Saturday, June 27, 2015

Onyo - Sindano Za Kuongeza Saizi ya Makalio!

Wadau, nimewaambia mpende Mwenyezi Mungu alivyowaumba. Acheni huo mtindo wa kujichubua na kutaka matako yako yawe makubwa sana!  Kuna mtindo Afrika sasa ya kutaka  kuongeza saizi ya matako kwa kuchoma sindano.  Sindano zingine na nyingi ni feki na zina sumu kama Fix a Flat ambayo inatumika kama tairi ya gari ikipata pancha. Sasa unalipa hela yako, wahuni wanakuchoma hiyo sindano, siku mbili tatu unatamba na matako yako waliyovimba kama puto halafu baada ya wiki unaona matakao yako yanaoza.  Hebu ona yaliyompata mwenzenu.


Wednesday, June 24, 2015

Tanzia - Mrs. Mariamu Mwajuma Musisa

11261405_1439531623036433_198071232238341808_o

DR. ALI MZIGE wa Mikocheni, Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha Dada yake MRS MARIAMU -MWAJUMA MUSISA (NEE MZIGE) kilichotokea Raleigh, North Carolina Marekani tarehe 21-06-2015. Mwili wa marehemu utaletwa Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Tutatoa taarifa zaidi mwili utakapowasili. Kwa mawasiliano tafadhali mpigie Yussuf Mhiro 0754-609-338 / 0714-979-014.Usoma taarifa hii tafadhali wajulishe ndugu jamaa na marafiki wa Ukoo wa Humbi Ziota na Musisa. Au Kaka wa Marehemu DR. ALI A. MZIGE 0713 410 531, 0754 495 998.

Inna Lillahi, wa inna ilaihi ra'ajiun.

Sunday, June 21, 2015

Wapiga Picha wa Vyombo Vya Serikali Enzi Hizo!

 Nilifanya kazi nao wapiga picha nikiwa mwandishi wa habari Daily News miaka ya 1980's! Enzi zile tulikuwa wachache na wote tulijuana.  Mzee Makwaia alikuwa Mwalimu wetu TSJ. Alifariki tukiwa mwaka wa kwanza baada ya kugongwa na gari Morogoro Road.

 Kwa hisani ya Kaka Juma Dihule:

WAFAHAMU WAPIGAPICHA WA VYOMBO VYA SERIKALI ENZI HIZO.
Wapigapicha wa wakati huo ambapo vyombo vya habari vilimilikiwa na Serikali pamoja na chama tawala. Waliosimama nyuma toka kushoto marehemu Max Madebe (Mpigapicha Mkuu gazeti la Mfanyakazi, Marehemu Sam Mbando, mpigapicha mwandamizi Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA), Marehemu Vincent Urio (Mpigapicha Mkuu magazeti ya Serikali ya Daily News & Sunday News, Marehemu John Makwaia ndiye aliyekuwa mwalimu wetu sisi wote na mpigapicha mkuu wa Serikali katika Idara ya Habari (MAELEZO), akifuatiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye pia ni marehemu, David Saileni ambaye wakati huo akiwa mpigapicha mwandamizi wa Sinema, upande wa Idara ya Habari, (Film Unit), Juma Dihule, Mpigapicha Mkuu SHIHATA, Marehemu Adnani Mihanji, Mpigapicha Mwaandamizi, SHIHATA na Moshy Kiyungi, Mpigapicha mwandamizi ( Idara ya Habari).
Walioketi toka kushoto, Steven Kasange, IKULU, Charles Kagonji , Mkutubi Mkuu wa maktaba ya picha MAELEZO na pia akiwa mpigapicha, Gaspar Msilo, Daily News, Mwanakombo Jumaa, MAELEZO, Hatib Ali Mpichapicha Mkuu (Uhuru na Mzalendo) Raphael Hokoro , ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

Saturday, June 20, 2015

Ubaguzi Marekani!

Yaani kama huyo kijana wa kizungu aliyeua watu 9  huko South Carolina angekuwa mweusi polisi wangemwua!  Alikamatwa na kurudishwas South Carolina kwa ndege! Eric Garner alikuwa anauza sigara tu, walimwaua! Mimi binafsi nilikuwa namfahamu marehemu Eric, alikuwa jitu kibonge cha mtu lakini mstaarabu.

