Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA Dkt.Agness Kijazi (Katikati) akitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016. Kushoto ni Samwel Mbuya ambae ni Meneja Kitengo Kikuu cha Habari TMA Dar es salaam na Kulia ni Dkt.Hamza Kabelwa ambae ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mamla ka ya
Hali ya Hewa nchini TMA imewatahadharisha Wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali ikiwemo za Uokoaji,
kujiandaa juu ya namna ya kukabiriana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana
na mvua za masika ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.
Mkurugenzi
wa mamlaka hiyo Dkt.Agness Kijazi alitoa tahadhari hiyo juzi Jijini Mwanza,
wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika
kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.
Dkt.Kijazi
alisema kuwa mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza nay a pili
ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika
maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
Alisema Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi nchini, na kwamba
zinaweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka
za uokozi zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Mkutano baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA ilikuwa ikitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.

Bonyeza HAPA Kutazama Semina Kwa Wanahabari.
No comments:
Post a Comment