Saturday, June 24, 2006

Ni Summer sasa, usije ukapofuka!

Hivi sasa ni kipindi cha joto hapa Marekani, yaani Summer. Joto linavayozidi na nguo watu wanazovaa zinapungua. Wengine wanatembea nusu uchi au karibu uchi kabisa kwa vile eti joto. Wangeonja ule joto wa Tanzania, sijui wangejionaje. Labda wangetembea uchi kabisa! Wanaume wanatembea bila sharti, na wanawake wanatembea na vikaptura na viblausi kama sidiria.

Cha ajabu basi wanatembea barabarani na vinguo vyao bila aibu. Sawa ni mila ya siku hizi kuvaa nguo viduchu hivyo lakini nimeona vituko na lazima niwasimulie.
Juzi nilikuwa Roxbury, yaani ghetto ya Boston. Basi kapita mama fulani mmarekani mweusi, mtu mzima kwa mtazamo wangu labda miaka 50 na zaidi. Alikuwa amevaa kibukta na kablausi. Halafu kanyoa kipara. Uso wake ulikuwa mchanganyiko wa uso wa yule Mwimbaji Seal na yule mgombea wa Uganda Kizza! Yaani alikuwa na uso mbaya! Halafu mapaja na mikono yake ilikuwa imejaa cellulite, nyama zinacheza ovyo akitembea! DUH, alikuwa kama kinyago. Basi anatembea barabarani na watu unaona kabisa wanaona kinyaa. Hivi alijiona mzuri? Angesikia watu walivyokuwa wanamsema, bora angejifunika.

Haya mtaani kwetu Cambridge niliona mzungu mwanamke, huenda ana miaka 60. Basi naye katia kaptura, na blausi isiyo na mikono. Nguo alizovaa hazikuwa mbaya, lakini mama mwenye alikuwa na kitambi, matiti makubwa na hakuvaa sidiria, kwa hiyo akitembea matiti yana ruka hapa na pale. Hiyo blausi haikuwa na mikono na hakunyoa mavuzi kwapani, hivyo nywele zilikuwa zinaing’ingia karibu zifike kwenye kiuno chake! Alikuwa kama katuni! Naye anatembea bila kujali!

Usifikirie kuwa nasema wazee tu. Kuna ma tineja kibao wanavaa hizo vikaptura na visidiria na kujiona wazuri kabisa. Wengine wanapendeza lakini wengine wanaonekana vituko, hasa hao wasio na shepu na wanavaa nguo saizi ndogo wakati wanahitaji saizi kubwa! Hiyo ni kwa sababu hapa Marekani watu wana ugonjwa wa kutaka kuwa wembamba wakati milli yao haitaki. Pia wakienda dukani wananunua nguo eti saizi 8 wakati wanahitaji saizi 12! Basi sababu hizo nguo ndogo manyama yanaing’inginia! Unakuta visichana vidogo vidogo wana manyama nyama lakini kusudi wawe ‘fashionable’ wanavaa hivi vinguo! Hao ambao unawaona kwenye Rap video ni wazuri na wamechaguliwa kutoka kwenye mamia ya wasichana. Lakini hao wanajaribu kuwaiga na kuvaa kama wao kwa kweli! DUH, wanatisha.

Hivi mila ya summer ni kuwa mradi umefunika nyeti zako basi uko sawa? Nimesikia watu wengi, wazungu na weusi, wakilalamika kuhusu jinsi wasichana wasivyojiheshimu na kutembea nusu uchi. Kumbe watu wanajali!

Swali lingine, mbona sioni wanaume wakivaa vinguo nguo?

Haya tungojee baridi uanze tena watu wajifunika na masweta na makoti!

* Nyongeza - Jana nilimwona mama fulani naye katia fola! Huyo ana miaka 35 hivi, ni Mmarekani mweusi, ngozi yake kama ya chui, kuanzia kichwani, hadi miguuni, sijui ni ugonjwa gani! Ni mwembamba na isingekuwa huo ugonjwa wa ngozi angekuwa mzuri, na ana matako makubwa. Basi gauni kavaa shifti, fupi, ina bana anatembea anajiona mzuri! Nguo ilipanda kwenye matako basi ndo mapaja yanaonekana zaidi nayo yako kama ngozi ya chui. DOH! Anatembea na watu wanamwangalia kwa mshangao! Angekuwa Bongo tungemtupia khanga ajifunike!

4 comments:

Anonymous said...

Mimi nimeshafikiria sana kwa kina kuhusu uvaaji huu wa akina dada zetu ila naona sio tu ni fasheni na pia wengine wanatumia summer kama kisingizio. Nimeshajaribu kuwahoji kirafiki wanadada kama 10 wa imani na asili tofauti tofauti kwamba ni kwa nini wanawake wenzao wanapenda kuvaa nguo za kuonesha miili ila jibu sahihi hakuna. Kwa ufupi dada zetu wengine wamekuwa 'mentally disturbed' na fasheni za kileo na tamaduni za 'mjini' zisizo endana na hali halisi. Faida wapatayo kwa uvaaji huu ni ndogo sana ukilinganisha na madhara yake. Ikumbukwe uvaaji huu unatoa tafsiri tofauti kati ya wanawake na wanaume. Hivyo katika kujadili swala kama hili utaona wanawake wanavyolichukulia kirahisi rahisi na kwa mtazamo mwingine ukilinganisha na wanaume.

Jeff Msangi said...

Ukiwauliza wengi watakuambia kwamba vazi hili au uvaaji huu ndio fasheni.Nasema hivi sikatai kwamba vazi hilo au uvaaji huo ndio fasheni.Cha muhimu sana ni kwamba je fasheni hii ni yako?Inaendana na mfumuko wa mwili wako?Lakini wakati mwingine huwa sipendi kuwasema sana,natimiza wajibu wa kuheshimu uhuru wa mtu kufanya analotaka.Ila anapokuwa anatia kinyaa,yabidi aambiwe.

Simon Kitururu said...

Du jana inasemekana Bikini imetimiza miaka sitini.Na ilivyoanzishwa huko ufarasa ilikuwa kasheshe kabla hollywood haijaipa ujiko mpaka ikakubalika

Chemi Che-Mponda said...

Hi Kaka Kitururu,

Hiyo bikini ya miaka ile ungeweza kutembea nayo barabarani leo. Ilikuwa inafunika sana mpaka kitovu. Bikini za siku hizi ni nyuzi tu! Nashangaa mtu anatembea na likamba ndani ya 'crack' ya matako na kujiona kavaa nguo huko nyama zote nje!