Thursday, September 29, 2005

Barack Obama

Hii ni jambo la kujivinia sisi wana Afrika Mashariki kuwa huenda rais wa kwanza wa Marekani Mweusi huenda akawa Barack Obama ambaye ni Senator huko Illinois. Senator Obama ni hafukasti, mama yake ni Mzungu na baba yake ni Mkenya. Ajabu zaidi ni kuwa mama yake ni mtukuu wa Jefferson Davis ambaye alikuwa Kiongozi wa Confederates. Yaani enzi za utumwa Marekani, Davis alikuwa ni rais wa maConfederates waliochukia weusi na kutaka wabakie katika utumwa na kusababisha Civil War, vita vya wenyewe kwa wenyewe (1860’s). Watu wa Kaskazini hawakutaka utumwa na watu wa Kusini walitaka utumwa udumu. Huyo Jefferson Davis bila shaka anajigueza huko kaburini kwake.

Mwaka jana, Obama alipewa nafasi kuwa keynote speaker katika Democratic National Convention, wana Demokrat walivyomchagua bwana John Kerry kuwa mgombea wa rais katika uchaguzi uliyopita. Na nilishangaa jinsi alivyoweza kuongea na watu kumsikiliza kwa makini kama vile wanamsikiliza Martin Luther King au Mahatma Gandhi. Kila mtu alimpenda na wazungu ndo kabisa sikusikia neno baya juu yake isipokuwa kutoka kwa mpumbavu Alan Keyes (MRepublican) aliyekubaliwa kuwa toi.

Na hivi karibuni alitoa shutuma kali dhidi ya serikali ya Marekani kuhusu Jinsi walivyowasaidia walioathirika na Hurricane Katrina. Bila haya, alisema kuwa serikali ilikuwa legelege na response yao kwa vile walioathirika wengi walikuwa ni weusi na maskini. Katika siku zijazo tufuatilie kawa makini matendo na maneno ya Senator Barack Obama.

5 comments:

Anonymous said...

Last time I checked the guy who genuinely tried to help out Africa did not last! Remember that guy-the Commerce secretary in the Clinton administration (Brown). That is the issue here! Ukitaka kusaidia Africa kwa dhati kabisa wakuua kama walivyomfanya huyu jamaa!!

Anonymous said...

shemeji yangu ananiambia Obama bado ana connections na Kenya na alisha kwenda Nairobi a couple of times .That is good news, I think !
To me kuwa na asili ya Africa ni kazi ya kwanza ya pili na muhimu ni kuwa na connection
I mean wapo wazungu wenye Uafrika zaidi ya waafrika wenyewe if Imake any sence

Anonymous said...

If Africans dont take their continent to the next level NOBODY WILL!!!

Anonymous said...

I got this web site from my friend who informed me
regarding this site and now this time I am visiting this web page and reading
very informative content at this time.

Take a look at my homepage; teeth whitening kits

Anonymous said...

fantastic post, very informative. I ponder why the other experts of this sector don't notice this.
You must proceed your writing. I am confident, you have a huge
readers' base already!

My weblog teeth whitening kit