Ugonjwa wa Mafua ya Ndege (Bird Flu) – Disease of the Day!
Haya jamani, kuna huo ugonjwa unaitwa Bird Flu ambayo wanasema iko hatarini kuingia bara Marekani na kuangamiza maelfu ya watu. Kila ukifungua TV unasikia mtu au ndege kapatikana na ugonjwa huo hatari huko China au bara Asia eti kapata kwa kula kuku mwenye huo ugonjwa. Basi watangazaji wanaanza kujadili na kutabiri lini utaingia Marekani.
Lakini nataka kuzungumzia hasa jinsi watu Marekani walivyo waoga wa magonjwa yanayotoka barani Asia na Africa. Miaka ya nyuma kulikuwa na tishio la ugonjwa wa Ebola. Basi waafrika waliotoka barani Afrika walikuwa wanachunguzwa kwa makini. Yaani mtu atoke Africa hasa Congo, aende kwa daktari hapa USA, basi kisirisiri daktari anajaza ile fomu ya CDC (Center for Disease Control) halafu mtu anashutukia anatembelewa na mtu wao! Mtu atasumbuliwa na simu, visits, halafu medical record yake itachunguzwa we! Nia yao ni kuwa huo ugonjwa usisambzwe kwa watu wengine.
Halafu ulitokea ugonjwa wa West Nile Virus. Huo ugonjwa unasambazwa na mbu. Iliingia na iliua watu wachache. Yaani huo uoga wa mbu ilikuwa balaa. Mpaka walichora katuni ikionyesha ndege ya jeshi inatumwa kuua mbu moja! Caption ilisema (West Nile Mosquito sited!) Walikuwa wanapuliza miji mizima na mapori dawa ya kuua mbu kusudi waue mbu. Wanadai uliletwa nchini Marekani na ndege iliyotoka Africa. Eti mbu mwenye West Nile alidandia lifti kwenye baggage compartment ya ndege kutoka Africa na alishukia Logan International Airport! Basi hata ndege zilizotoka Afrika zilikuwa zinapulizwa dawa mara wakifungua mlango wa baggage compartment!
Kutokana na huo uwoga waBongo ma waafrika wengi wamegunda ni bora kusema unaumwa UKIMWI kulikoni usema unaumwa Malaria! Kuna MBongo alifukuzwa kazi baada ya kutoka likizo Tanzania. Alirudi na malaria, kachukua off (sick days) siku mbili. Aliporudi kazini, na bosi kamwuliza alikuwa anumwa nini. Jamaa bila kusita alijibu kuwa alikuwa na Malaria! Loh! Yule bosi aliogopa nakumfukuza kazi mara moja eti alihofu ataambukiza watu wafanyakazi ofisini huo ugonjwa. Na hata mwafrika akienda hospitalini USA analalamika anaumwa malaria utaona wafanyakazi, manesi na hata madaktari wanamkwepa na kumtenga na wagonjwa wengine. Sijui wanadhania malaria ni ugonjwa wa aina gani! Wnagejua hiyo malaria ndio common cold ya waafrika!
Na tusisahau tishio la SARS mwaka juzi! Mbona waChina wenye Restaurants hapa USA walilia shauri ya kukosa wateja! Watu kwenye TV na magazetiu walidai ukienda Chinatown au kula Chinese food unaweza kupata SARS! Jamani! Na kweli watu hawakwenda huko!
Haya nimegusia hayo mgonjwa mengine, lakini leo hii naona watu hapa USA wanahofia hiyo Bird Flu. Halafu wanadai kuna chanjo lakini ni watu wachache wanaoipata, ni wenye hela ya kulipia na watu wakubwa yaani wenye vyeo. Wanasomba hiyo chanjo ya Tamiflu na kampuni mwenye patent haitaki makampuni mengine yaitengeneze generic version, ambayo inaweza kuuzwa kwa bei rahisi. Huo ndio ubepari hasa… kujali pesa mbele ya maisha ya binadamu! Kwa sasa hapa Marekani mtu wa kawaida akina kamchape class, tulie tu. Lakini hata hivyo najiuliza kama kuna haja ya kupata hiyo chanjo kweli, na je, Bird Flu ikiingia USA itakuwa hatari kama wanavyotabiri?
