Uwongo mbaya, wadau wakubwa wengi wa makampuni makubwa makubwa Marekani wameambiwa wasisafiri na aina fulani ya simu na laptop. Wanasema kuwa eti wakifika Uwanja wa Ndege tu, pale majasusi wamekwisha copy kila kitu kilichokuwemo humo tena katika sekunde chache!
*************************************
Chansela wa
Ujerumani Angela Merkel amempigia simu Rais wa Marekani Barak Obama baada ya
kupata taarifa kuwa Idara ya Ujasusi ya Marekani imekuwa ikifanya udakuzi wa
mawasiliano ya simu zake za mkononi.
Msemaji wa
serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert amesema serikali ya Ujerumani inahitaji
uthibitisho wa taarifa hizo na kusema kwamba kitendo hicho ni uvunjifu wa
uaminifu.
Naye msemaji
wa ikulu ya White House, Jay Carney amewaambia waandishi wa habari kwamba, Bw.
Obama amemhakikishia Bi. Merkel kwamba, Marekani haikuwahi kusikiliza
mawasiliano ya simu zake na haitafanya hivyo wala kwa siku za usoni japo
haikufafanua kama mawasiliano Bi Merkel yaliyahi
kufuatiliwa.
Wakati huo
Umoja wa Ulaya unaanza mkutano wake mjini Brussels nchini Ubelgiji huku kukiwa
na malalamiko kuhusu majasusi wa Marekani kudaiwa kuingilia mawasiliano ya simu.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment