Na. Benjamin
Sawe
Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara amewasihi wadau wa
filamu kuongeza ujuzi na kubadilika ili kuendana na mabadiliko yanayotokea
ulimwenguni katika masuala yanayohusu tasnia hiyo hasa katika suala zima la teknolojia
ya uandaaji na usambazaji wa filamu.
Hayo
aliyasema jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa
filamu za Kitanzania kwa njia ya mtandao ambao mfumo huo umebuniwa na kampuni
ya Proin Promotion Limited ya nchi.
Dr.
Mukangara alisema hatua hiyo ni fursa muhimu katika kupanua wigo wa soko na
kuendana na mabadiliko yanayotokea duniani katika kila nyanja ikiwemo mauzo ya
filamu kwa nja ya mtandao.
“Ipo aja kwa
wadau wetu kupanua eneo la mauzo ya kazi za filamu kwa kutumia mifumo ya kisasa
katika usambazaji na uuzaji wa kazi ikiwemo mauzo na manunuzi kwa njia ya
mtandao”.Alisema Dr. Mukangara
Alisema njia
hiyo ikitumiwa vizuri itakuwa na faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha
wadau kuongeza idadi ya wanunuzi wa kazi za filamu kwani zitaweza kuwafikia
watu sehemu mbalimbali ulimweguni kwa urahisi pamoja na kuwawezesha
wafanyabiashara wadogo kushindana na wafanyabiashara wakubwa kupitia kazi
watakazozizalisha.
Alizitaja
faida nyingine nia pamoja na kupata wafadhili na misaada mbalimbali kutoka kwa
wadau wa filamu ulimwenguni ikiwa ni pamoja na kupata faida zaidi kutokana na
kuongezeka kwa idadi ya wanunuzi wa kazi zao.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotion Bw. Johnson Lukaza
alisema kunachangamoto ya jinsi ya kudhibiti maharamia wanaoiba kazi za wasanii
amabazo wanazifanya kwa jasho na manufaa wanayopata huwa finyu.
“Tunatumaini
njia hii huenda ikaleta nafuu ya kipato zaidi kulingana na hali ilivyo sasa kwa
kuongeza wigo wa mauzo ambao kwa sasa utakuwa ni wa urahisi duniani kote”.Alisema
Bw. Lukaza.
Alisema
kampuni yake hainunui haki za msanii bali inampa mrahaba wa kila nakala ambayo
inauzwa ambapo mfumo huo unaongeza kila nakala ambayo itakuwa imenunuliwa hivyo
kumfanya msanii kufaidika kwa kila nakala inayouzwa na kwa wakati wowote
“Sasa hivi
wasanii watapata fursa ya kuuza kazi zao kupitia mtandaoni hata kaziwalizofanya
miaka ya nyuma na kuanza kufaidika tena pamoja na vizazi vyao.”Alisema Bw.
Johson.
No comments:
Post a Comment