Showing posts with label Liz Michael. Show all posts
Showing posts with label Liz Michael. Show all posts

Monday, August 06, 2007

Mjue Msanii Chipukizi wa Bongo - Liz Michael

Liz in her costume for Bongoland II scene.
Cameraman Sam Fischer akipozi na Liz Michael baada ya audition yake.


Nilisema siku nyingi kuwa Bongo kuna watu wenye vipaji vikubwa katika mambo ya uigizaji. Na kweli, tulivyokuwa kwenye shoot ya Bongoland II huko Dar, tuliona wengi wenye vipaji. Hata vijana wadogo wamebarikiwa.

Nilikutana na msichana Liz Michael Kimemeta, mwenye miaka 12 tu. Kama uko Bongo huenda umemwona akihosti vipindi vya watoto. Katika sinema ya Bongoland II anaigiza kama mtoto muuza chapati. Alijua lines zake mara moja na kushangaza watu. Nilimwuliza kama mzazi wake alimsukuma katika mambo ya uigizaji na filamu, alisema hapana na alitokea kupenda mwenyewe.

Pia Liz aliweza kuongea kiingereza kizuri sana (alisema alianza kujifunza kiingereza mwaka jana tualipo hama shule) na kuelezea crew kuhusu ndoto yake ya kuifka Marekani na kuigiza katika sinema huko. Akiendelea na moyo wake huenda atafanikiwa.

Thursday, July 26, 2007

Utengenezaji wa Sinema ya Bongoland II mjini Dar es Salaam

Msaidizi wa Josiah Kibira, Chris Audet kutoka Minnesota, akipanga mambo ya shoot. Hapa ni Manzese.

Mama Thecla Mjata anayecheza kama Mama yaka Juma, na Mzee Olotu anayecheza kama Uncle, akitoka kwa hasira ndani ya nyumba. Hapo ni eneo la Tenki Bovu.

Cameraman Sam Fischer, wakiandaa kufanya scene barabarani na Thecla Mjatta na Mzee Olotu.

Hapa ni Manzese. Tulipiga sinema kwenye maeneo hayo. Utatuona tunkimbia maeneo la uchochoroni, hapo ni sehemu moja tulipokimbia. Huyo baba ni Baba Saidi, mjumbe wa eneo hilo la Manzese. Pia alikuwa anakaanga samaki safi sana waliotoka freshi Ferry.


Josiah Kibira akimwelezea actor kuhusu scene ya 'chooni'.

Bongo Child Superstar Liz Michael Kimemeta alicheza kama mtoto muuza chapati. Liz alitueleza kuhusu ndoto yake ya kuja kuacti kwenye sinema za Hollywood. Kwa kweli mtoto ana kipaji. Nilimowna akihosti kipindi cha watoto kwenye TV Bongo.


Hapa wanashoot scene ya 'chooni' hapo Magomeni Mikumi.

Hapa wako Tanki Bovu nyumabni kwa wazee wangu.


Hapa Peter Omari anayecheza kama mhusika mkuu, Juma, akifanya scene na landlady wake anachezwa na mcheza sinema maarufu wa Bongo, Bi Hindu.