Sunday, February 04, 2007

Leo ni SuperBowl - Wanaume wanakuwa Wajinga!

Leo ni siku ya SuperBowl. Yaani msimu wa mchezo wa football unaisha leo. Wanaocheza ni timu za Chicago Bears na IndianapolisColts. SuperBowl inachezwa mji ambayo haina uhusiano na timu wanazoshindana, maana lazima watu wangeuana. Mwaka huu inachezwa Miami, Florida.

Mimi siyo mshabiki wa football wa Marekani. Naona kama wanaumizana, kazi kuangushana. Mara unaona mtu kazolewa kavunjika mguu, mkono au mgongo!

Lakini wanaume hapa USA wanaipenda kweli. Mpaka wasichana wanaotafuta wapenzi, mume wanaambiwa wajifunze kuelewa huo mchezo na itakuwa rahisi kumpata!

Lakini nacho shangaa ni hivi, wanaume wanakuwa wajinga hawajali nini zaidi ya mambo ya hiyo SuperBowl. Wengine wananua tiketi za kwenda huko na mshahara wa miezi kadhaa, mradi wanaenda. Pia TV Kubwa kubwa zinauzwa sana kipindihiki, wanunuzi wakuu wanaume wanaotaka kuangalia Superbowl.

Magazeti, na TV wanaongea habari ya SuperBowl tu mpaka inachosha. Ukienda Grocery store, (dukani) unakuta wanaume wamejaa huko wananunua vyakula vya party kama potato chips, nachos, salsa, chicken wings, cold cuts platters, vinywaji kama soda na bia na nyama za kufanyia barbecue. Hata kwenye baridi unakuta wanaume wako nje wanafanya barbecue. Kwenye football wanita ‘tailgating’

Ajabu wikiendi ya SuperBowl kunakuwa na seli nzuri ya chakula. Mameneja huko Corporate Offices wanakuwa na huruma na kuwapunguzia bei nini? Halafu kila sehemu utasikia kuna SuperBowl party hata majumbani mwa watu. Mabaa zenye TV zinafanya kazi nzuri kweli siku ya SuperBowl.

Niliuliza akina mama wa kizungu kwa nini wanaume wanapenda sana SuperBowl na kupika wao wenyewe siku hiyo. Wakasema ni siku ya mwanaume kuonyesha kuwa ni mwanaume bila kujali wanawake. Haya SuperBowl ikisha watatukumbuka sisi wanawake.

Mama moja kaniambia habari ya chakula fulani wanachopika hao tailgaters, inaitwa jambalaya. Hicho chakula kina wali, sausage, nyanya, vitunguu, pilipili hoho, na viungo kadhaa. Halafu wanatia vipande vya nyama ya kaa. Eti hiyo kaa inaongeza ladhaa. Ukweli eti ina harufu kwa uke wa mwanamke, ndo maana wanaishangalia. Unaona wanaume wananusa halafu wanshangalia. Fikiria mbuzi beberu anvayotanua tanua pua akitaka mambo. LOH!

Hapa Boston timu yetu New England Patriots, hawakufanikwa kwenda. Mbona wanaume walilia machozi walivyoshindwa! Haya tuone nani atashinda Colts au Bears. Na kwa mara ya kwanza timu zote mbili zina kocha mweusi.

UPDATE- Washindi ni INDIANAPOLIS COLTS

Score ilikuwa 29-17.


3 comments:

Unknown said...

duh,yaani hii story umeiandika kama umekaa kibarazani unasimulia.nilivyoanza kusoma nilitaka nisiimalizie nikakuta naendelea mpaka mwisho.cheers!

Anonymous said...

Kweli we Chemi ni mtaalamu wa kuandika. Ninakubaliana kabisa na Zemarcopolo, yaani utadhani tumekaa kibarazani unasimulia hadithi, yaani unavutika kuisoma habari, alfau habari yenyewe ni ya kweli kabisa kuhusu siye wanume na mambo yetu ya SuperBowl.

Alafu hii Blog yako ni babukubwa sana yaani topics zake ni za nidhamu na za kufindisha, tofauti na ile ya Issa Michuzi ambayo wakati mwingine inakuwa na mabo ya kiswahili na majungu. Hii ni yako "Classy" yaani, ndio maana wambeya, watu wenye wivu, na matusi sioni comments!

Hongere sana Dada Chemi

Amani

MICHUZI BLOG said...

amani asante kwa salaam! nitazifikisha kunakohusika....

chemi nasikia fahari kujuana na mtu mwenye kipaji kama chako. naungana na zemarcopolo na amani kukusifia kwa mtiririko wa stori. hata mie nimejihisi niko huko...