Tuesday, October 18, 2005

Sinema Mpya - TUSAMEHE

Watu wanangojea kwa hamu sinema mpya iitwayo, TUSAMEHE. Hiyo sinema ni kitoto cha Ndugu Josiah Kibira wa Minneapolis, Minnesota. Sinema hiyo una husu janga la ukimwi kwa sisi waTanzania na Afrika kwa ujumla. Hadithi yake ni hivi, Ndugu Bilantanya kasoma USA na kafanikiwa kupata kazi nzuri, anaoa Mtanzania mwenzake. Lakini anatembea nje ya ndoa na kupata ugonjwa wa ukimwi na kumwambukiza mke wake. Lakini cha kusikitisha mke wake anapata mimba huko Bilantanya anazidi kuumwa. Anaomba aweze kuishi mpaka mtoto atakpozaliwa. Je, atafanikiwa! Kwa habari zaidi nenda kwenye site ya Kibira Films, http://www.kibrafilms.com/tusamehe.

Walioigiza hiyo sinema ni waTanzania waishio USA, na mimi nimo kama Mama Kurusumu. Nilifurahi sana kupewa nafasi ya kushiriki katika hiyo sinema, kwanza sinema kuhusu sisi waafrika hapa USA ni chache. Pia, mimi ni sawa na waTanzania wengine, nina Ndugu, marafiki, majirani na wafanyakazi wenzangu waliokufa shauri ya ukimwi. Kama huo ugonjwa utasaidia kupunguza kasi ya ukimwi au kusaidaia dawa zipelekwe Afrika kusaidia waathirika tutatkuwa tumefanya la maana.

3 comments:

Ndesanjo Macha said...

Sikujua kuwa uko kwenye filamu ya Tusamehe. Juhudi kama hizi (za kutengeneza filamu zetu) zinatia moyo sana.

Chemi Che-Mponda said...

Hi ndesanjo macha,

Asante sana kwa commment. Nimefurahi sana kusikia kutoka kwako maana mimi ni mmoja wa fans wako!

Best Wishes!

Ndesanjo Macha said...

Asante sana. Naona umeibuka kwa nguvu. Uchambuzi huo wa magonjwa nimeupitia. Baadaye itabidi tutazame pia na haya magonjwa "mapya mapya" yanatoka wapi? Ni mkono wa mtu au? Mwanablogu Idya Nkya (http://pambazuko.blogspot.com) huwa anatazama sana pia masuala haya ya magonjwa ya ajabu ajabu.