Saturday, March 10, 2007

Wasio na Makaratasi wakamatwa Massachusetts

Jamani, wiki hii wasio na makaratasi wana haha hapa Massachusetts. Ni hivi, siku ya jumatatu walivamia kampuni fulani huko New Bedford and kukamata wasio na makaratasi karibu 400! Tena wengi wao walisafirishwa kwa ndege na kupelekwa kwenye makambi ya wasio na makaratasi huko Texas. Watarudishwa kwao (Deported)!

Cha kusikitisha ni kuwa wengi ya waliokamatwa walikuwa na watoto wadogo. Wamebaki bila wazazi, bila mama au baba. Kuna watu ambao wanawaonea huruma na wengine wanasema shauri zao, maana walivunja sheria kwa kukaa USA bila makaratasi. Na mbaya zaidi, waligundua kuna duka iliyokuwa inauza vyeti feki (social security card na green card) kwa dola $120! Wanaesema wakuu wa hiyo kampuni walishirikiana na wenye duka kuwapatia hao wafanyakazi makaratasi feki!

Lakini jamani, walikuwa wanafanya kazi kwa hela ndogo, na kufanya kazi ngumu. Wanaofanya kazi pale wanasema hata ruksa ya kwenda chooni ni shida. Ukichelewa kazini dakika tano unakatwa mshahara. Hiyo kampuni ilikuwa inatengeneza vifaa vya jeshi.

Wengi ya waliokamatwa wanatoka Guetemala, na El Salvador. Sijasikia kama mwafrika alikuwemo.

Unaweza kusoma habari zaidi hapa:

http://business.bostonherald.com/businessNews/view.bg?articleid=187373&srvc=biz

http://biz.yahoo.com/ap/070306/ma_immigration_arrests.html?.v=1

3 comments:

Anonymous said...

Ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye blog yako hii Dada Chemi. Nawapa pole hao ambao hawana makaratasi, Blog yako inafurahisha na nimependa utaratibu wako wa kujibu hoja za watu wanaoingia kwenye blog yako. Inakuwa kama 'conversation' fulani hivi na inaleta raha. Keep it up dada!!

Chemi Che-Mponda said...

Dear Anonymous wa 12:51 am, kwanza asante sana kwa kutazama blogu yangu. Nashukuru na unakaribishwa. Huwa najitahidi kujibu watu, ni mtindo wangu. Ukijibu watu lazima watarudi kusoma umejibuje.

Nasema tena KARIBU!

Anonymous said...

Mpendwa dada Chemi asante kwa kutuletea habari mbali mbali za uko majuu. uwa napitia kwenye blog yako karibu kila siku lakini sijawahi kutoa hoja yoyote. kuhusu hii habari ya uyu waziri wa liberia zinasikitisha sana kuona kuwa Waziri mzima anaweza kufanya vitu kama hivyo cha zaidi ni waziri wa Afrika. asante sana dada Chemi endelea kutupa Michapo zaidi. Maisha mema na malefu kwako. Ubarikiwe