Monday, February 10, 2014

Rais Kikwete Aifariji Familia ya Marehemu Mzee Patrick Qorro


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombelezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam.
Marehemu Qorro ambaye wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwamo Waziri mdogo wa Kilimo na Ushirika na baadaye kuwa waziri kamili wakati wa awamu ya pili, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvuja damu kwenye mzunguko wa kichwa kulikosababishwa na hitilafu ya figo.Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. James Bwana, Marehemu anatarajiwa kuagwa rasmi kesho kabla ya kusafirishwa Jumatano hadi Kijiji cha Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Dkt Martha Qorro na wanafamilia wengine nyumbani kwa  aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72)  aliyefariki  dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI)  jijini Dar es Salaam.

 PICHA NA IKULU

No comments: