Saturday, April 11, 2020

JIhadhari na Ugonjwa wa Coronavirus



Mgonjwa wa Coronavirus akipata matibabu hospiatlini
Wadau,  tafadhali jikinge dhidi ya ugonjwa wa Coronavirus (COVID-19).  Huo ugonjwa unaua!   Hauchagui rangi, umri, au kama wewe ni maskini au tajiri!

Shemaji yangu, Dennis Whitlow, amefariki kwa coronavirus hapa Boston usiku wa kuamkia jumatatu. Hakuna aliyeruhisiwa kumwona hospitalini hadi amefariki.   Nafahamu wagonjwa wengi, wengine wamepona, wengine wamefariki!  Kuna babu wa miaka 88 aliyefariki niliyekuwa namfahamu na kijana mwenye afya mwenye miaka 28 ambaye amefariki. Coronavirus hauchagui.

Tafadhali mfuate masharti. Ukae mbali na mtu mwingine, kaeni majumbani na ukitoka funika  mdomo na pua!  Nawa mikono kila mara. Usiguse uso wako.

Kifo cha coronavirus ni sawa na kifo cha maji, mapafu yanajaa maji, mwili unashindwa kupata hewa (oxygen).


Mungu Atunusuru!


Kirusi cha Coronavirus
Kaburi la pamoj a ya waliofuka kwa Coronavirus mjini New York

No comments: