JERUSALEM
Imejengwa kinadhifu, waislamu tujivunie
Mji huu mtukufu, Illaahi tubarikie
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie
Wakati umewadia, jerusalem itun'garie
Rehma kutufikia, na mema tujifanyie
Tuwache yenye udhia, umoja tujivunie
Amani ni fursa, adhim jerusalem tuililie
Masjid al-aqsa, ziara tujifanyie
Mola ameitakasa, Wajibu tujivunie
Al-quds ya sasa, twende tukajionee
Amani ni fursa, adhim jerusalem tuililie
Kwenye Kisa cha miraj, sote tukifatilie
Ardhi na mbigu siraj, Alipita Rasulie
Baada ya ile hajj, Jerusalem tukatembee
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie
Tawhid na imani, sote tujihimizie
Kamba yaa ikhwan, wajib tushikilie
Hii itajenga imani, umoja itupatie
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie
Jamii palestina, ya rabi wajaalie
Subra nayo neema, dhambi uwaghufurie
Uwapatie Rehma, amani uwatandie
Amani fursa adhim, jerusalem tuililie
Shairi si fani yangu, wajibu munikosoe
Hili ni la kwanza langu, hivyo munisaidie
Nakiri makosa yangu, ya illahi nighurufie
Amani ni fursa adhim, jerusalem tuililie
Imetungwa na:
Dr. Amur Abdullah Amur
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
nimelipenda sana shairi hili
Shairi zuri kwa umbo (form) lakini ujumbe wake unategemea ni miwani gani uliyoivaa, kwa Muislamu ni sawa akasema hivyo, lakini si kwa Myahudi na Mkristo na hata kwa anayetafuta suluhisho la kudumu la Mashariki ya kati kwa jamii zote zilizopo hapo.
reDada Chemi
Unataka tuingie kwenye malumbano ya dini?
Mungu utukubalie, maombi yakubalie.
Amani uijalie, mji uubarikie
Dini zote wakulie, umoja uwajilie
Jeruselamu kwa wote, dini zote watukuza
Post a Comment