Tuesday, March 28, 2006

Ulafi wa Bia Haipendezi Marekani

Ulafi wa Bia Haipendezi Marekani!

Hivi majuzi nilienda kwenye ‘Party’ ya waBongo hapa Boston. Party ilifanyika kwenye basement ya nyumba. Na kama kawaida waBongo walijaa. Na kama kawaida chakula kilikuwa kingi na vinywaji tele. Kwa ‘Party’ waBongo ndo wenyewe maana wanachanga bia na chakula bia shida. Huyo anakuja na kesi ya bia, yule anakuja na kesi, yule anakuja na tray ya mapochopocho, mambo swafi kabisa!

Basi kuna MBongo kashuka kwenye ndege juzi juzi, alikuwa kalala kwenye Lawn Chair ndefu anastarehe huko akipunga upepo wa USA. Jamaa kalala kwenye hiyo lawn chair tena bila wasiwasi wowote, huko anaongea na watu. Nikamcheki, jamaa kalegea kabisa na kikofia kichwani anakula maisha ya USA. Basi chini ya hiyo Lawn Chair alikusanya kama chupa kumi za Heineken.

Nikasogea kwa huyo jamaa kumcheki, kama ni mzima au taira au nini, au labda mtu hajiwezi, ndo maana kalala hivyo. Kuongea na jamaa nikakukuta ni mzima kabisa. Basi nikamwuliza sababu ya kulundika mabia chini ya kiti wakati ziko tele jikoni. Na nikamwuliza kama hapendi bia baridi maana kuziweka chini ya kiti zinapata joto. Nikamwambia jamaa kuwa ni mshamba na anajiaibisha. Jamaa kabisha kasema yeye ana bia tele chini ya kiti atakuwaje mshamba na hawezi kujiaibisha. Hakuwa na habari kabisa kuwa wageni waliokuwepo walikuwa wanamsema chini chini. Lakini jamaa hakujali maana kajiona kafika! Tena kafika USA.

Nadhani watu wangemwona kafika kama hizo bia kununua yeye, na hiyo nyumba ilikuwa yake.

Kwa kweli tabia zingine za Bongo tunaweza kuziacha Bongo. Maana nakumbuka kwenda kwenye shughuli mbalimbali Bongo, na kuona watu wanakusanya bia chini ya kiti. Hiyo kukusanya bia chini ya kiti watu walikuwa wanafanya wakidhania bia zitaisha. At least walikuwa na akiba na rafiki akija wana kitu cha kumpa. Halafu ilikuwa ni sifa kuonyesha kuwa una hela ya kununua bia zote hizo.

Lakini hapa USA bia ziko tele! Kila mahala kuna liquor store na kuna bia tele. Hela yako tu. Na kwenye party za waBongo hata siku moja sijawahi kusikia bia zimeisha, au zikiisha basi watu wanaenda kununua zingine.

Jamani eh, tabisa zingine zinafaa ziachwe huko Bongo. Mnasemaje?

3 comments:

boniphace said...

Chemi umenichekesha sana. Sisi watoto hatuuti hizo Bia bali juisi za Maembe na unajua juisi bomba ni ile inayochanganywa na Ice kiasi fulani huyo wa kuja iulikuwa lazima ushamba huo uwepo tu. Ukukutana naye katika pati nyingine muulize kama atafanya hivyo hivyo...thubutu anaweza kukana kuwa hakuwa yeye

Ndesanjo Macha said...

Chemi, ninakuja pande hizo (Boston) mwezi wa tano. Pengine tunaweza kunywa maji ya madafu pamoja.

Asante umerudi. Uendelee kutupa zaidi kuhusu kazi zako za uigizaji.

Chemi Che-Mponda said...

Kaka Ndesanjo,

Karibu Boston! Holla at chemiche3@yahoo.com so we can hook up.

Kaka Boniface,

Kweli huyo jamaa anaweza kukataa si yeye, lakini wengi walimwona.