Showing posts with label Ms. Thelma. Show all posts
Showing posts with label Ms. Thelma. Show all posts

Saturday, February 06, 2010

The Harlem Renaissance Revisited - Mchezo wa Kuigiza

Mother Africa /Mama Afrika
Linda Henderson akimpaka make-up Joe Banks Jr. (Steve Lucky)

Kushelia, Linda na Catrina walioigiza kama watumwa

Muongozaji (Director) Wetu Lee Smith na Oscar feki tuliyomkabidhi kama shukurani kwa kazi nzuri. Lee aliigiza kama Langston Hughes pia.


Mimi na Ruby Hill tukiwa tumevaa costumes kwa ajili ya Party Scene.


Mimi niligiza kama Mother Africa pia, safari hii. Father Africa alikuwa David Bowden. Kwa mara ya kwanza walikuwa na Mother Africa ambaye anaongea lugha ya Afrika. Khanga na vitenge nilinunua nilivyokuwa Dar mwezi Novemba. Ungo nilinunua Ubungo TANESCO. Nilikuwa na nyingine ambaye nilikuwa nafanya mazeozi nayo, ilibiwa pale tulipokuwa tunafanya mazoezi! LOL!


Costume yangu ya awali kama Ms. Thelma anayetafuta mapenzi na ana ndoto ya kushinda bahati nasibu.


Mimi na Charles Jackson aliyeigiza kama Joe the Bartender. Mwanzo Ms. Thelman anamkataa Joe, lakini baadaye anamkubali na wanafunga ndoa.



Wadau, jana jioni (Ijumaa) niliigiza katika mchezo wa kuigiza, The Harlem Renaissance Revisited with a Gospel Flavor. Mchezo wa Harlem Renaissance umetungwa na Haywood Fennell Sr.

Thursday, February 04, 2010

The Harlem Renaissance Revisited at Northeastern University

Wadau, kesho nitaigiza katika mchezo wa kuigiza The Harlem Renaissance Revisited with a Gospel Flavor. Role yangu ni ile ile ya Ms. Thelma anayependa kucheza bahati nasibu na mabaye anatafuta mwanaume wa kumwoa.

Kiingilio ni bure, tiketi zinapatika Box Office ya Blackman Theater, Northeasternm University, 360 Huntingto Avenue, Boston, MA. Itaanza 7:00pm (saa moja jioni).

Karibuni!

THE HARLEM RENAISSANCE REVISITED

BLACKMAN THEATER

IN ELL HALL, KRENTZMAN QUADRANGLE

NORTHEASTERN UNIVERSITY

360 HUNTINGTON AVE, BOSTON MA.

FRIDAY, FEBRUARY 5, 2010

STARTS AT 7:00PM.

Monday, May 11, 2009

Tumemaliza Harlem Renaissance Play 2009

Wadau, wiki iliyopita nilikuwa kwenye mchezo wa kuigiza (tamthiliya)hapa Boston. Tulicheza May 7-9. Show ya mwisho ilijaa watazamaji mpaka ilibidi wengine wasimame. Show inahusu kipindi cha Harlem Renaissance miaka ya 1920-39. Ni kipindi ambacho wasanii waMarekani weusi walistawi Marekani na Ulaya.
Mtunzi na Producer wa mchezo, Haywood Fennell Sr. Nyuma yake mnaweza kuona mlango wa stage
Kabla sijavaa costume. Kwenye mchezo mimi niliigiza kama Mama, Bibi na Ms. Thelma.
Joe Banks (Steve Lucky) na Mwongoza mchezo Lee Smith wakitaniana

Ron Murphy (Father Africa) akipumzika Dressing Room kabla ya kwenda stage

Ona nilivyokuwa tajiri kwenye mchezo, binti Sidney ananiibia.

Ron Murphy, Ruby Hill (Bag Lady) na Charles Jackson

Ms. Thelma (Mimi) na Joe the Bartender (Charles Jackson). Kwenye mchezo Joe anampenda Ms. Thelma lakini namkataa halafu baadaye namkubali.

"Mko Tayari!" Mwongoza mchezo Lee Smith na msaisdizi, Stanley Everett (Weldon Johnson) wakihakisha wachezaji wako tayari.

Ms. Thelma
Baba Afrika (Ron Murphy) na Mama Afrika (Irene O'Bannon)

Mimi na Lee Smith (Hapo nimevaa costume ya kwanza. Mimi ni mtumwa na tunafanyakazi shambani, halafu ghafla mwanangu wa kike anachukuliwa kwenda kubakwa, naishia kulia na kuzuiliwa kwenda kumfuata mwanangu)
Mapacha Dariana na Dashiana na Nia (Katikati)

Costume yangu kwenye scenes za mwisho. Ms. Thelma amekubali kufunga ndoa na Joe.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.dotnews.com/2009/harlem-renaissance-revisited-three-shows-lilla-g-frederick

http://oscarmicheauxrep.tripod.com/id13.html