Showing posts with label Lowell. Show all posts
Showing posts with label Lowell. Show all posts
Thursday, March 21, 2013
Friday, June 01, 2012
Wednesday, April 23, 2008
Sinema - This Side of the Truth
Leo nilikuwa extra kwenye sinema, THIS SIDE OF THE TRUTH. Stelingi wake ni mwingereza Ricky Gervais. Inapigwa Lowell, Massachusetts na Andover, Massachusetts. Tulikuwa Downtown Lowell, kwenye benki.
Crew wake wengi wanatoka Uingereza. Basi ilikuwa kichekesho watu walikuwa wanalalamika kuwa wanshindwa kuwaelewa wakiongea. Kweli kama umezoeza kiMarekani, kusikia Kiingereza halisi ni shida. Nilikuwa nawatafsiriwa wazungu niliokuwa nao. Wanauliza kasema nini? Nami najibu kasema hivi, na wao wanasema "Oh!". Nami nikasema huenda na sisitukiongea anapatashida kutuelewa.
Picha chache hizi kutoka seti. Haturuhusiwi kupiga picha kwenye seti. Hizi nilipiga baada ya kumaliza shoot. Leo nilikuwa mpita njia, natembea nyuma ya Ricky Gervais. Lakini hasa walitumia gari yangu. Walibadilisha plates. Nikatoka holding (wanapopumzika extras) na kwenda kwenye seti, sikutambua gari yangu mpaka niliona permits zangu kwenye dirisha.
Wanasema wataniita tena. Wiki ijayo nitakuwa kwenye sinema, Mall Cop tena.
Labels:
Andover,
Extra,
Lowell,
Ricky Gervais,
This Side of the Truth
Subscribe to:
Posts (Atom)



