Saturday, February 27, 2010

Wanajeshi wa Marekani Waugua Malaria Haiti

Leo kuna habari kuwa wanajeshi sita wa kiMarekani walioko Haiti wamepata ugonjwa wa homa (Malaria). Na sasa kuna habari kuwa wanajeshi walioenda Afrika pia wameugua, wengine mpaka karibu wafe. Kwa kweli watu wanaanza kuhaha maana wanadhani malaria ni ugonjwa mbaya mno. Sasa hivi mtasikia watu wanahofu kwenda Haiti au Afrika shauri ya kuhofu kuambukizwa malaria.
Ukiumwa malaria Marekani unafungwa quarantine, utadhani una ugonjwa wa ukoma. Nakumbuka MBongo fulani alienda likizo Bongo, alivyorudi alimwambia mwajiri wake kuwa anaumwa malaria, walifukuza kazi mara moja. Mwingine aliiambiwa asirdui mpaka ana cheti cha daktari kuhakikisha ni mzima.

Mnaweza kusoma habari zaidi hapa:

4 comments:

Anonymous said...

Mimi nipo nchi 1 ya Scandnavia. Mwanangu alipata allergy lakini wataalam walisema ni mbu walimuuma tulipokuwa nyumbani. Nimehangaika na mwanangu mwaka 1 na alienda kuponea nyumbani. Hawa watu malaria wanaiona kama ukoma au ukimwi.

Anonymous said...

Ni bora useme una UKIMWI kuliko malaria! Sijui wanaionaje! Kuna mbongo alienda kwenye hospitali fulani emergency eti malaria. Duh! Anasema hata madaktari walikimbia halafu walimweka chumba cha peke yake na waliokuwa wanamhudumia walivaa nguo kama wanasayari!

Anonymous said...

Yalinikuta pia. Ilinibidi nimfundishe kwanza daktari kwamba nina dalili za malaria. Akaenda kumwuliza daktari wa tropical medicine. Ndipo alipokubaliana nami na kuniandikia dawa aliyopendekeza daktari mwenzie. Wiki mbili baadae nikapata follow up call kutoka idara ya afya hapa jimboni. Nikaanza kumwelezea juu ya ugonjwa huo. Afisa huyo akaniuliza mwishoni ninafanya nini hapa nchini. Nikamwambia mimi ni mwalimu. Akauliza kama ninafundisha microbiology. Nikamjibu, la, mimi ni mwalimu wa Kiswahili. Ati "unajuaje habari za malaria hivyo?"

MARKUS MPANGALA said...

ipo kazi hapo, matibabu hadi nini sijui