Wadau, inabidi niwaage! Kuna watu wanaodai kuwa kesho siku ya jumamosi, May 21, 2011 ni mwisho wa dunia! Yaani karibu kila kona unaona tangazo inayoonya kuwa kesho ni mwisho wa dunia. Sasa ni habari kuu kwenye taarifa ya habari.
Wanasema kuwa Bwana Yesu Kristo atarudi duniani kesho, na kutakuwa na tetemeko kubwa mno la ardhi itakayo anagamiza dunia nzima. Hivyo inabidi niwaage. Tutaonana huko mbele.
Habari za mwisho wa dunia zilitabiriwa na Mtume/Mchungaji Harold Camping (90) kutoka California. Aliwahi kutabiri kuwa mwaka 1994 itakuwa mwisho wa dunia.
Huo utabiri wake unawafanya wengine wahaha na wengine wanacheka. Yaani hapa kuna wanaocheka kwa kutokuamini na wengine ambao wanaamini. Leo na kesho kutakuwa na party kadhaa za kusherekea mwisho wa dunia, wengine watakuwa kwenye maombi makali usiku mzima. Kuna waliochimba mahandaki na majumba chini ya ardhi na kuzijaza na maji ya kunywa na vyakula vya makopo. Binamu yangu (upande wa mama) mwenye miaka 94, alinipigia simu na kunionya kuwa kesho ni mwisho wa dunia na hatutaonana tena.
Ila kuna jaama alinifurahisha. Kamwambia mchungaji Camping hivi: Kama kweli siku ya jumamosi, May 21, itakuwa mwisho wa dunia nitakumia dola $5,000. Kama haitakuwa mwisho wa dunia basi nitumie dola $100.
Haya wadau, kazi kwenu!
Kwa habari zaidi za mwisho wa dunia 2011 someni:
4 comments:
Kwa heri Dada Chemi!
he he he he jajimenti dei hinhaaaa!!! huyo pasta atakua chizi au karukwa n,akili anatabiri nini huyo! kazi ipo mwaka huu ngoja tusubirie ya mwaka ni sasa.
jamani nimepita kukujulieni khali tu wikendi njema
Da Chemi upo? Au ndio wote bila kujijua maswala ya intaneti haya twayafanyia ahera?:-)
dada chemi umenichekesha sana ama kweli kama husomi biblia ni rahisi kudanganyika sana, pole kwa wote waliodanganyika na kuhusu mwisho wa dunia, hakuna ajuae siku wala saa ya mwisho wa dunia, Mungu amsamehe huyo pasta anaewambia watu uongo.
by mpenda injili ya Yesu kristo
Post a Comment