Kolonia Santita: Riwaya ya Kiswahili ya
Kijasusi Inayosisimua
Kolonia Santita ni shirika kubwa la
madawa ya kulevya (drug cartel). Panthera Tigrisi ni mfanyabiashara wa madawa
ya kulevya, katili kuliko wote katika Hemisifia ya Magharibi. Kitabu hiki kinahusu
ujasusi, madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa. Ukianza kukisoma hutakiweka
chini kamwe unless kimeisha …
Kitabu hiki kimetungwa na mtunzi
anayekuja juu akiwa ni mjomba kabisa wa mtunzi maarufu wa Riwaya za Kijasusi
Marehemu Elvis Musiba ambaye alitamba na kitabu chake cha kwanza cha 'Njama'.
Enock Maregesi ambaye anaishi na kufanya
shughuli zake kwa Malkia Elizabeth anasema kitabu hiki amekifanyia kazi kwa
umakini na kitaleta mapinduzi kwenye uandishi wa Riwaya za Kiswahili za Kijasusi.
“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi
zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni
makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.” www.goodreads.com
Kwa habari zaidi wasiliana na Enock
Maregesi kupitia ukurasa wake wa Facebook: http://www.facebook.com/pages/Kolonia-Santita/462971887081149 au enockmaregesi.wordpress.com
Kwa wapenzi wa vitabu kaeni mkao wa kula
kwani kiko njiani na kitapatikana kwenye Bookstores zote. Altenatively,
kinapatikana Amazon na Authorhouse.com.
No comments:
Post a Comment