Showing posts with label Richa Adhia. Show all posts
Showing posts with label Richa Adhia. Show all posts

Thursday, September 06, 2007

Maneno ya Hoyce Temu juu ya Ushindi wa Richa

Top Photo from Jiachie Blog
Hoyce Temu (Miss Tanzania 1999)

From Haki Ngowi Blog:

HOYCE Temu, mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, amesema hapingi taji la Miss Tanzania kwenda kwa Richa Adhia kutokana na rangi au asili yake, bali mrembo huyo hana sifa na vigezo vya kuvikwa taji hilo.

Hoyce alisema hayo jana kwenye Ukumbi wa Haidery Plaza, ikiwa ni siku tatu baada ya kufanyika kwa shindano hilo na Richa kuvikwa taji la Vodacom Miss Tanzania 2007.

Muda mfupi baada ya Richa kuvikwa taji, Hoyce alifikia hatua ya kububujikwa machozi kwa kile alichosema na anachoendelea kusisitiza kuwa, mrembo huyo hakustahili kutwaa taji hilo. Kitendo hicho cha Hoyce kilitafsiriwa kwa maana mbalimbali, huku wengine wakimlaumu kwamba mrembo huyo wa mwaka 1999, ameonyesha ubaguzi kwa sababu anampinga Richa kwa asili yake.

Akifafanua msimao wake jana, Hoyce alisema hampingi Richa kwa uasili au rangi yake, bali hakustahili kuvikwa taji hilo, isipokuwa mrembo namba mbili hadi wa tano. Walioshika nafasi hizo katika shindano hilo lililofanyika kwenye viwanja wa Leaders Club ni Lilian Abel, Queen David, Victoria Martine na Khadija Sulla.

Hoyce alisema kilichotokea katika shindano hilo, kinatishia kutekwa kwa maudhui halisi ya uwepo wa shindano hilo nchini kutokana na baadhi ya wadau kujali zaidi lugha ya kigeni katika kujibu maswali.

“Sikuona kigezo chake cha kumfanya achaguliwe kuwa Vodacom Miss Tanzania mwaka 2007, kwani inaonekana wazi wadau kuangalia zaidi lugha ya kigeni katika kujibu maswali baada ya kuipa kipaumbele lugha yetu.“Napenda nieleweke kuwa simpingi Radhia kwa uasili au rangi yake, bali ninahoji vigezo vilivyomfanya hata akavikwa taji kwa sababu hana hadhi aliyopewa ya kuiwakilisha nchi katika shindano la kimataifa,” alisisitiza Hoyce huku akionyesha masikitiko.

Alisema kilichomliza siku ya shindano, si suala tu la Radhia kutangazwa mshindi, pia ni kuona shindano zima la safari hii lilivyokuwa na upungufu mwingi. Hoyce miongoni mwa upungufu huo, anasema ni kukosekana kwa vazi la ubunifu wakati kila wakati imekuwa ikisisitizwa kuhusu suala la ubunifu wa vazi la taifa.

Alisema, hofu yake ni kwamba, kama hali hiyo itaendelea hivyo ya warembo kutoshindanisha ubunifu wao, kuna hatari hata utamaduni halisi wa Mtanzania ukamezwa na ule wa kigeni.

Alisema dosari nyingine ni utaratibu uliotumika katika kuuliza maswali, kwani kwa kawaida kapu la maswali linapopelekwa mbele, huwa halirudi nyuma hadi wote wamalizike, lakini safari hii wakati wa kujibu swali kwa mrembo Victoria Martin, kapu liliondolewa na baadaye karatasi ikatolewa tupu.

“Sipo hapa kwa ajili ya kutaka kumvua taji Richa, isipokuwa nipo kwa ajili ya kurekebisha haya, ili yasije kutokea miaka ijayo.“Na tunachotakiwa ni kuangalia Nancy alipungukiwa vigezo gani hadi kushindwa kuchukua taji la ‘Miss World 2005’, ili tuweze kuchagua ambaye ataweza kujazia vigezo hivyo na kurudi na taji hilo na si kurudi nyuma tena,” alisema kwa uchungu huku akionekana akitaka kulia.

Aidha, alisema kuwepo na utaratibu wa kutangaza mataji, kwani unapotangaza mapema mrembo aliyeshika taji jingine kabla ya taji la Tanzania, unamnyima haki yake ya kupigania taji lake, kwa kuwa atajua hataweza kushinda tena.

Vinginevyo anasema watangaze utaratibu wa kuwa mrembo anaweza kushinda taji la Miss Tanzania hata kama katangazwa kupata taji lingine.Pia alishauri kwa wanaopewa kazi ya kusimamia kambini wanatakiwa kuwa makini kuangalia warembo ambao wanatakiwa kushika taji hilo kwa uhalali

Wednesday, September 05, 2007

Hongera Miss Tanzania 2007







Natoa pongezi kwa mrembo Richa Adhia, kushinda Miss Tanzania 2007. Richa alikuwa pia Miss Kinondoni 2007. Natumaini utatuwakilisha vizuri huko kwenye mashindano ya Miss World, Miss Universe. Siku ya kwanza kumwona Richa nilijua atashinda Miss Tanzania kama majaji watakuwa fair.

Pia natoa pongezi kwa majaji wa Miss Tanzania 2007. Waliweka ubaguzi pembeni na kuangalia sifa za warembo. Nasema hivyo kwa sababu kumetokea mzozo kuhusu asili ya Bi Richa. Yeye ni mTanzania mwenye asili ya kihindi. Lakini ni mTanzania. Kazaliwa Tanzania na kakulia Tanzania na ni nchi yake na yeye hana haya kusema kuwa yeye ni MTanzania.

Mbona kuna waTanzania wengi wenye asili ya kihindi. Tena wengi wanafanya mazuri. Kuna wana siasa kama akina Mheshimiwa Shamim Khan, na marehemu Amir Jamal. Na tunaowaona wengi huko Tanzania ni wafanyabiashara, walimu, na maengineer.

WaTanzania tujifunze kupenda waTanzania wote, awe mzungu, mwarabu, China nk. tuachane na ubaguzi maana ni sawa na ukabila.

Nakumbuka nikiwa shule watu walifundishwa kuchukia wahindi. Nakumbuka kuona mvulana mweyewe asili ya kiafrika akivuta nywele ya mwanafunzi mwenzake mwenye asili ya kihindi. Na tusisahau Rev. Mtikila alivyosababisha wahindi wachukiwe kwa kusema wao ni 'magabachori'. Nadhani sababu moja ya hiyo chuki ni kwa vile kuna wahindi amabao wanajitenga na waafrika na mambo yao yanakuwa siri. Ukienda Carribean utaona wahindi, lakini wako sawa na weusi kwa maongezi, mila, wala hawajioni kama wametoka Asia.

Tukitaka maendeleo tuachane na fikra za kibaguzi tuwe na umoja, tuonyeshe dunia kuwa waTanzania ni tofauti na nchi zingine. Na tumeshafanya hivyo kwa kuishi katika amani miaka mingi. Naomba tuendelee kuwa hivyo.

Pia kuchaguliwa kwa Richa inaweza kuwa ni strategic move mzuri, maana watu wataona kuwa kumbe Tanzania kuna watu wa rangi mbalimbali na tunakaa kwa umoja na amani. Kama Flaviana alivyokuwa na upara na mwaka huu watu watamtazama Miss Tanzania kwa macho mkakubwa, maana watasema hivi Tanzania si African Country?

Richa uendelee na poise yako, na uonyeshe uzalendo wako wakiTanzania huko mbele. Utafika mbali.

Huko Italy walikuwa na Miss Italy mweusi 1996. Mama yake mzungu wa Italy, baba katoka Domincan Republic. Naye alipata upinzani kwa vile alikuwa ni mweusi na watu walisema hawezki kuwakilisha waItaly. Lakini Mungu yupo, waItaly waliungana na kumsupport alivyoshiriki kwenye mashindano ya Miss World. Kwa habair zaidi za Denny Mendez soma:

http://en.wikipedia.org/wiki/Denny_Mendez