Saturday, April 10, 2010

Kitabu kuhusu Mwalimu Nyerere




Dear Reader/Mpenzi Msomaji,

MDAHALO KUHUSU KITABU CHA UKOMBOZI WA AFRIKA NA MCHANGO WA MWALIMU NYERERE/ PANEL DISCUSSION AROUND A NEW BOOK TITLED: AFRICAN LIBERATION: THE LEGACY OF NYERERE.

Tembelea Bongo4ever [B4E] katika: http://bongo4ever.ning.com/?xg_source=msg_mes_network

2 comments:

Mbele said...

Ni muhimu sana tuwe na vitabu vya aina hii na makongamano ya kuzikumbuka na kuzitafakari fikra za Mwalimu Nyerere, kwani ni fikra zilizotoa mchango mkubwa kwa nchi yetu, Afrika na dunia kwa ujumla, na bado zinaendelea kukumbukwa na zitaendelea kukumbukwa duniani.

Wa-Tanzania wanajionea wenyewe jinsi watu sehemu mbali mbali wanavyozidi kukumbuka mchango wa Mwalimu na kutoa shukrani zao. Kwa mfano, hivi karibuni pamefanyika kumbukumbu ya Mwalimu kule Uingereza, ambako wa-Tanzania walialikwa. Ilitolewa tuzo kule Umoja wa Mataifa, kwa Mwalimu Nyerere. Kule Darfur wakati polisi wetu wanatuzwa kwa utumishi bora, watoa tuzo walikumbushia sifa za Mwalimu Nyerere. Kule Namibia pia, tumeshuhudia tuzo ikitolewa kwa Mwalimu Nyerere. Ningeweza kuongezea mifano, kama vile Kampala na Cape Town. Hata hapa Minnesota, Wamarekani wameanzisha taasisi ya Mwalimu Nyerere, ambayo itakuwa inaendeleza mchango wake.

Tatizo ni sisi wa-Tanzania, pamoja na CCM, ambayo ilitakiwa iwe inatuongoza katika mambo ya aina hiyo. Hapajawa na mwamko wowote katika CCM wa kuliongoza Taifa katika kumwenzi Mwalimu Nyerere. Badala yake, CCM imekuwa mstari wa mbele kufifisha fikra na mwelekeo wa Mwalimu Nyerere.

Huwa najiuliza, ni viongozi wangapi wa CCM wanavyo vitabu vya Mwalimu Nyerere na wanavisoma? Je ukimbana kigogo wa CCM na akutajie majina tu ya vitabu vinne vya Mwalimu Nyerere ataweza?

Mwalimu Nyerere mwenyewe alianza kuilalamikia CCM wakati hata mfumo wa vyama vingi haujaanza. Kutokana na kukerwa na mambo ya CCM, Mwalimu alifikia hatua ya kujenga hoja kuwa labda vikiwepo vyama vya upinzani CCM itaamka.

CCM haikuamka. Iliendeleza sera za kuvuruga yale yaliyokuwa yameanzishwa na Mwalimu. Mifano ya uvurugaji iko wazi, kama vile Azimio la Zanzibar, ambalo Mwalimu alilishutumu, na mfano mwingine ni sera za huu unaoitwa uwekezaji.

Kuna usemi kuwa nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake. Hayo ndiyo yaliyotokea kwa Mwalimu Nyerere. Ni bora wa-Tanzania tujirekebishe, na kwa msingi huu nakikaribisha kitabu hiki kwa mikono miwili.

zitto kiaratu said...

tatizo la nyerere kama kweli alikuwa anataka tufaidike na vyama vingi vya upinzani kwa nini mali za wananchi/serikali kama vile jumba la ccm dodoma na rasimali nyingi za wananchi zimegawiwa kwa ccm, tatizo la wasomi wa bongo wanafuata upepo kulinda maslahi!!!!