Monday, July 02, 2012

Madaktari Muhimbili Warejea Kazini

Muhimbili National Hospital, Dar es Salaam, Tanzania

MADAKTARI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WAREJEA KAZINI

JULAI 2, 2012


Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.

Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.

Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo

Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.

Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.

Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.

Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..

KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.

Imetolewa na;

Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 1, 2012

1 comment:

Anonymous said...

Kama serikali imeweza kukubali kuongeza mshahara wa wabunge hadi Sh Milioni 10 kwa mwezi, inakuwa nongwa kwa wataalamu wetu madaktari, tena waliosota kusoma kwa miaka lukuki kuokoa roho za wanadamu, sembuse hao wengine mbumbumbu wanaiosinzia bungeni lakini mwisho wa cku wanalamba kitita chote hicho?

Acheni unafiki, serikali tumeipa kazi ya kukusanya kodi ili ituhudumie, ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara mizuri kwa watumishi wetu. kama imeshindwa kufanya hayo, ingatuke tu.! ipishe wengine wajaribu, habari ndiyo hiyo, liwalo na liwe!
Macho ya maiti anayo mzikaji,