Tanzia - Florence Dyauli, Mtangazaji wa TBC

 Nimesikitika sana kusika habari ya kifo cha Dada Florence Dyauli.  Nilifanya kazi naye nilipokuwa Practical Training RTD nikiwa mwanafunzi Tanzania School of Journalism. Pia tulikuwa pamoja kwenye shughuli za TAMWA.  Rest in peace Dada Florence.

*************************************************

KUTOKA LUKWANGULE BLOG:


The Late Florence Dyauli (1961-2015)

MWANDISHI wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa upande wa Televisheni Florence Dyauli amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Rabininsia memorial iliyopo jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kutokana kusumbuliwa na maradhi ya Nimonia

Taarifa iliyotolewa jana na ofisi za TBC ilisema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Nimonia na alilazwa kwa ajili ya matibabu hadi jana usiku mauti ilipomfika.

Taratibu za mazishi zilikuwa bado hazijafanyika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo ya Rabininsia ukisubiria taratibu za mazishi kutoka kwa ndugu wa familia.

Florence alizaliwa Julai 27, 1961 ambapo alipata elimu yake ya msingi kuanzia 1968 hadi mwaka 1975 katika shule ya Msingi Chang’ombe iliyopo jijini Dar es salaam.

Alifanikiwa kujiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Kisutu girls kati ya mwaka 1976 hadi 1979. Baadae alijiunga na chuo cha Tabora secretarial College kuanzia mwaka 1980 hadi 1981 na kujipatia mafunzo ya cheti cha ukarani.

Mnamo mwaka 1986 hadi 1988 alijiunga na chuo cha uandishi wa habari kwa ngazi ya stashahada ya uandishi wa habari.

Aliniajiriwa kama mwandishi wa habari msaidizi katika kituo cha Radio Tanzania Dar es salaam kuanzia 1982 hadi Novemba 1999.

Kisha mwaka 1994 hadi Novemba 1999 alikuwa Shift Editor .

Hadi mauti inamkuta, marehemu alikuwa mwandishi wa habari daraja la kwanza kwa upande wa Televisheni ya Taifa TBC.

Kampeni ya Kinana Katika PIcha

KINANA APIGA KAZI BUSANDA NA MJI MDOGO WA KATORO LEO, MIKUTANO YAFURIKA MAELFU YA WATU, AACHA GUMZO KWA HOTUBA ZAKE NZITO, NAPE AWANYAMAZISHA WAPINZAI KUONA PICHA TAFADHALI>BOFYA HAPA AU CHUKUA CODES HAPA CHINI
 
