Tuesday, August 16, 2011

Unakumbuka SUPA-GHEE?





Wadau, hapo zamani za kale kulikuwa na mafuta ya kupikia Tanzania maarufu yanaitwa SUPA GHEE. Yalikuwa mazuri sana, lakini miaka ya sabini hasa baada ya Vita Vya Kagera, quality ilishuka vibaya mno. Hata hivyo ilikuwa mali kweli kupata SUPA GHEE! Watu walikuwa wanapanga foleni ndefu za makilomita (siyo utani) kuipata. Nyumba zilikuwa zinavunjwa na SUPA GHEE inaibiwa. Supa Ghee ni moja ya bidhaa ambayo wenye uwezo walikuwa wanaunua na mwisho yalikuwa yanuzwa magendo! Mama Mwenye nyumba anatoa kijiko kimoja kwa ajili ya kukaangia mboga halafu yaliyobaki yanafichwa chumbani! Tumetoka mbali wadau. (Picha ya SUPA GHEE kwa hisani ya mdau S.K.)

3 comments:

Subi Nukta said...

Looooo Mama weeee, enzi zile.

Ghafla umenisababisha nikumbuke TanBond!

Sabuni za Kanga, Mbuni, Kuku wapi?

Magendo ya sabuni za Gardenia, Lux, marashi ya kimkebe cha pink/reddish cha LadyGay na poda zake?

Dah, jamani tumetoka mbali, mbali, mbaaali, historia huandikwa hivi kumbe. Kweli mmenikumbusha mbali. Asante SK kwa kumtumia picha da Chemi aliye-post habari.

Anonymous said...

Hizo foleni za Mwalimu acha tu! Familia nzima mnapanga foleni kwa ajili ya robo kilo ya sukari! Sabuni za kuchibua, ugali kwa chumvi au maziwa! Nguo zilikuwa Unifomu, maana Urafiki Mwatex waktitoa basi hakuna kingine! Mitumba ilikuwa hamna! Ukifua nguo zako kutoka Ulaya, kaa uziangalie mpaka zikauke! Mitumba Nyerere aliita Kafa Ulaya kusudi watu wasiwe na hamu nazo na walidai eti zimetiwa sumu kusudi usizae!

John Mwaipopo said...

hapa naona mie mdogo wenu japo sio kwa saana maana kuna vitu navikumbuka kama mafuta ya mkebe