna anayepinga ukosoaji bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema kwa nchi.

Ndugu wanahabari,
Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita ya tathmini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Katika taarifa yake hiyo, alidai kuwa alileta msisimko mpya katika siasa za Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi yetu maana ya demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais.

Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki na kuheshimu mawazo ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii, tunajiuliza ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa nayo?
-          Tulishuhudia akiwa mgombea urais wa chama ambacho hakijui, hakushiriki kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya kupeperusha bendera huku katiba na kanuni ya chama hicho  ikivunjwa.  Kidemokrasia, anayepewa fursa ya kupeperusha bendera ya chama chochote makini duniani ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo, kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi ya chama hicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi dhamira ya chama husika machoni kwa wananchi.

-          Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua mgombea “MTUNGUO” (ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia.

-          CHADEMA watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge wa viti maalumu. Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya viongozi  kuteua wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM. Msingi wa kawaida wa kupata wabunge wa viti maalum ukiacha kura za maoni, kigezo kingine muhimu ni mchango wa mgombea/mwanachama huyo katika kukijenga na kukitumikia chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA kwenye wabunge wake wa viti maalum ni mapya kwenye ulimwengu wa demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa kufanya utafiti wa aina hii mpya ya demokrasia.
Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa wangelikuwa wamejifanyia tathmini, kujikosoa, kujisahihisha na hata kufanya uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi ya demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao.

Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo za kuburudisha au kutoa matumaini hewa kwa wanachama na wananchi. Kanuni mojawapo ya demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na katika utekelezaji wa muundo huo.

Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza kuuza sera ili kujijenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya wananchi. Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia itakavyoendeshwa katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa mmoja wa vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia kupanga safu yake ya uongozi.

Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za nchi kuja Dar es Salaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kufanikisha mpango huo.

Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli, ameendela kufanya juhudi kubwa katika kuijenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya utumishi serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha, kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na wajibu kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa umma kaa la moto.

Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege mpya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, afya kwa kununua vitanda vya wazazi, kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari  na nyinginezo hazipaswi kukatishwa tamaa kwa maslahi ya wachache, ni vyema kuziunga mkono kwa maslahi ya taifa letu.

Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk. Magufuli madarakani, CCM inawaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono katika dhamira yake safi ya kuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na;-
                                                CHRISTOPHER OLE SENDEKA
MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM
28/10/2016.

Khadija Omar Kopa Adunda Mjini Mwanza na Show Kabambe!

Malikia wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omar Kopa, akitoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Mwanza usiku wa kuamkia leo ndani ya Villa Park Resort kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.
Na BMG
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Wananzengo wakifurahia burudani iliyotolewa kwenye Usiku wa Mshike Mshike na 102.5 Lake Fm
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Wananzengo kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ikijitambulisha kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Madjz wa 102.5 Lake Fm, Dj Hcue (katikati), Dj KFlip (kushoto) na Dj Dhifa (kulia)
Dj Dhifa
Dj KFlip (kushoto) na Dj Hcue
Khadija Omar Kopa akihojiwa na wanahabari baada ya show
Hakika 102.5 Lake Fm Mwanza ni Raha ya Rock City na ni Redio ya Wananzengo. Kaa tayari kwa show ijayo.
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi

Friday, October 28, 2016

Wapiga Cheni Walalamikiwa Kwa Kuvizia Magari mjini Mwanza

"Kama kuna watu wanajua kuvizia, basi hawa jamaa wa cheni wanaongoza, wanaweza kukuona unaelekea kuegesha gari eneo lisilo sahihi pengine bila kujua, badala wakuambie, wao hujificha na ukiisha egesha gari utaona wanavyolikimbilia". Amelalamika mmoja wa madereva Jijini Mwanza ambaye gari lake limeviziwa na kufungwa cheni na vijana wanaokusanya ushuru wa maegesho.
Na BMG
Kumekuwepo na malalamiko ya mara kwa mara kwamba huenda wakusanya ushuru hao ni kama wamepewa maagizo ya utendaji kazi ikiwemo kuzingatia kiwango cha kukusanya pesa, hali ambayo husababisha watumie njia za kuvizia ili kufikia lengo hilo.
Hapa ni baada ya dereva kusimamisha gari ili kushusha mzigo wake katika eneo la ofisini, wazee wa cheni wakatimba bila kujua wametokea wapi.
Zoezi likawa gumu kwa wapiga cheni baada ya kulalamikiwa sana.
Mmoja wa watu waliosadikika ni kiongozi wa wakusanya ushuru wa maegesho Jijini Mwanza, akipiga simu kwa mtu ambaye hakujulikana mara moja kufuatia watu wengi kulalamikia utendaji kazi wa wapiga cheni hao.

Saturday, October 22, 2016

Pikipiki Mzimu Jijini Dar Yazua Hofu!

 Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Dar es Salaam.
 Mwonekano wa pikipiki hiyo kwa nyuma.
Pikipiki hiyo ikiwa katika kijiwe hicho cha  Veterinary Maganga Temeke jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale

PIKIPIKI yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Temeke jijini Dar es Salaam inazua hofu kwa wananchi na hata kwa askari polisi ambao wameshindwa kuipeleka kituoni.

Imeelezwa kwamba pikipiki hiyo iliegeshwa katika eneo hilo na mtu mmoja ambaye alifika nayo akiwa akiiendesha mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza jana na mtandao wa www. habari za jamii.com mmoja wa waendesha bodaboda wa kituo hicho ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake alisema pikipiki hiyo inawapa hofu wananchi wa eneo hilo na hata waendesha bodaboda.

"Hata sisi wenyewe tuna hofu na pikipiki hii ndio maana tunaegesha mbalimbali na pikipiki zetu na ndio maana sitaki kutaja jina langu" alisema mwendesha bodaboda huyo.

