Tuesday, July 26, 2011

Rais Kikwete ana SIRI!



Nimeletewa kwa barua pepe (Email), naona ni mambo mazito ya kufikiria:

Kuna siri nzito ambayo mh. JK anayo na ninaamini inamtesa sana. Siri yenyewe ni kama ifutavyo:

Kwamba watu anatuongoza hatutoi msaada kwake. Ninavyoelewa mimi ni kwamba kazi ya Rais sio kufikiri kwa niaba ya watu anaowaongoza. Kazi yake ni kusimamia mahitaji na matakwa ya watu anaowaongoza. Lakini kwa Tz ni tofauti. Kazi ya rais imekuwa ni kufikiri kwa niaba yetu.

Mwl. Nyerere wakati anadai uhuru, aliamini kuwa watanzania ni wanadamu wenye utashi. Akataifisha mali ya wageni na kuwakabidhi wazawa, akiamini tunaelewa kama yeye alivyokuwa. Akatukabidhi viwanda, mashamba, nk. Lakini badala ya kwenda mbele, vikafa. Akashangaa, allah! nilidhani hawa jamaa tu kitu kimoja, kumbe!, akaamua kung'atuka.

Mh. JK akaja na style tofauti. Akasema ngoja niwachokoze, maana siwaelewielewi!
Akaenda kutuombea vyandarua, akiamini kwamba tutalipuka na kusema, haiwezekani, yaani tuombewe vyandarua?! Alitegemea pia kwamba tunatambua kwamba hivyo vyandarua baada ya muda fulani, vitachanika na hivyo tutajiuliza swali, Je! aende kutuombea tena? Lakini cha ajabu, kimyaaa! wote kwa ujumla wetu! Sasa anajiuliza, atumie njia gani ya kutufikishia ujumbe kwamba alitutania/alituchokoza tu ili tuzinduke? Na HATUJAZINDUKA! TUMELALA USINGIZI MZITO! Hivi ni kweli tunafikiri kwamba vikichakaa ataenda tena kutuombea?

Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu na tumeumbwa tuvitawale viumbe vyote(kulingana na maandiko matakatifu). Je! sisi watz tumo? Kama tumo mbona mbu ametushinda? Utashi wetu uko wapi? Kama malaria ndio inaongoza kwa kuleta vifo hapa nchini, tunashindwa nini kumdhibiti mbu na uchafu?

Ukiangalia mbinu tunazotumia kukabiliana na maradhi, utashangaa kabisa! Kuna jamaa walijenga hospitali ya kipindupindu pale buguruni, ajabu! (sina uhakika, lakini inawezekana ni nchi ya kwanza dunia kukijengea kipindupindu ghala la kuhifadhia badala ya kukikomesha). Watanzania mpo!? Kweli mpo?!

Hivi ni kweli tunajisikiaje, kila rais wetu akikaa na marais wenzake, yeye ni kulia kila siku malaria inatumaliza. Si wanashangaa kwamba nchini kwake hana watu? Ni bahati mbaya wengi wetu huwa hatukai chini tukatafakari. JK amekuwa akiuliza maswali kadhaa ambayotungekuwa makini, yangetuumiza. Mojawapo aliwahi kusema, hivi wataalam tunaowapeleka nje ya nchi kusoma, huwa wanasoma nini? Kama ulishawahi kupelekwa nje ya nchi, jiulize ulienda kusomea nini? Kila mtu ajiulize! Baada ya kurudi amefanya nini? Inawezekana vya darasani hukuvielewa, vya kuona pia umesahau? Watu wa mazingira, mpo! wa afya nanyi mpo? manispaa Je!? wa fani nyingine nanyi mliona nini? mliumwa na mbu kule? mliumwa malaria kule? Kama hamkuumwa, mlijiliza ni kwa namna gani mkirudi mtatatua hilo tatizo? Au niwatanie kwamba wengi wetu tukirudi fikra zetu zinabaki kuwaota wazungu na kutamani kuwa kama wao wanavyoonekana na si wanavyotenda. Ndio maana sasa hivi ukitafuta mtu halisi unaweza kupata wakati mgumu.

Nywele kama wazungu! Rangi kama wazungu! Ni hayo tu ndio nayaona tumefanikiwa sana! Wenzetu walishajitambua thamani yao na ndio maana wakajipambanua na kujitofautisha na wanyama wengine kwa sababusi class ya wanyama wengine.