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwasili katika viwanja vya stendi kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Katoro, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, mkoani Geita, leo. Kulia ni Msemaji wa Chama, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya stendi katika mji mdogo wa Katoro, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, mkoani Geita, leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisisitiza jambo alipohutuba mkutano huo katika mji mdogo wa Katoro
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, uliofanyika leo katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita
 Nape akisisitiza kuwa CCM ni imara, hivyo itashinda uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu kwa kupata kura za kishindo kutokana na kuwa ndicho chama ambacho bado kinakubalika Tanzania kutokana na kuonyesha kwa vitendo kuwajali wananchi.
 Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya stendi, katika mji mdogo wa Katoro, Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika mji huo mkoani Geita leo
 Baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Katoro wakiwa wamepanda hadi kwenye majengo ili kuweza kumshuhudia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo hilo mkoani Geita,leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia na 'msela' wa mji mdogo wa Katoro, aliyefuata meza kuu, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji huo mdogo mkoani Geita leo
 Mbunge wa Busanda, Lorencia Bukwimba, akisalimia wananchi katika mkutano huo wa Kinana uliofanyika katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita leo
 Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata akisalimia wananchi katika mkutano huo wa Kinana uliofanyika leo katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kulima barabara katika kijiji cha Nyakanga, katika jimbo la Busanda, mkoani Geita, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani humo leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi alipofika kukagua shughuli za vikundi vya wajasiriamali na vijana wanaoshiriki mchezo wa soka, katika mji mdogo wa Katoro, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita, leo. Kushoto ni Mbunge wa Busanda Lorencia Bukwimba.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi alipofika kukagua shughuli za vikundi vya wajasiriamali na vijana wanaoshiriki mchezo wa soka, katika mji mdogo wa Katoro, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita, leo. Kushoto ni Mbunge wa Busanda Lorencia Bukwimba.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi alipofika kukagua shughuli za vikundi vya wajasiriamali na vijana wanaoshiriki mchezo wa soka, katika mji mdogo wa Katoro, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita, leo. Kushoto ni Mbunge wa Busanda Lorencia Bukwimba.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi alipofika kukagua shughuli za vikundi vya wajasiriamali na vijana wanaoshiriki mchezo wa soka, katika mji mdogo wa Katoro, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita, leo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana azungumza na wananchi alipofika kukagua shughuli za vikundi vya wajasiriamali na vijana wanaoshiriki mchezo wa soka, katika mji mdogo wa Katoro, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Geita, leo..
Mbunge wa Busanda Lorencia Bukwimba akisalimia wananchi kwenye mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili katika Kijiji cha Chikobe,  kukagua ujenzi wa Ofisi ya CCM na kuzungumza na wananchi katika kijiji hicho jimbo la Busanda
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji hicho cha Chikobe
 Kinamama wa kijiji cha Chikobe wakimshangilia Kinana alipozumgumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumzana wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Chikobe, katika jimbo la Busanda mkoani Geita leo
 Mbunge wa Busanada Lorencia Bukwimba akisalimia wananch katika mkutano huo wa Chikobe
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili katika kijiji cha Nyakanga, jimbo la Busanda mkoani Geita ambapo wananchi walimlaki wa nderemo na vifijo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa Kijiji cha Inyala, katika Jimbo la Busanda mkoani Geita, leo
 Wananchi katika ijiji cha Nyakanga jimbo la Busanda wakimshangilia Kinana alipohutubia mkuano w hadhara katika kijiji hicho leo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata alipowasili katika kijiji cha Nyakanga, kuanza ziara yake katika jimbo la Busanda mkoani Geita leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nyarugusu, ambako alipokea malalamiko kuhusu wananchi kunyimwa eneo la kufanya uchimbaji mdogowa madini huku serikali na mwekezaji wakiwa hawalitumii eneo hilo kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
 Kijana akionyesha machejo wakati kikundi cha ngoma ya Baswezi kilipotumbuiza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika kijiji cha Nyan'kanga, jimbo la Busanda mkoani Geita leo
 Nyumba ya Mganga inayoendelea kujengwa katika Kijiji cha Inyala, jimbo la Busanda  mkoani Geita
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu nyumba hiyo ya mganga wa Zahanati ya Kijiji cha Inyala katika jimbo la Busanda, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na uhai wa Chama mkoani Geita, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM BLOG

Wednesday, June 10, 2015

Nyimbo za Kumuaga Rais Kikwete

NYIMBO ZA KUMUAGA RAIS JAKAYA KIKWETE HEWANI !

SI WENGINE NI NGOMA AFRICA BAND AKA FFU -Ughaibuni
yenye maskani kule ujerumani 
 Mtunzi:Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja 
Waimbaji: Kamanda Ras Makunja
            Afande Chris-B ambaye pia ni mpiga solo gitaa
Bendi: 
Ngoma Africa band aka FFU
wasiliana nao at ngoma4U@gmail.com

Tuesday, June 09, 2015

Muigizaji 'Mzee Kankaa' Afariki Dunia

Kutoka Tanga Yetu Blog:

MSANII mkongwe wa filamu nchini, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amefariki dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwake Tandale jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu.

Mwili wa Mzee Kankaa unatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni katika makaburi ya Ali Maua jijini Dar es Salaam.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya miaka mitatu. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Tandale-Chama jijini Dar.


The Late Mzee Kankaa
 Kwa habari zaidi Tembelea TANGA YETU BLOG