Sunday, November 30, 2014

Wafunga Ndoa Uchi

Haya jamani, kwa nini mnapoteza kununua nguo za harusi wakati mnaweza kusevu pesa kwa kufunga mkiwa uchi?  Hao wazungu walisema hela ya nguo watatumia kwa ajili ya kulipa mortgage ya nyumba! Ingekuwa safi kama wageni nao wangekuwa uchi.  Kutoka https://www.facebook.com/pages/Ijebu-News-Xtra/121224847988714?fref=photo


Saturday, November 29, 2014

Rais Kikwete Awasili Dar es Salaam, Apata Mapokezi Makubwa!


PICHA NA IKULURais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati
ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye
matibabu leo Novemba 29, 2014
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la
Polisi IGP  Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea
Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na
waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29,
2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama
Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye
matibabu leo Novemba 29, 2014

.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua
kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya
kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa
mjukuu wake aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu
akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
.

Saturday, November 22, 2014

Tanzania Imeibiwa Tanzanite

Kutoka THE CITIZEN

Jamani, serikali iko wapi? Tunaibiwa madini, wengine wanafaidi. Hiyo hela ingesaidia kukarabati hospitali, shule etc.Al Shsabab Waua Abiria wa Basi wasio WaIslam Kenya

 Jamani, jamani! Tunaelekea wapi? Hizi chuki za kidini ziishe!  Siyo utamaduni ya Afrika Mashariki.

Mungu ailaze roho zao mahala pema mbinguni. Amen.

****************************************

Police: Al-Shabab militants kill 28 in Kenya bus

   NAIROBI, Kenya (AP) - Police officials say al-Shabab militants from Somalia have hijacked a bus in northern Kenya and killed 28 non-Muslims on board.

   The two police officers said Saturday that the bus traveling to the capital Nairobi was hijacked 50 kilometers (31 miles) from Mandera town. The officers say the gunmen singled out non-Muslims and shot them dead.

   The officers insisted on anonymity out of fear of reprisals because of an order from Kenya's police chief that officers not speak to the media.

   Kenya has been hit by a series of gun and bomb attacks blamed on Somalia's al-Qaida-linked al-Shabab militants since it sent troops into Somalia in October 2011. Authorities say there have been at least 135 attacks since then, including the Westgate Mall attack in which 67 people were killed.

Friday, November 21, 2014

Amsulubu Aliyemwibia Mume Wake!Wadau, hii kali! Wanawake wote wangesulubu wanaowaibia wanaume wao hivyo, wizi huo ungepungua sana!

Sunday, November 16, 2014

Jaji Mkuu Amjulia Hali Rais Kikwete Marekani

 Picha na habari kutoka Ikulu.


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe
Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba
16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins
jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika
hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa
Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi
ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria
mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi
jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na
marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo
ya mahakama.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake
waliopomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika
hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore,
Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo
alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako
Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na
ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya
Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi
mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia
wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya
rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,
daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Mhe Hussein Katanga.

Saturday, November 15, 2014

Mchawi Atubu, Aomba Msamaha! (Samahani Yuko Uchi)

Huyo mchawi alikamatwa aliloga. Wachawi wakitambika wanakuaga uchi, ndo mana huyo mchawi yuko uchi!  Akome kabisa kuloga watu! Naona aliogopa kipigo cha kufa huyo! Mwone na shanga zake! Wangemtoa kabisa!
Friday, November 14, 2014

Maoni ya Prof. Joseph Mbele Kuhusu Kunyayaswa kwa Jaji Warioba

 Kutoka  Hapa Kwetu  Blog 

Kuhusu Kunyanyaswa kwa Jaji Warioba

Kati ya mambo yaliyonishtua sana mwaka huu ni kunyanyaswa kwa Jaji Warioba. Kadhia hii imetokana na kazi murua aliyofanya Jaji Warioba na tume yake ya kukusanya mawazo ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.

Kumekuwa na mlolongo wa matukio kadhaa ya unyanyasaji huo, ambao, kwa kadiri ninavyofahamu, mwanzilishi wake ni Ikulu. Tukio la kupigwa Jaji Warioba mkutanoni, ambalo limeripotiwa sana, ni kilele cha utovu huu. Wengi tunaamini kuwa Jaji Warioba ananyanyaswa kwa sababu ya uwazi na uwakilishi wa mawazo ya wananchi, jambo ambalo ni mwiba kwa mafisadi.

Nimeshtushwa vile vile na kauli ya Rais Kikwete kuhusu tukio hili la vurugu na kupigwa Jaji Warioba. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, Rais Kikwete aliishia tu kusema kuwa anaomba yasimkute yaliyomkuta Jaji Warioba. Sikuona popote kama aliongelea suala hili kwa undani na mapana kama linavyostahili.

Yeye kama Rais, nilitegemea kwanza atambue kuwa vurugu zile ni aibu kwa nchi anayoiongoza. Nilitegemea awakemee walioleta vurugu zile zilizohusisha pia kunyanyaswa kwa Jaji Warioba.

Nilitegemea Rais Kikwete atumie fursa ile kuwakumbusha wa-Tanzania, wajibu wao wa kuheshimiana na kulumbana kwa hoja, sio kwa mabavu. Angefanya hivyo, nigesema Rais ameonyesha busara za kiuongozi. Nilitegemea angekemea utovu wa ustaarabu uliojitokeza. Angewakumbusha wa-Tanzania njia ya usataarabu. badala ya yeye kujiwazia yeye binafsi, kwamba anaomba yasimpate. Je, kauli yake hii si sawa na kumezea uovu? Kauli yake haikuonyesha busara za kiuongozi.

Halafu, kuna pia kauli ya Samuel Sitta, ambayo nayo imenikera. Sitta aliripotiwa akisema kuwa Jaji Warioba alijitakia yaliyomkuta. Niliposoma taarifa hii, sikuamini kama mzee Sitta, anayetegemewa ana busara, angeweza kuwa na msimamo kama huo.

Nasikia Sitta ni msomi. Nami najiuliza: ni msomi gani ambaye hatambui wala kutetea mijadala au malumbano ya hoja. Kusema kuwa Jaji Warioba alijitakia yaliyompata ni sawa na kumezea suala la mjadala kuingiliwa na vurugu ambazo hazikubaliki katika mijadala. Kauli ya Sitta ni kama inahalalisha ukosefu wa ustaarabu unaotegemewa hasa kwa wasomi.

Sijui Sitta alikulia wapi na katika maadili gani. Sisi wengine tulilelewa katika maadili ya kuwaheshimu wazee. Kitendo cha kumpiga mzee, kwa mujibu wa maadili yale, ni mwiko kabisa. Kama hukubaliani na mzee, unapaswa kutafuta namna ya kujieleza, ambayo ni ya heshima kabisa. Nilitegemea Sitta atambue na kuzingatia hilo. Atoe mfano kwa watoto na vijana.

Tena na tena, katika jamii yetu, tumezoea kukemea tabia tunazoziiita haziendani na maadili au utamaduni wetu. Nimeshangaa kuona kuwa Sitta, ambaye ni mzee, anayetegemewa kuwa mlinzi na mtetezi wa maadili bora, haonekani kutambua kuwa Jaji Warioba kama mzee, hawezi kuletewa vurugu kama alizoletewa. Nimekerwa kabisa na kauli ya Sitta na kauli ya Rais..

Rais Kikwete Atoka Hospitalini Baada ya Kupata Nafuu

 PICHA NA HABARI KUTOKA IKULU:Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akisindikizwa na Daktari Bingwa
Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya
kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali ya Rais
Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapumzikoni
akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa, kabla ya
kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya
mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za
Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia
pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi
mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye
amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer
muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Hali ya
Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa
mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku
chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete
pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi
(SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu
mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi
wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza  (Picha na
Freddy Maro)

Rais Kikwete Aruhusiwa Kutoka Hospitalini!

 Kutoka  AllAfrica.com

President Jakaya Kikwete has been discharged from the Johns Hopkins Hospital in the United States on Wednesday evening after a successful prostate gland surgery and moved to a special hotel under close medical supervision.

A statement issued in Dar es Salaam on Thursday by the Directorate of Presidential Communications said the hotel is having close working relationship with the hospital, which is located in Baltimore in the Province of Maryland.

President Kikwete, who is in the US for a health check-up, underwent a prostate gland surgery last Saturday. His condition has improved and he has started light exercises.

While at the special hotel, he will regularly be visited by doctors and nurses for a period of one week. According to the treatment plan, the president will later undergo another check-up to enable doctors decide on the next course of action, read the Ikulu statement in part.

Meanwhile, following the barrage of text messages (SMS), which the president has been receiving from well wishers, the public can also wish him well through number +1-646-309-2295.

Sunday, November 09, 2014

Rais Kikwete Anaendelea Vizuri Baada ya Upasuaji John Hopkins Hospital (USA)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini
Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika
hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini
Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi
Dume.

Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema
na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo
yote ni mswano. Tutaendelea kwuashirikisha taarifa ya maendeleo yake
mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani
kulijenga Taifa.

PICHA NA IKULU

Rais Kikwete Afanyiwa Upasuaji Marekani!

Tumwombee uzima Rais wetu Mpendwa, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Amen, Amin.

****************************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akizungumza na  Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya
Johns Hopkins na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi(kulia) baada
ya kuwasili katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore,
Maryland,  Marekani kwa upasuaji Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo
uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa
Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha
upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo
Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua
muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa
upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.

Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji
matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa
Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini
ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete
kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.

