Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (katikati) akizungumza hii leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu mkoani humo. Mafunzo hayo yalianza juzi Disemba 14,2016 kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Msoma.
Yaliandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa lengo la kuwajengea welezi wanatasinia wa filamu ili kuzalisha kazi zenye ubora na hivyo kukidhi ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi ambapo zaidi ya washiri 200 walionufaika na mafunzo hayo wamepatiwa vyeti. Tayari mafunzo ya aina hiyo yamefanyika mikoa ya Morogoro na Mwanza na yataendelea katika mikoa mingine.
#BMGHabari
Wanatasnia wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Katibu Tawala mkoani humo, Adoh Mapunda, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia hao. Ameahidi kutoa fulana (Tshirt) 250 kwa ajili ya wanatasnia wa filamu mkoani Mara waliohudhuria mafunzo hayo ambapo zitawasaidia hususani kuwa na sare ya aina moja wakikutana kwa pamoja
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, amesema sekta ya filamu ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wanatasnia wake na taifa kwa ujumla hivyo Bodi za filamu mikoani zihakikishe zinasimamia maendeleo ya tasnia hiyo.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, amebainisha kwamba wadau wa filamu wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji wamefundishwa vyema mafunzo hayo ili kuzalisha kazi bora.
Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda (wa pili kulia), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, akipokea cheti cha utambuzi
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Bi.Deograsia Ndunguru, kutoka Chuo Kikuu Dodoma, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari Genoveva kutoka Idara ya Habari Serikalini, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara, Johnson Ibambai, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mara, akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba yake kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari Amicus Butunga, akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya TBC kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari George Binagi akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya 102.5 Lake Fm kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (mwenye suti) na viongozi wengine wakiwa pamoja na washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (mwenye suti) na viongozi wengine wakiwa pamoja na washiriki zaidi ya 200 wa mafunzo ya filamu mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mwigizaji Dan Msimamo kutoka Tarime amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuinua ubora wa filamu mkoani Mara na hivyo kukuza soko lake
Mwigizaji Justar Lucas kutoka Tarime amesema mafunzo hayo yamewaongezea weledi na kutambua kwamba filamu ni ajira na ikitumika vyema husaidia kukuza kipato cha wanatasnia wa filamu na taifa kwa ujumla.
Mwigizaji Innocent Mbalwa kutoka Bunda ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kutoa mafunzo hayo ambapo amesema yatafungua milango mipya kwenye tasnia ya filamu mkoani Mara.
Mwigizaji Jackline James kutoka Musoma amesema mafunzo hayo yamemsaidia kutambua kwamba filamu ni ajira tofauti na alivyokuwa akidhani awali kwamba tasnia hiyo ni sehemu ya burudani.
******************
Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda, amewahimiza wanatasnia wa filamu mkoani humo kuwa wabunifu katika uzalishaji wa kazi zao ili kupanua soko la filamu ndani na nje ya nchi.
Mapunda ametoa rai hiyo hii leo, wakati akihitimisha mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu mkoani Mara, yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini ili kukuza welezi katika uzalishaji wa kazi bora na zenye maudhui yanaykubalika katika jamii.
"Ubunifu ndio unahitajika hivi sasa, watu wengi wanahitaji ubunifu binafsi na siyo "kucopy" na "kupaste" kazi za wengine". Amesisitiza Mapunda na kuongeza kwamba serikali itatoa ushirikiano wa dhati katika kuboresha tasnia hiyo ya filamu kwani hivi sasa hutoa ajira na kukuza uchumi kwa taifa.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Millao, ameziagiza Bodi za Filamu za mikoa kuhakikisha kwamba zinatimiza wajibu wake ipasavyo ili kuboresha zaidi sekta hiyo.
Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisso, amewahimiza wadau wa filamu mkoani Mara wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji walionufaika na mafunzo hayo, kuyatumia vyema ili kukuza soko lao la filamu.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amewasisitizia hao kutumia mafunzo hayo ili kuzalisha filamu na vipindi vya luninga vyenye ubora ili kunufaika na uhitaji uliopo.
Akisoma maazimio ya wanatasnia wa filamu mkoani Mara, Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani humo, Johnson Ibambai, ametaja baadhi ya maazimio hayo kuwa ni pamoja na kuiomba serikali kuweka mitaala ya filamu kuanzia shule za msingi na vyuo vya ufundi VETA ili kusadia utoaji wa elimu hiyo ya filamu.