OHIO: USA, MAMA BISHANGA AMLILIA KUAMBIANA
Nimepokea
kwa huzuni taarifa ya kifo cha msanii mwenzagu wa fani ya filamu
marehemu Adamu Philip Kuambiana, ni pigo kubwa kwa tasnina yetu na kwa
taifa pia kwa kuondokewa na mtaalamu mahiri kama yeye, namuombea
usingizi wa milele wa amani.
Adamu
alikuwa mtoto wa mwalimu Philip Kuambiana mwalimu wangu wa major yangu
chuoni Theater Arts, alikuwa director na producer mkali sana. Na kama
itakumbukwa nilihojiwa mwaka 2001 baada ya kupokea Award ya The Best
Actress wa mwaka wa 2001, nilieleza mengi pamoja na production
tuliocheza mbele ya wabunge na Rais wa kwanza Mwl Julius
Nyerere, Marehemu Mwalimu Philip kuambiana ndie aliidirect, na
alisimamia Nyanja zote, mandhari, costumes, sound, na hata lebasi za
ulibwende (wale tuliokuwa darasa moja mnaikumbuka hiyo?), na alikuwa
very serious kazi inapoanza, alikuwa akitutania kila
tunapoanza mazoezi kuwa kila mtu aende chooni kabisa kwani kazi ikianza
ni moto moja kwa moja, kazi moja tu, na hakika matokeo ya production
zake yalikuwa mazuri sana. Na ndio hapo nilimjua Adamu akiwa mdogo sana
mwaka 1982-83.
Mwaka
2011 niliporudi tz kufunga ndoa ndipo nilipoonana tena na Adamu akiwa
mkubwa kabisa, na tulipanga kuicheza tena jukwaani ile production ya
mtihani wetu wa mwisho, alisema pamoja kuwa alikuwa
mdogo sana lakini anakumbuka ile production ya
mfalme Odepasi (The King Odepus) kutoka kwenye kitabu cha Shake Spear,
ambayo kwa kifupi mfalme Odepas alifungwa miguu na mikono kwenye mti na
kupewa wafugaji wakamtupe mtoni akafe maji, Odepus alikuja kuwa mfalme
baada ya miaka mingi, alimuua baba yake bila kujua kuwa ni baba yake na
alimuoa mama yake na kuzaa nae watoto wawili bila kujua! ni production
nzuri sana na ninasikitika kuwa Adamu amefarika na ndoto ya kuicheza hii
production tena jukwaani sijui ndio vipi! Pamoja na yote namuombea
Amani ya kudumu,
Mwisho nawapa pole kwa familia yake, na kwa taifa Zima.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa; Pumzika kwa Amani Adamu Philip Kuambiana.
Christina Innocent Marolen
Mama Bishanga
OHIO
The Late Adam Kuambana |
No comments:
Post a Comment