Imetolewa na

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014

Saturday, November 08, 2014

Basi la Happy Nation yapata Ajali Mbeya!


 Natoa pole kwa waliojeruhwa!

****************************************************Basi lenye namba T281 ARR mali ya Happy Nation likiwa limepinduka eneo la Meta Igurusi kilometa 54 kutoka Mbeya

Picha na Maelezo Kutoka MBEYA YETU BLOG:Watu 37 wamenusurika kifo baada ya basi la abiria lenye namba za usajili T 281 ARR aina ya Scania linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar es Salaam linalomilikiwa na Kampuni  ya Happy Nation kuacha njia na kupinduka eneo la Meta Kata ya Igurusi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa moja asubuhi  basi hilo likitokea Mbeya baada ya kupasuka gurudumu la mbele kulia kisha kupoteza uelekeo  na baadaye kumgonga mpanda baiskeli na kupinduka.Msangi amesema baada ya ajali hiyo Dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina moja la Shabani alikimbia ambapo Jeshi la Polisi linafanya juhudi za kumtafuta ili kueleza sababu za ajali hiyo.Aidha Msangi amesema katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi 37 wanaume 26 wanawake 10 na mtoto mmoja wa kiume.Baada ya ajali hiyo majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala ambapo mjeruhi 10 bado wamelazwa na wanne wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.Kwa mujibu wa Daktari Mkuu Mahenge wa Hospitali ya Chimala amesema kuwa waliolazwa Hospitalini hapo ni wanaume sita na wanawake wanne na walohamishiwa Rufaa ni wanaume wanne.Daktari Mahenge amesema kuwa hali za majeruhi 10 walipo Chimala hali zao zinaendelea vema ingawa wanakabiliwa na upungufu wa damu na wameomba msaada katika kitengo cha benki ya Damu salama Mbeya.Hata hivyo baadhi ya abiria wamelalamikia mwendo kasi wa basi hilo kwani baada ya kutoka kituo kikuu cha Mabasi lilianza kwenda kwa mwendo wa kasi na mara kadhaa walikuwa wakimuonya Dereva lakini alikuwa akikaidi.Pia walikuwa wakifukazana na mabasi mengine yaliyotokea Mbeya kuelekea Jijini Dar es Salaam hali iliyosababisha basi hilo kupasuka gurudumu la kulia likiwa katika mwendo kasi na kona kali kisha kupinduka.Wakati huo huo Kamanda Ahmed Msangi amesema  watu wawili wamefariki dunia wilayani Mbozi baada ya roli la mizigo kugongana uso kwa uso na gari linalomilikwa na NSSF.


Msangi amesema bado majina ya waliofariki hayajapatikana na kwamba Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali na miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali Mbozi.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA:

Usikate Tamaa

Nilibakwa nikiwa na Umri wa Miaka 9" - Oprah Winfrey

"Sikumaliza hata Elimu yangu ya Chuo" - Bill Gates

"Kwenye Maisha ya Utotoni, Nilidhurumu Viatu" – Abraham Lincoln

"Nilipata sana shida katika kipindi chote nilichokuwa Shule" - Dr Ben Carson

"Nilikuwa nauza Chai Dukani ili niweze kupata Hela kwa ajili kufanikisha Mazoezi" - Lionel Messi

"Nililala Sakafuni kwenye Vyumba vya Marafiki , nikiwa nakusanya Chupa za Coke kwaajili ya Hela
ya Chakula, na pia kupata Chakula cha Bure cha Wiki kinalichotolewana Wahisani" - Steve Jobs

"Mwalimu wangu alikuwa akiniita Anayefeli" – Tony Blair

KUMBUKA:
Maisha sio kile ambacho hujakifanya mpaka sasa, ila ni juu ya kile ambacho bado una muda na uwezo wa kukifanya!!!
USIKATE TAMAA


Sunday, November 02, 2014

Jaji Warioba Anusurika Kupigwa Kwenye Mkutano!

Nchini Tanzania vurugu zimekatisha mdahalo ulioitishwa kujadili yatokanayo na rasimu ya katiba iliyopendekezwa. Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Warioba, alikuwa jukwaani wakati vurugu zilipozuka. Wanaounga mkono rasimu wamedaiwa kusababisha vurugu ukumbini.Wapo watu waliojeruhiwa. Nini maoni yako na umelipokea vipi tukio hilo? Habari zaidi katika Amka na BBC.

Saturday, November 01, 2014

Mzee Richard Mabala Amefiwa na Mke Wake

Kutoka Facebook

Mke wangu mpenzi, Etinisimbo (Manka) amefariki dunia leo baada ya kuugua muda mrefu. Mungu amempumzisha maana magonjwa yalikuwa yanamtesa sana. Naomba sala zenu.

My beloved wide Etinisimbo (Manka) passed away today after months of fighting sickness. She has suffered so much. May God grant her peace now and all of us.