Saturday, September 16, 2023

Mji wa Derna, Libya Yaangamizwa na Mafuriko! Watu zaidi ya 20,000 wahofia kufa!

Ni Mambo ambayo tumesoma kwenye biblia...mji mzima kuangamizwa!   Wiki iliyopita huko Libya mashariki ulipita Kimbunga Daniel.  Mvua ulinyesha mwingi sana hadi bwawa mbili zilipasuka na kusababisha mji wa Derna kuteketezwa kwa maji!   Ajabu, Libya ni JANGWA! Crescent Nyekundu wa Libya wanasema watu karibu 20,000 wamehofia kufa!  Ila wataalamu wamiundo mbinu wanasema kuwa tangu Rais Ghadaffi auawawa hizo Bwawa hazikutunzwa ipasavyo ndo maana zika pasuka

KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA:

Monday, May 15, 2023

Tanzia - William Malecela aka. LeMutuz

 

Hayati William Malecela aka Le Mutuz
1961-2023

Yaani, kweli hujui siku utaaga dunia hii. Nimeshutuka sana kusikia habari ya kifo cha kaka yangu wa ubatizo, William Malecela 'aka' LeMutuz.  Baba yake  Mh. John Malecela, na marehemu mke wake walisimamia ubatizo wangu.

Nilikuwa namwona William Dar wakati nasoma Zanaki Girls Secondary School. William kipindi kile alikuwa na afro, kijana fit. Nilisikia alienda kuwa baharia, halafu nilikutana naye tena New York City.  Baada ya muda aliamua kurudi kimoja Tanzania. Tulikuwa tunawasiliana kwa muda lakini...ndo hivyo alivyokuwa King wa Social Media Tanzania, alikata mawasialiano maana skikubaliana naye kuhusu mambo kadhaa.  Nikawa namwona  kwenye mtandao tu...mara kanda za majungu..mara fashion show. 


Mara la mwisho kumwona William ilikuwa hivi na shati hiyo hiyo...tuliongea kidogo..Aliniaga na mikono hivyo hivyo  kama pichanai..kumbe ananiaga. Siku hiyo nilimwona Mlimani City, Dar es Salaam. Sikujua itakuwa mara la mwisho kumwona ana kwa ana.

Kaka William ametangulia.  Mungu ailaze roho yake mahal pema mbinguni. Amen

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Saturday, January 14, 2023

Msiba Boston - Bibi Sipora Minani

 Familia ya Mzee David Mvuyenkure, wa Chelsea, Massachusetts, USA inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao..Bi Sipora Minani, kilichotokea jan, Ijumaa Tarehe 13, Januari nyumbani kwao.  Alikuwa ni muamini wa siku nyingi wa kanisa la The International Gospel Church, Chelsea, Ma.

Mipango ya mazishi ni yafuatayo:


The Late SIPORA MINANI  

1950 – January 13th, 2023

Wake and Viewing

  Thursday, January 19th, 2023   from 4:00PM to 8:00PM

Vazza Beechwood Funeral Home - 262 Beach St, Revere, MA 02151

Funeral

Friday, January 20th, 2023 

Viewing from 9:30 – 11:00AM

Service 11:00AM – 12:30PM

Vazza Beechwood Funeral Home - 262 Beach St, Revere, MA 02151

Burial 

Woodlawn Cemetery   - 302 Elm St, Everett, MA 02149

Repas Immediately After Burial

The International Gospel Church, 85 Crescent Ave., Chelsea, MA 02150

Saturday, December 31, 2022

Papa Mstaafu Benedict wa XVI (16) Afariki Dunia                                                      Hayati Papa Benedict XVI

 Papa Mstaafu Benedict XVI amefariki dunia leo asubuhi huko Vatican, Italia.  Ilitanganzwa mapema wiki hii kuwa afya ya Papa Benedict XVI ilikuwa imezorota.  Amefariki kwenye Monestari ya Vatican.  Alikuwa na miaka 95. Jina aliyozaliwa nayo ilikuwa Joseph Ratzinger. Alizaliwa Ujerumani mwaka 1927.

Atazikwa Alhamisi Ijayo huko Vatican baada ya Misa itakayosimamiwa na Papa Francis.  Papa Benedict XVI hakutaka mazishi enye makuu. 

Papa Benedict XVI  alistaafu ghafla mwaka 2013.   Alikuwa Papa wa kwanza kustaafu katika miaka 600 iliyopita ya Vatican. Kwa kawaida mtu anaachia upapa akifa.  Papa (Pope) ni mkuu wa kanisa Katoliki duniani.

Mungu Ailaze Roho ya Papa Benedict XVI mahala pema peponi.  AmenSaturday, December 17, 2022

Nyani Wasaidia Wanasayansi katika Utafiti kugundua chanzo cha Binadamu kutembea kwa Miguu Miwili


                           Familia ya Nyani aina ya Chimpanzee

Nyani wa Tanzania wanasaidia wanasayansi kugundua sababu ya binadamu kutembea kwa miguu miwili.  Pia tusisahau kuwa wanasayansi wanasema Tanzania ni chimbuko la bindamu duniani.  Kusoma habari zaidi BOFYA HAPA 
Saturday, October 01, 2022

Mnaifahamu Tanzania Life Project ?
Tanzania Life Project ni NGO inayaosaidia wananchi wanaoishi kwenye vijiji vilivyo n ukosefu wa maji kupata maji.   Wanachimba visima ili kusaidia kupata maji na kuepuka kutembea misafa mirefu kutafuta maji

Nilipotoka Tanzania nilikutana na baadhi ya watu waliojitolea (Volunteers) walioenda  Dodoma, Tanzania kusaidia wanavijiji.

Kwa kweli niliguswa sana na moyo wao wa kusaidia watu kupata maji.  Ninakumbuka enzi zile...Tabora maji yalikuwa ya shida sana. Ukiyapata yana rangi ya maziwa. 

Zaidi ya kuchimba visima, wanatoa ruzuku kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, na wantaoa elimu kwa wanawake na wanaume kwa ajili ya kuimarisha maisha yao.


tKwa habari zaidi BOFYA HAPA: 

Saturday, May 14, 2022

Mauaji Buffalo New York! Mzungu Aneyechukia Watu weusi Amewaua wakiwa Shopping Supermarket!

 
 (AP) Multiple people have been shot at a supermarket in Buffalo, New York. Police there said in a Saturday afternoon tweet that the alleged shooter was in custody. Details on the number of people shot at the Tops Friendly Market and their conditions weren't immediately available. Police officials and a spokesperson for the supermarket chain did not immediately respond to messages seeking comment. Gov. Kathy Hochul tweeted that she was "closely monitoring the shooting at a grocery store in Buffalo," her hometown. The supermarket is in a primarily residential part of a predominately Black neighborhood, about 3 miles north of downtown Buffalo.