Showing posts with label Miti. Show all posts
Showing posts with label Miti. Show all posts

Monday, April 01, 2013

Utani wa April Fools! Tambi unaota Kwenye Miti

TAMBI UNAOTA KWENYE MITI HUKO USWISI!

Mwaka 1957 BBC walitangaza kuwa Uswisi inavunwa Tambi kwa wingi.  Walisema kuwa wamefanikiwa kumwua mdudu anayeua miti ya tambi (spaghetti weevil) na pia msimu wa baridi (winter) haukuwa mbaya sana, hivyo tambi unaota kwa wingi.  Watu waliaamini na wengine walidiriki, kuuliza wanawezaje kupata mtu wa tambi, ili walime wenyewe!



Kusoma habari kamili BOFYA HAPA:

Tuesday, October 30, 2012

Hurricane Sandy Ilivyotupiga Cambridge, MA!

Wadau, jana Kimbunga Sandy kilipita kwetu. Upepo mkali sijawahi kuona. Hiyo kelele utadhani treni inapita.  Mtaa wa jirani, Howard St., Cambridge, MA walikipata!  Tuliruhusiwa kuondoka kazini mapema jana kwa vile  MBTA walikuwa wanasimamisha huduma ya basi na treni. Nilivyofika Howard St. nilikuwa mitawi ya mti imeanguka na kuponda magari kadhaa. Dirisha zao zilivunjwa.  Leo asubuhi nikapita tena na kukuta usiku mtu wote umeanguka! Yaani imevunjika kwenye kisiki. Bahati mbaya gari iliyokuwa upande wa pili wa barabara umepondwa kabisa! Duh! Lakini uzuri hakuna aliyeumia. Sasa sijui kama bima itamlipa jirani yangu hela ya kutosha kununua gari nyingine.

Tazama picha nilizopiga, Howard St., Cambridge, Massachusetts.


10/29/12 Howard St. Mitawi ya miti imeanguka na kuvunja vio vya magari




10/30/12  Upepo mkali ulivunja ule mti!

Maskini gari ya watu

Mti ulikatika kwenye kwenye kisiki!