Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama
Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa walipokwenda kutoa
pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es
salaam aliyefariki katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es
Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.
Mama Salma Kikwete akiweha saini
katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa
pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es
salaam aliyefariki katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es
Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.
PICHA NA IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaDkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za RambirambiMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, National Electoral Commission (NEC) kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwaMwenyekiti wa Kwanza wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, MheshimiwaLewis Makame kilichotokea katika Hospitali ya AMI TraumaCentre Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifocha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania naMwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) chini ya Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa,Mheshimiwa Lewis Makame ambaye amelitumikia Taifaletu katika Utumishi wa Umma kwa uaminifu, uadilifu,bidii na umahiri mkubwa”, amesema kwa masikitiko RaisKikwete katika Salamu zake.
Katika utumishi wake, Marehemu Jaji Lewis Makame, enzi zauhai wake, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kabla yakuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na baadaye Mwenyekiti wa NECambayo aliiongoza kwa miaka 17 mfululizo hadi alipostaafumwaka 2011. Uongozi wake ulichangia sana kuimarisha amani,utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa katika mazingira mapyaya demokrasia ya vyama vingi vya siasa hapa nchini.“Ni kwa kutambua kipaji kikubwa cha uongozialichokuwa nacho Marehemu Jaji Lewis Makame, Taifa.
No comments:
Post a Comment