Nimeletewa kwa E-mail.
**************************************************
Habari za kazi na shukrani kwa kutuhabarisha kwa kutumia blog.
Naleta malalamiko yangu kuhusu tovuti ya school of law (zamani faculty of law) ya chuo kikuu cha dar es salaam. tovuti hii ina zaidi ya miezi sita sasa ipo under construction. watu tunataka habari za chuo aidha kujiunga kwa kozi mbali mbali au kujua habari mbali mbali lakini tunatatizwa na kukosekana kwa tovuti hiyo.
Inashangaza na kusikitisha kuwa zaidi ya miezi sita tovuti hiyo ipo matengenezoni... jee wahusika wanalijua hili? jee wanajenga tovuti au ghorofa la makaazi na ofisi?
Ustaarabu ungewafanya kuimaintain tovuti ya awali ya faculty of law kabla ya kuifuta wakati wanaendelea kuitengeneza hiyo ya school of law ili kutokatisha wananchi na wadau habari kwa muda mrefu. tunaomba wahusika walitafutie ufumbuzi tatizo hili.