Saturday, September 15, 2012

Maandamano Bongo Kupinga Filamu Inayodhalilisha Waislamu


Wadau, hiyo sinema. "Innocence of Muslims'  haikutengenezwa kwa idhini ya serikali ya Marekani.  Mtu yeyote Marekani anaweza kutengeneza sinema bila idhini ya serkali. Na pia FBI wanasema kuwa mtengenezaji alitumia jina feki, Sam Bacile ambaye katengeneza sinema kadhaa za ngono (Porn).  Kwa sasa Nakoula Basselly Nakoula  yuko rumande. Mnaweza kusoma habari za kufungwa kwake HAPA.  

Nakoula Basseley Nakoula aka Sam Bacile (mwenye kitambaa cheupe usoni) akipelekwa rumande usiku wa kuamkia leo

Kutoka Blogu ya Wananchi:

WAISLAMU WAJAJUU TENA,SASA NI NCHI NZIMA

WAISLAMU nchini, wanatarajia kuandamana wiki ijayo kupinga filamu iliyotengenezwa nchini Marekani na kumdhalilishaji Mtume Muhammad. Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, alipokuwa akizungumza na MTANZANIA kwa simu.

Kutokana na hali hiyo, Shehe Ponda amelitaka Jeshi la Polisi nchini, kutojihusisha kwa namna yoyote na harakati za kuzuia maandamano hayo.

Sheikh ponda alisema kuwa, baada ya filamu hiyo ya Marekani kumdhalilisha Mtume Muhammad, waislamu hawawezi kukaa kimya na badala yake watalazimika kuandamana kupinga udhalilishaji huo.

“Maandamano hayo yatakuwa ni ya nchi nzima, lakini kwa sasa siwezi kusema yatafanyika siku gani kwa sababu tunafanya maandalizi ya kuyafanya wiki ijayo. Najua kwa kuyasema haya, kuna watu wengine watajitokeza kuyazuia, tunatoa wito kwao mapema waache kutuingilia katika mambo ambayo ni haki yetu na tuna uhuru wa kuyafanya. Jeshi la Polisi litambue wazi kwamba, sisi waislamu hatuna fujo, ni vema wakae pembeni kabisa waache tuandamane na kutoa tamko letu, vinginevyo ni kuanzisha machafuko. Leo nimewashangaa sana hawa polisi, wamefika mahali pa kulinda watu wanaofanya maovu, nimeshangazwa na kitendo cha kuweka ulinzi katika ofisi za makao makuu ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na katika ofisi za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA). Tena katika ulinzi huo, polisi walikuwa na silaha, nashangaa sana, yaani mtu anayefanya makosa, badala ya kumkamata anaendelea kulindwa, hii haiwezekani,” alisema Shehe Ponda.
Alisema kwamba, filamu hiyo iliyotengenezwa na Wamarekani, inachochea uhasama na chuki baina ya wafuasi wa dini mbalimbali.

Kwa mujibu wa Shehe Ponda, filamu hiyo inadaiwa kutengenezwa na raia wa Israel mwenye uraia wa Marekani na kwamba imejenga mtazamo mbaya ndani ya jamii yote duniani.

Hata hivyo taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari zimemtaja mtengenezaji wa filamu hiyo ya Innocence of Muslims ni Sam Bacile, ambaye aliitayarisha kwa idhini ya Serikali ya Marekani.

Taarifa hizo zimeeleza kwamba, mtengenezaji huyo amejificha kusikojulikana, ambapo Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) na Vatcan, zimelaani filamu hiyo inayomvunjia heshima Mtume Muhammad.

*******************************

Kutoka NEW YORK DAILY NEWS:
 
LOS ANGELES (AP) - Authorities say federal probation officers have interviewed a Southern California filmmaker linked to an anti-Islamic movie inflaming protests across the Middle East.

A Los Angeles County Sheriff's spokesman said early Saturday that 55-year-old Nakoula Basseley Nakoula was interviewed at the department's Los Cerritos station.

 Deputy Don Walker says Nakoula was not arrested and traveled voluntarily in a squad car with deputies to the station, which is near his home.

   Walker says he doesn't have information on the interview or how long it lasted.

   TV station KC says Nakoula went to the station early Saturday morning.

  Federal probation officials couldn't be reached early Saturday. Earlier they said they were investigating the activities of Nakoula, who has been convicted of financial crimes.

1 comment:

Anonymous said...

Fact of the matter is, mainstream religions have reduced the value of important figures in their religions and Islam continues to revere those important figures. Everyone here would be up in arms if someone made a video like that about their mother or father, yet Muslims are being condemned for having respect for someone that they truly love and admire. Then this stupid film takes that disrespect to another echelon and even is in violation of youtube's terms and conditions.

Furthermore, it is clear that its purpose is to incite violence, which is a worse crime than the violence itself so it should be banned on that basis alone. It is based on the imaginations of individuals who want to take an already unstable situation in the middle east and make it a worse and want to create a rift between Muslims and Christians. Come on, everyone knows that the film is funded by Jews.

I am a Muslim, and I condemn the film, those who incite violence, and the violence and deaths cause by this incident. Yes, the video should be taken down merely upon its intent to disturb the peace and because it is a seriously blatant and uncalled for disrespect to a revered individual to billions of Muslims worldwide.

This is coming from an American living in Egypt, This film and its aftermath is putting me and my family's lives in danger. I may have to leave and return to the states if the anti-American sentiment grows any further.