WaMarekani wako macho sana. Nyama ya kuku na bata kutoka bara Asia imepigwa marufuku kuingia USA kwa sasa. Kuku, bata, bata mzinga (turkey) wanapimwa kabla ya kwenda kwenye bucha. Na siku akipatikana kuku, bata, au bata mzinga mwenye huo ugonjwa mtasikia, nyama ya kuku hakuna madukani! Maana serikali wata- recall yote na kuichoma moto! Au hata ile nyama iliyo salama, watu wataogopa kununua. Heri tuliyozoea kula maharagwe na mchicha!
Halafu watu wanaotoka barani Asia/ China kwa sasa wanapimwa Airport wakishuka kwenye Ndege. Kama wana dalili ya ugonjwa wanawekwa quarantine. Nasikia hata marubani na ma-air hostess wa Ndege wamembiwa wawe macho kwa watu wanaokohoa au wenye dalili za mafua kwenye ndege halafu wawa ripoti! Juzi juzi hapa USA kuna Mzee wa Kichina alifariki baada ya kurudi kutoka likizo huko China. Walizuia familia yake wasimzike mpaka maiti ilifanyiwa uchunguzi. Lakini kumbe hakufa kwa Bird Flu bail Natural causes, yaani ilikuwa wakati wake.
Halafu hapa USA watu wanapenda kulisha ndege chakula yaani Birdfeeding kama hobby. Wengine wameacha eti kwa vile wanaogopa hao ndege wataleta bird flu kwenye balcony na yard zao. Serikali wamekwisha tangaza kuwa kulisha ndege ni salama, hivyo hakuna haja ya kuacha! Ndege wenyewe hasa ni wa porini na hapa USA kuna akina blue jay, sparrows, robins, njiwa, lark woodpecker, na aina mbalimbali. Wakati wa winter wanapendeza kweli.
Pamoja na yote hayo nashukuru kuwa watu wako macho kwa magonjwa tishio. Na ni bora huko Afrika watu wawe makini pia maana ukiingia huko itakuwa balaa. Kwa kweli ukiingia barani Afrika maelfu ya watu watakufa. Hivi waliopewa jukumu la kufuatulia masuala ya Public Health Afrika wanafuatilia kweli? Au wana tumia muda mwingi kwenye miradi kusudi wapate pesa za kutosheleza mahitaji ya familia ya mwezi?
Pamoja na uwoga kuna mengi ya kujifunza kuhusu jinsi wanavyoshughulikia magonjwa yanayohatarisha usalama wa jamii! Mko macho Lakini?
Saturday, November 26, 2005
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Kwanza nchi nyingi Afrika sera za afya ni maneno tu kwenye karatasi. Likija gonjwa lolote tunasubiri wazungu waje "kutusaidia." Hadi leo hii hatujaweza kuwawezesha wanasayansi wetu wawe wanatengeneza chanjo. Kila chanjo inatoka kwa hawa jamaa. Na kawaida huwa chanjo hizi hatuzifanyii utafiti kabla ya kuwasukumia wananchi. Hivi unadhani waafrika wanaweza kupeleka chanjo Ujeremani, Uingereza, au Marekani kisha zikaanza kutumiwa hivi hivi bila kufanyiwa utafiti...tena unaweza kuwa wa miaka na miaka.
Chemi,
Karibu sana kwenye hii dunia ya blogu.Nimependa sana tafakuri yako kuhusu haya masuala ya afya.Ni kweli kabisa kwamba hawa jamaa ni waoga sana linapokuja suala la magonjwa.Ndio maana miili yao imejaa madawa halafu wanashangaa jinsi wanavyokuwa na maradhi ya ajabu ajabu.Suala la uwezo au maandalizi ya serikali yetu kukabiliana na maradhi kama hiyo homa ya ndege ni gumu kulijadili maana mwili unakufa ganzi kabisa nikijaribu kuwaza.Badala ya kupanga mikakati hivi sasa nasikia kuna kongamano kibao zinaendelea juu ugonjwa huu.Sasa kongamano zitasaidia??Karibu sana
Post a Comment