Thursday, November 29, 2012

Tanzia - Freddy Mtoi wa BBC


Asante Kaka Freddy Macha kwa kuleta taarifa hii:

SALA, KUAGWA NA MAZISHI YA MWANAHABARI FREDDY MTOI- LONDON NA DAR ES SALAAM…

The late Freddy Mtoi
  haa ya Kiswahili ya BBC London inawaarifu wapenzi wa BBC, ndugu, jamaa na marafiki hasa walioko Uingereza kuwa, ibada ya kumuaga mtangazaji wake Fred Mtoi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 17 Novemba 2012 itakuwa Jumamosi tarehe Mosi Disemba 2012.
Ibada hiyo itafanyika katika Kanisa la St. Anne’s Lutheran mjini London kuanzia saa tano kamili asubuhi.
Anuani ya Kanisa ni: St Anne’s Lutheran Church, Gresham Street, London, EC2V.

 Safari ya kuupeleka mwili wa marehemu Dar es salaam nchini Tanzania itakuwa Jumatatu tarehe 3 Disemba 2012 jioni kwa ndege ya Shirika la British Airways.
Mwili unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jumanne saa moja asubuhi.
Mipango ya Ibada na mazishi nchini Tanzania inafanyika nyumbani kwa wazazi wake Tabata Maduka Manne jijini Dar es salaam. Ibada ya kumuaga Fred itafanyika katika kanisa la Lutheran Tabata Kuu saa saba mchana siku ya Jumatano tarehe 5 Disemba 2012. Maziko yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam saa tisa alasiri.
Fred alianza kazi ya utangazaji Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa masomo. Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya Uzamili kuhusu ‘Digital Media’ katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.

 Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na aliyepatana na wote. Alikuwa mtangazaji mtulivu na akishikilia kazi alihakikisha anaimaliza vema.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Fred atakumbukwa kwa umahiri wake katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Shukran za dhati kwa Shirika la BBC kwa kushughulikia na kugharamia mipango yote ya kuusafirisha mwili wa marehemu Fred hadi Tanzania.
Pia shukran kwa wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha mipango ya yote kuhusu msiba huu.
Imetolewa na:
Zawadi Machibya
Mratibu wa Mazishi
Idhaa ya Kiswahili ya BBC
London

Kwa maelezo zaidi piga simu
+44 795 260 7038

Kwa picha  na habari zaidi BOFYA HAPA:

1 comment:

Anonymous said...

RIP Freddy Mtoi