Imeletwa na Mdau YM:
Mimba na Siri ya Precious
MIMBA
Mimba ilitungwa baada ya baba kutoa hongo kwa kimada
Ili kuthibitisha kama ni mimba kweli kimada akatoa rushwa kwa daktari ili apimwe harakaharaka kwa kuwa kulikuwa na msongamano wa wagonjwa
Kila alipoenda kliniki wakati wote wa Ujauzito alitoa 'chai' ili ahudumiwe vizuri na wauguzi na madaktari
Hata wakati wa kujifungua akatoa 'chai' kwa manesi apate huduma safi
BAADA YA KUJIFUNGUA
Baada ya kujifungua aliendelea kutoa hongo awe wa kwanza kuhudumiwa, mwanae awe wa kwanza kuchomwa sindano za Chanjo n.k.
Mwanae akaitwa 'Precious'
ELIMU KWA PRECIOUS
Kuandikishwa chekechekea akatoa hongo ili Precious apate nafasi katika shule nzuri kwa kuwa nafasi zilikuwa chache, Precious anaangalia
Kuandikishwa shule ya msingi mchezo uleule, Precious anaangalia
Tena sekondari akatoa 'Chai' kwa mwalimu wa Hisabati ili Precious apate alama nzuri
Chuo kikuu Precious hali ikawa ngumu, akagawa uroda kwa mkufunzi ili apate alama nzuri
KAZI
Precious akagawa uroda ili apate kazi, akapata
Precious akatishiwa mara kwa mara kufukuzwa kazi kutokana na utendaji mbovu kinga ikawa ni kugawa uroda
Akatumia nafasi yake kwa manufaa yake binafsi
Kwa tamaa ya vitu vya thamani kuliko mshahara wake akaendelea kupokea rushwa
NDOA
Kwa kuwa wazazi wake (baba yake) hakuwa mwaminifu katika ndoa yake (Precious ni mtoto wa kimada), naye Precious hakuona sababu ya kuwa mwaminifu ktk ndoa
Watoto wake wote walifuata mlolongo kama wa kuzaliwa kwake
KIFO
Hata alipougua ghafla , hongo ikatumika apate huduma bora lakini Mungu alimpenda zaidi
Walipoenda kuchonga jeneza, wakakuta kuna order nyingi ikabidi watoe 'Cha Juu' ili kuchukua jeneza lilokuwepo tayari
Wakati wa mazishi Kwaya iliyotakiwa kuimba wakati wa Maombolezo ilikuwa na safari , ikapewa 'cha juu' ili kuahirisha safari
MWISHO
Kwaya ikaimba na Kumsifia Precious alivyokuwa 'mtumishi mwema wa Mungu', tena wakamwomba Mungu ampokee kwa mikono miwili , amuepushe na Moto wa milele.
Risala ikasomwa, na kusifia utumishi wake uliotukuka, tena kaacha pengo lisilozibika.
TAKE HOME MESSAGE
Wazazi 'huwapakaza' watoto wao matope ya dhambi toka pale mimba inapotungwa hata baada ya kuzaliwa
Watoto wote huakisi tabia walizojifunza toka kwetu, kama wazazi (Observational Learning)
Kama hatuwezi kuwa wawazi hasa pale kaburini hata kwa mtu aliyekufa na sifa mbaya akasifiwa basi tunahalalisha matendo mabaya aliyoyafanya marehemu.
Ili Kupambana na Rushwa twahitaji kuanzia wakati wa Ujauzito, mtoto azaliwe bila rushwa, akue bila rushwa n.k
KWA LEO NI HAYO TU!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment