Friday, March 24, 2006

Nilikuwa 'Busy' Kidogo





Habari zenu wasomaji wapendwa. Kwanza naomba mnisamehe kwa kutokubandika posti mpya hapa siku nyingi. Nilikuwa busy kidogo, na mambo ya uigizaji (acting). Kuna kujitayarisha kwa ajaili ya auditions, na mengine.

Wiki hii nilienda New York City kwa ajili ya Casting Call ya Mo'nique's Fat Chance.
Mnaweza kusoma Blog yangu hapa lakini ni kimombo. Nilikuwa najiona kibonge kumbe hamna kitu, pale nilionekana mwembamba! Nilirudi zangu Boston bila hata kufika raundi ya pili.

http://chemiche.blogspot.com/2006/03/my-experience-at-fat-chance-casting.html


Pia najiandaa kwa ajili ya auditions za sinema kadhaa zitakazo kuwa filmed hapa Massachusetts wakati wa summer. Auditions zina kazi jamani na ni lazima kila mara kufanya mazoezi ya monologues.

Wapendwa Wasomaji, asanteni kwa uvumilivu wenu na naahidi mapya yanakuja!

5 comments:

boniphace said...

Asante na hasa kapicha haka. Sisi twangoja tu ahadi yako kutimizwa. Taarifa kama hizi zinafaa sana maana tunajawa na wasiwasi kuwa unaweza kuwa umeshatukimbia bila kuaga.

Jeff Msangi said...

Kila la kheri.Endelea kutuletea visanga na visa vya hapo kwa Joji

MICHUZI BLOG said...

duh! kumbe bado unadai!!! my offer stands. bring the acting thing here! u can mint money as nigerians do to us with their 'f' class so-called movies. haki ya nani tena!

Chemi Che-Mponda said...

michuzi,

Asante kwa mwaliko! Na kweli mipango yangu ikifanikiwa nitakuwa Bongo kutengeza films.

Anonymous said...

Think twice dada Chemi about kuhamia Tanzania.