Tukichukua mfano, jiulize kwanini taka zimezagaa kila mahali hasa kwenye miji mikubwa. Taka za kuzagaa zinatakiwa zionekane zile tu zinazozalishwa na mijusi au viumbe visiyokuwa na akili. Wewe mwanadamu unatakiwa utumie akili yako na kuhakikisha kuwa taka unazozalisha huzitupi ovyo. Sasa angalia ambavyo hatutumii akili. Zile taka unaitupa ovyo ukidai huoni dustbin. Taka zile zinazagaa, zingine zinaanguka na kujaa kwenye mitalo. Mvua ikinyesha, maji machafu yanazagaa na kutuletea magonjwa. Tukienda hospital dawa hamna, tunalalamika. Lakini CHANZO CHA TATIZO NI WEWE MWENYEWE! Hapo ndipo wenzetu wanapotucheka, hawa jamaa vipi? utashi wao uko wapi?Ukiwaambia magari yote ya abiria yawe na dustbins, utaambiwa ooh! magari ya wakubwa. Sasa wakubwa si ndio hasa wanatakiwa watuonyeshe njia? Kuliwahi kutokea tangazo la tigo la jamaa kuachwa na gari wakati akichimba dawa, na watu hatukuona tatizo/udhalili wa lile tangazo. Hivi kweli walishindwa hata kusema jamaa akiachwa akimshangaa pundamilia!!!

Niliwahi kuongea na Mh. mmoja kwamba wajitahidi kuwaelimisha watu na kusimamia taratibu zilizowekwa kwa kuwa sasa hivi tuna vituo vingi vya TV na radio, akaniambia ni gharama! Nikashangaa! Tangu lini elimu ikawa rahisi? Au kwa sababu tulisoma bure?Basi tujaribuni ujinga kwa kuwa elimu ni gharama!!!



Tufike mahali tujitambue thamani yetu na kusema tumechoshwa na kunyanyaswa na magonjwa badala ya kila siku tukiumwa, tunakimbilia hospitali bila kujiuliza kwanini tunaumwa. Kauli mbiu ya miaka 50 ya uhuru, kwamba tumethubutu, tumeweza, sijui nini! Huwa najiuliza, tumeweza katika sekta ipi? Vitu vya wachina kujaa madukani ndio kuweza? Used cars za wajapan zilizojaa barabrani ndio kuweza? Elimu down, umaskini juu, magonjwa juu, uchafu juu, vifo juu, michezo down, viwanda down, njaa juu, tumeweza wapi? Kama tumeshindwa hata kufagia, tunaweza nini? Kama unashika ganda la muwa au chungwa na ukalitupa tu ovyo, unaweza nini? Utashi wako uko wapi? Tumelogwa, au ni pepo!?

Kwa mtazamo wangu, badala ya kusema tumeweza, tulipaswa kusema tumetambua tulipoangukia, sasa tunasimama na kuanza hatua ya kwanza. Jamani tutokomeze maradhi kwa kuweka mazingira safi. Kila mtu ajione ni mjinga pale anapotupa taka iwe ni dirishani mwa gari, iwe ni kwenye mtalo, iwe ni kukojoa ovyo, nk. Bila kujitambua sisi wenyewe na kuacha tabia za uchafu kwa mtu mmoja mmoja, magonjwa yataendelea kututesa daima na juhudi zinazofanywa na mamlaka za kufanya usafi kila Jumamosi ya mwanzo wa mwezi hazitaweza kufanikiwa kwa kuwa unaweza ukafagia sasa na mimi nikatupa uchafu dakika 2 zijazo na kufanya usafi uliofanya ukawa bure. Tuwe tunathubutu kuwakumbusha wenzetu pale tunapoona wanakwenda kinyume.

Tatizo kubwa ninaloliona ni kwamba tunaogopa kuthubutu. Kwa mfano jiji la Dar, utaambiwa ni jiji kubwa hivyo ni vigumu. Mimi naona ni rahisi sana. Hivi tukiwachukua wale vijana wanaopiga debe, tuwakawapa vitambulisho na kuwakabidhi hilo jukumu la kuwawajibisha watu, unadhani watashindwa? Cha muhimu ni kuwajulisha wahusika kwamba hao vijana watakuwepo mtaani kwa ajili ya kazi hiyo na kila mtu ajue hivyo. Baada ya hapo ni utekelezaji.Nadhani hawawezi kushindwa.Wanachohitaji ni kibali tu na waambiwe wakimkamata wachukue kiasi gani kwa huyo mtu na akibisha wampeleke wapi.

TAFAKARI NA UCHUKUE HATUA!

Mdau TS

1 comment:

Anonymous said...

Jameni jameni jameni, msituchanganye na mada ngumu ukweli mnao marehemu babu nyerere alisema ikulu ni mahala patakatifu na ikulu ni mzigo si sehemu yakukimbilia kuingia hama kwa kutumia rushwa au hila zozote na hakuna biashra yoyote na ukiona mtu anataka kuingilia ikulu kwa kupakimbilia huyo mtu mtu mwogope kama ukoma JE maneno hayo yana mantiki gani,maono gani,hekima gani na mtazamo gani kwa uwongozi wa kikwete. Kweli marehemu babu nyerere fikra zako zinaishi na nitakuandikia barua kukueleza nchi yako onavyoibiwa na watanzania wanavyoteseka serikali imekuwa ya unyanganyi na upendo umepotea ukoloni umerudi tena.