Tuesday, June 13, 2006

Usicheze na Wanyama Marekani!

Duniani kuna mambo! Marekani usicheze na wanyama, wakati mwingine wanakuwa na haki kuliko bindamu.

Leo hii jamaa fulani, Christopher Guay (mzungu), kafikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kuua ndege aina ya seagull (wale wa baharini) mjini Boston. Alisema kuwa alimwua kwa vile alikuwa anamsumbua akiwa kazini. Kazi ya Guay ni kuosha madirisha kwenye maghorofa! Lazima mmewaona wanainginia na makamba yao! Kazi hatari hiyo! Na hao seagulls wanakuwa wengi mjini japo bahari ni karibu maana wanatafuta chakula.

Ni hivi kuna mtu kwenye hiyo jengo alimwona na kapiga picha ya tukio. Yule aliyepiga picha kaipeleka kwenye MSPCA (Chama cha Kutetea Haki za Wanyama) nao wakaita polisi. Siku haijaisha Guay kufungwa jela na kufukuzwa kazi. Anaweza kufungwa gerezani miaka mitano!

Cha kushangaza zaidi ni kuwa hiyo habari imeandikwa kwenye kila gazeti, na iko kwenye kila TV stesheni mpaka CNN. Wakati mwingine mtu anaweza kuuawa na habari isiandikwe kwenye gazeti na msione kwenye TV hasa kama marehemu alikuwa ni mweusi.

- Kuna Mfanyakazi mwenzangu mzungu ambaye mbwa wake anaumwa. Jana alitumia nusu siku kwenda kumpeleka hospitali ya wanayama. Leo hakuja kabisa eti anamwuguza. Nisinge jali lakini hapa napofanya kazi kuna mwenzangu MKenya mwenye mtoto mdogo. Mtoto akiugua na inabidi ampeleke hospitalini ni maneno. Mtoto wa mzungu akiumwa wanamwambia atumie muda wowote anaohitaji!

- Nilipokuwa nafanyia zamani mwenzetu alifiwa na paka wake. Wiki mbili nzima anakuja kazini anakaa kwenye deski yake na kulia! Watu walimnunulia makadi, maua na lanchi lakini wapi! Hakufarajika kabisa! Utadhani kafiwa na mtu!

-Kuna MBongo mwenzetu hapa New England alikuwa anafuga mbuzi nyumbani kwake kwa ajili ya kula. Kuna siku majirani zake waliita polisi kwa vile mbuzi moja alitoroka. Polisi waliamua kwenda kufanya ‘search’ nyumbani kwake. Kufika basement wakaona ngozi za mbuzi ambao walichinjwa na kuliwa zamani! Alifungwa jela eti kwa kosa la jinai! Baadaye, baada ya kupata wakili mashitaka yalipunguzwa! Ubaya zaidi walitaka kumnyang’anya watoto wake waliesema eti kama mbuzi anawatesa eti, hao watoto hawako salama!

Hebu mchangie story zenu za wanyama hapa USA!

5 comments:

Jaduong Metty said...

Tatizo ni kwamba hawa jamaa wanapenda wanyama kuliko binadamu. Kuna wakati Humane Society walishutumiwa kwamba wapo tayari kulibebe bango suala la wanyama kuliko watoto wadogo...ukiwauliza watakwambia "it is all relative".

mloyi said...

Rafiki yangu mmarekani aliniambia hao wanaitwa WASP(White Anglo Saxon People) na hizo ndiyo tabia zao. Ubaguzi kwa watu wasio WASP Fikiria wao wanavyotumia muda mwingi kuhudumia wanyama wao na jinsi huyo rafiki yako wa kikenya anavyogombeza akitumia muda kumpeleka MTOTO wake hospitali.
Kujifanya wanajali huku hawajali, Fikiria ahadi za mamillioni ya dola wanzotoa kwa Afrika kupambana na umasikini wakati kwa kuna masikini kupita kiasi. Wanampango wa kuongeza ajira Afrika wakati kwao Ajira ni tatizo kubwa na wanaendelea kupunguza wafanyakazi bila kuwaambia waende wapi.
Huku tunasema wanatupa misaada kidogo lakini mwisho wa siku wanapata faida kubwa kulinganisha na mitaji yao (misaada waliotupa).
Usishangae sana, Walifanya Marshal Plan kwa ajili ya mataifa ya Ulaya yaliyoharibiwa kwa vita ya miaka mitano lakini kwa afrika ambayo imeharibiwa kwa vita na unyonyaji wa wazi kwa zaidi ya miaka mia tano hawaoni haja ya marshal plan.

Chemi Che-Mponda said...

Hi Mloyi,

Kwa kweli wangefanya Marshall Plan kwa ajili ya Afrika.

Kuhusu kupenda wanyama, WASP wako tayari mnyama alale ndani na ndugu yao wa damu alale nje! Hebu sikia malalamiko ya watu waliyokumbwa na Hurricane Katrina! Kuna watu walidiriki kusema ni bora mbwa au paka wao angeokolewa kuliko binadamu! Na wengine wanaona heri kufuga mbwa au paka kuliko kuzaa mtoto!

Anonymous said...

Mimi ninavyoona mahusiano ya binadamu wa hapa Amerikani, ni rahisi sana kupenda wanyama kuliko binadamu. Wewe angalia Wamarekani hawana upendo kati yao bila kuwepo na ulterior motive, mara nyingi urafiki wao ni fake!! Sasa wanyama ndio wana provide refuge kwao emotionally!

Anonymous said...

Bonjour mama,pardon moi pour la terme que je vies de utilise : mama , moi je m appele MPONDA MUANZA , alliace DJENTO , VRAIMENT NA SEPELI MINGI KOMONA PHOTO NA YO ET PUIS SURTOUT PO NA NKOMBO NAYO EKOKAMI NA NGAI ,NA SEPELI MINGI KOSALA COMTACT NA YO , SOKI OKOKI KOKOMELA NGAI , djentomponda@yahoo.fr