Monday, August 21, 2006

Idi Amin Hajambo?



Sisi waTanzania hatutasahau ushenzi wa aliyekuwa Dikteta wa Uganda marehemu Idi Amin Dada. Lazima yuko motoni kwa mauaji aliyofanya akiwa kiongozi wa nchi hiyo. Lakini alivamia nchi yetu Tanzania na kusema eti Kagera ni sehemu ya Uganda. Ndipo Mwalimu Nyerere kaja juu na kutuma Jeshi la Wananchi na Mgambo kumtoa nduli Idi Amin! Na hatutasahau ile miezi kumi na nane ya shida baada ya hapo ambayo karibu iwe miaka kumi na nane ya shida. Enzi za kukosa sabuni, sukari, na vyakula na bidhaa mbali mbali madukani na sokoni! Lakini asante Nyerere huyo kichaa kafukuzwa Uganda maana maiti zilikuwa zinajaa Ziwa Victoria mpaka watu walikataa kula samaki kutoka pale!

Leo nimepata habari kuwa kuna sinema itatoka mwezi ujao (Septemba) kuhusu Dikteta Idi Amin wa Uganda. Sinema hiyo inaitwa, ‘The Last King of Scotland’.

Sinema ilipigwa Uganda na mcheza sinema maarufu hapa Marekani, Forrest Whittaker, ndiye anaigiza kama Idi Amin. Mcheza sinema mrembo, Kerry Washington anaigiza kama mmoja wa wake za Amin. Sinema hiyo inasubiriwa kwa hamu na wengi na tayari wanazungumzia habari za ma Oscar kwa ajili ya Forrest Whittaker na Kerry Washington.

Uzuri sinema ilipigwa Uganda kwa ruksa ya Rais Yoweri Museveni. Alitoa msamaha ya kodi mbali mbali kwa ajili ya watengeneza sinema waliokuwa na bajeti ndogo ya kutengeneza hiyo filamu. La sivyo wasingweza kuitengeneza. Alikubali kuwa hatimaye sinema hiyo inaweza kusaidia kuongeza utalii Uganda.

‘The Last King of Sctoland’ inatoka tarehe 26 Septemba. Kwa habari zaidi someni hapa.

Bonyeza hapa kuona Trailer ya sinema: THE LAST KING OF SCOTLAND

9 comments:

Simon Kitururu said...

Lakini ningependa Waafrika wawewanapata guigiza sehemu nyeti za sinema hizi ambazo huzungumzia Afrika.Maana naona Danny Glover alicheza Mandela, hatashangaza mara Denzel Washington akacheza Nyerere...

Chemi Che-Mponda said...

Kaka Simon,

Nakubaliana na wewe 100 percent! Na kweli tunaweza kushangaa kuwa Denzel anaigiza kama Nyerere! Lakini tatizo ni kuwa wanasema eti sinema haitauzwa Marekani kama haina 'Name Actor' yaani mwigizaji anayejulikana.

Dawa ni sisi waafrika kuanzisha film network yetu. Na kwa maana hiyo lazima tuwe na distribution network pia. Maana hollywood bado wanai-monopolise!

Mija Shija Sayi said...

Chemi umesema kweli.

Jaduong Metty said...

Chemi,

Hawa watu wanamglorify Idd Amin au lengo la filamu hasa ni nini? Mimi nawaza tu hapa..pengine wenzangu wasanii (nikiwa na maana nzuri ya neno hilo, Mzee Sitta asije akanitafuta kama Mzee Kifimbo Cheza)mnaweza mkawa mpepata "artistic angle" ambayo sijaipata.

Anonymous said...

Nina hamu ya kuiona hii filamu. Huenda hii filamu ikaikumbusha dunia kuwa Tanzania iliwahi kufanya kitu Marekani inataka kufanya kule Iraki bila mafanikio. Wenyewe wanaita: regime change. Tanzania ilifanya "regime change" kule Uganda. Ikamuondoa rais aliyekuwa madarakani na kuweka madarakani marais wengine watatu (kama sijakosea) waliofuatia. Huenda Marekani inatakiwa kuja kwetu kutuuliza tulifanikiwa vipi.

Chemi Che-Mponda said...

trio kaka,

Idi Amin Dada Ooumee alikuwa na majina mengi sana na kajipachika. Moja ndo hiyo The Last King of Scotland.

Mengine ni:

President for Life
Conqueror of the British Empire
Big Daddy
Lord of All the Beasts and Earth
The Butcher of Uganda
The Butcher of Africa

Kuhusu acting kuna casting process. Lakini kuna kitu nimegundua hapa USA. Wako tayari kumchukua mMarekani na accent fake, kwa vile anajulikana, kuliko actor mwenye accent authentic.

Anonymous said...

Filamu ya Idi Amini usishangae ikaja ikauza na kumpa umaarufu. Kuna principle moja ambayo sometimes ina kera, kwamba scandals, sex and controversy sell. Hawa wanaotayarisha filamu huwa wanaangalia funny and peculiar characters ambazo watu wakiangalia wanabaki na mshangao hilo ndio kubwa wanalolitaka. Mandela na Steve Biko hawa ni watu positive na maarufu filamu zao zimetengenezwa kupitia mtiririko huo huo maana kulikuwa na mauaji, kufungwa na full of actions na ziko marketable.
Kuna sinema ya Idi Amini ilitengenezwaga hapo nyuma i think ilikuwa inaitwa the Rise and Fall of Idi Amin (mnaweza mkanisahihisha kama nimekosea) na Yule actor toka Kenya ilikuwa nzuri tu lakini ilikosa American international exposure sasa wanaitengeneza tena kwa kufuata American principles. Find an actor with a name invest a lot of money advertise it change some lines in the script sell it to the public.

Chemi Che-Mponda said...

Peter,

Ile sinema ya Rise and Fall of Idi Amini ikiwa na Joseph Olita akiigiza kama Idi Amin. Tena alifanana kweli na Amin. Sijiui kama waliwahi kuonyesha kwenye TV lakini unaweza kuipata Blockbuster video. Olita hajulikani USA lakini hiyo ndo sinema bora iliyotengenezwa kuhusu Idi Amin kuliko zote. Yaphet Kotto, na Julius Harris waliwahi kuigiza kama Idi Amin kwenye sinema mbalimbali.

Kwa habari zaidi ya 'The Rise and Fall of Idi Amin' Cheki...

http://www.imdb.com/title/tt0081430

african cocolate said...

nimeiona sinema kwakweli sio mbaya ila i dispised it somehow hasa kwa kitendo cha kusahau Tanzania au kumsahau nyerere kama one of the few leaders in Africa who kicked Idd Amin out of his dictactorior regime, sasa kama theme was to tell the present generation of what happened that time inakuwa haina maana kama hawakum-mention nyerere au tanzania, next time american or any person who want to make money out of african history they should take time and read the history kwanza sio kuja ku potray story too, if thats the case waendelee kuact muvi zao za kimarekani na waache filamu zenye touch n meaningful memory kwa waafrika wenyewe,i wonder am i the only one who knows about this fact, au ni wazungu tuu walimwondoa amin??jamani hebu nisaidieni,