Kwa mara nyingine kupitia mtandao huu tuupendao,ninapenda kuwakaribisha watu wote kutoka Afrika katika mkutano wa kihistoria ambao unaandaliwa na makanisa kutoka nchi mbali mbali za Afrika.Nchi hizi ni Uganda,Ghana,Kenya, Nigeria,Sudan na wenyeji Tanzania. Mkutano huu unawafanya APOSTLE VERNON na Mke wake PASTOR ANN, ambao ni wamiliki wa kituo cha Television cha Agape cha nyumbani Tanzania kuwa miongoni mwa wahubiri wachache kutoka Afrika kuandaliwa mkutano na nchi zaidi ya moja hapa Marekani.
Baadhi ya watumishi kutoka Afrika ambao huwa wanaandaliwa mikutano ya namna hii ni Robert Kayanja kutoka Uganda, Theresia Wairumi kutoka Kenya,Bishop Bismak kutoka Zimbabwe, Bishop Duncan William kutoka Ghana na wengine wachache ambao sijawataja.Kwa ujumla huu ni ukurasa mpya kabisa katika historia ya nchi yetu na kanisa kwa ujumla.Kuanzia wiki ijayo gazeti kubwa la hapa lijulikanalo kama DALLAS MORNING NEWS pamoja na redio station ya KLTY 94:9 FM,Zitaanza kurusha matangazo ya mkutano huu.Tunategemea pia Television ya DAY STAR itamrusha hewani huyu mtumishi wa Mungu pamoja na mke wake siku moja kabla ya mkutano.Ili kuhakikisha tunapeperusha bendera ya nchi yetu vema naomba tuweke uzalendo mbele.Ndugu zangu, naomba mnisaidie kufanya yafuatayo;
-Kwa watanzania ambao watasoma ujumbe huu na wanandugu,jamaa au rafiki katika jiji hili la Texas naomba muwajulishe juu ya mkutano kwa kuwaandikia email au kuwapigia simu kwani huenda wasisome tangazo hili.
-Kama wewe ni member katika FACEBOOK naomba uwakaribishe watu kupitia njia hiyo ya mawasiliano hata kama upo nje ya Marekani.
-Kama una watu maalumu ambao ungependa niwakaribishe na wako huku Marekani naomba unijulishe kwa kuniandikia email.
-Kama utapenda kuhudumu katika mkutano huu kwa njia moja au nyingine pia nijulishe.
-Kama utapenda kuchangia pesa ili kufanikisha maandalizi haya naomba uwasiliane nasi kupitia
JESCA KATARAIYA -972 506 7780 au 972 387 7104(kataraia@hotmail.com)
Kwa mawasiliano zaidi, nipigie au niandikie:
Kwa mawasiliano zaidi, nipigie au niandikie:
PASTOR ABSALOM NASUWA
UMOJA INT'L CHURCH
12727 DALLAS TEXAS,75230
CELL:214 554 7381, 972 780 2668
FAX:972 991 9460

