Kava ya mbele la gazeti Roswell Beacon (Georgia) iliyotoka May 15, 2008Ukiwa mgombea rais mweusi uko hatarini kuuliwa. Kwa kujua hivyo, Secret Service walitoa ulinzi kwa mgombea rais wa chama cha Democrats mapema. Obama amekuwa akilindwa kwa mieza 18 sasa.
Nchi hii kuna wabaguzi hasa. Yaani white supremacists wanaoamini kwamba mtu mweusi si bindamu na hasthili kuwa na chochote. Huwezi kuamini kuwa mwaka 2008 bado wapo. Sehemu zingine hapa Marekani huwezi kwenda na kuwa na uhakika wa kutoka na maisha yako ukiwa mweusi.
Ajabu, mpinzani wa Obama, Senator Hillary Clinton, amesema kuwa si ajabu watu kugombania nafasi ya mgombea hadi mwezi June, na kusema habari ya kuuliwa kwa Senator Robert F. Kennedy mwaka 1968. Sasa watu wameshutuka! Wametafsiri kuwa Clinton aikuwa na maana kuwa wakimwua Obama, yeye yupo kushika nafasi ya mgombea rais. DUH!
Kwa kweli watu wamemkasirikia Hillary kwa maneno yake.
Kwa habari zaidi someni:
http://blogs.abcnews.com/politicalpunch/2008/05/assassination-d.html
http://afp.google.com/article/ALeqM5jbMPoA_wjG3rgLbbsD-mT30oWfZA
http://ap.google.com/article/ALeqM5g-qGLDs-gAnZiUXD2NU51ry3j3dwD90RJVIO0