Aliongeza kuwa awali baada ya pikipiki hiyo kutelekezwa katika kituo hicho mtu yeyote alipokuwa akiisogelea au kuigusa ilikuwa ikijiwasha yenyewe lakini baada ya kupita mwezi mmoja iliacha kujiwasha jambo ambalo limeongeza hofu kwa wananchi.

Mkazi mwingine wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ismail alisema hata walipotoa taarifa kituo cha polisi cha Maganga walishindwa kuichukua pikipiki hiyo kutokana na tabia ya kujiwasha.

Alisema aaskari wa kituo hicho ambacho kipo mita 10 na eneo ambalo ipo pikipiki hiyo walitoa taarifa kwa wenzao wa kituo cha Chang'ombe ambao nao wameshindwa kuichukua na kwenda nayo kituoni kwa ajili ya kumtambua mmiliki wa pikipiki hiyo kupitia namba zake za usajili.

Ismail alisema inawezekana pikipiki hiyo ilifungwa kifaa maalumu cha utambuzi iwapo kama imeibiwa na ndio maana ilipokuwa ikiguswa au kusogelewa inajiwasha yenyewe licha ya baadhi ya watu wanahusisha kujiwasha kwake na imani za ushirikina.

Imeelezwa kuwa pikipiki hiyo wakati inatelekezwa ilikuwa katika hali ya upya lakini hivi sasa imeanza kupoteza upya wake kwa kukosa huduma ya matunzo.

Jitihada za mtandao huu kumpata Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo wa Maganga ili kuzungumzia suala hilo zimeshindika baada ya kuelekezwa alikuwa Manispaa ya Temeke kwenye mkutano.


Mchungaji Daniel Kulola Ziarani Mkoa wa Dodoma

Huduma ya injili iliyofanywa na mchungaji kiongozi wa Kanisa la "EAGT Lumala Mpya Internationa Church " lililopo Sabsaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), mkoani Dodoma imekuwa ya kufaana na watu wengi wameokoka na kubarikiwa.

Ni katika mkutano wa injili ulioandaliwa na kanisa la Siloam EAGT Ipagala mkoani Dodoma kwa juma zima ambapo unatariwa kufikia tamati kesho Oktoba 23, 2016.
Picha na Jorum Samwel
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akiendelea na huduma ya maombezi mkoani Dodoma
Wengi waliponywa na wanaendelea kuponywa kwa jina la Yesu, vifungo vilivyowatesa kwa muda mrefu.
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akifanya maombezi mkoani Dodoma.

Friday, October 21, 2016

Wanafunzi wa Nyakato Primary Mwanza Darasa la 1993 Waikumbuka Shule Yao!

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi Afisa Mtendaji wa Kata ya Muhandu ilipo shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo. 

Mbali na vifaa hivyo, pia wanafunzi hao ambao miongoni mwao ni wafanyabiashara na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, wametoa vifaa vya michezo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo mipira na jezi, pamoja na zawadi mbalimbali kwa ikiwemo kompyuka kwa baadhi ya waliokuwa waalimu wao kipindi hicho.
Na BMG
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakiwakabidhi baadhi ya waalimu pamoja na kamati ya shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo. 
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakikabidhi vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo. 
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo. 
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo. 
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo. 
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kulia), wakimkabidhi zawadi ya kompyuta aliyekuwa mwalimu wao, Mwalimu Nicholaus Magashi (kushoto).
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi zawadi mmoja wa aliyekuwa mwalimu wao, Mwalimu Elizabeth Makonda (kulia).
Kaimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, Florence Sam, akisoma taarifa ya shule hiyo kwa wanafunzi waliohitimu shuleni hapo mwaka 1993 walipoitembelea na kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta pamoja na printa.
Mwalimu Benadetha Athanasi, akitoa taarifa fupi kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza mwaka 1993.
Atley Kuni akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza mwaka 1993, namna wazo kusaidia shule ya msingi waliyosoma lilivyoanza kwenye mitandao ya kijamii (kundi la whatsupp).
Baadhi ya Waalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza, kamati ya shule pamoja na baadhi ya waaliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo.
Baadhi ya Waalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza, kamati ya shule pamoja na baadhi ya waaliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo, wakiimba wimbo wa Taifa.
Mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha.
Mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha.
Mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha.
Mwalimu Nicholaus Magashi, aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha
Mwalimu Elizabeth Makonda, aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akisalimia
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza, 2016
Moja ya darasa walilosoma wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwnza.
Moja ya darasa walilosoma wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwnza.
Picha ya pamoja kati ya wanafunzi waliohitimu darsa la saba shule ya Nyakato Jijini Mwanza, pamoja na waalimu wa shule hiyo.

Na George Binagi-GB Pazzo
Wadau wa elimu mkoani Mwanza wametakiwa kushirikiana na serikali katika kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za waalimu katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza.

Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Florence Sam, ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya kupokea vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta pamoja na printa, vilivyotolewa na wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo mwaka 1993.

Mwalimu Sam amesema shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1,800 huku vyumba vilivyopo vikiwa ni 18 hali inayosababisha kuwa na upungufu wa vyumba 32 ambapo ametumia fursa hiyo kuwaasa wadau mbalimbali kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo, Mwalimu Benadetha Athanasi, amesema wanafunzi hao wameamua kusaidia kutatua baadhi ya changamoto za shule hiyo ili kutoa mwamko kwa wadau wengine kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu nchini.

Vifaa vilivyotolewa na wanafunzi hao ni pamoja na vifaa vya michezo kwa wanafunzi, kompyuta pamoja na printa ambavyo vimegharimu Zaidi ya shilingi Milioni Mbili.