Tuesday, May 05, 2015

Sherehe za Madhimisho ya Wakunga Duniani Tanzania

DSC_0056

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi mkoani Mara wakijiaanda kuanza maandamano kutoka Hospitali Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Musoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

DSC_0060

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi wilayani Musoma wakiwa wamekusanyika nje ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma kwenye viwanja vya Mkendo, mkoani Mara.

DSC_0083

Pichani juu na chini ni baadhi ya Wakunga kutoka mikoa mbalimbali ya nchini wakijumuika na wenyeji wao kwenye maandamano ya maadhimisho hayo.

DSC_0086

DSC_0103

Baadhi ya Wakunga wakijumuika na wakinama wa mjini Musoma njiani kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo wakati maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga duniani burudani ya matarumbeta yaliyokuwa yakishereheshe maandamano hayo.

DSC_0108

Wakunga wa kiume kutoka wilaya ya Serengeti wakiwa wamejumuika na wenyeji wao kwenye maandamano hayo.

DSC_0127

DSC_0136

Shangwe zikiendelea kuelekea viwanja vya Mkendo.

DSC_0153

Kinababa nao hawakubaki nyuma waliwaunga mkono Wakunga kwenye maandamano hayo.

DSC_0161

Mkazi wa mjini Musoma mwenye ulemavu aliyejumuika kwenye maandamano hayo akisukumwa na mmoja wa Wakunga kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo zinakofanyika sherehe za maadhimisho hayo.

DSC_0164

DSC_0177

Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa modewjiblog, Zainul Mzige naye alishiriki maandamano hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma mkoani Mara.

DSC_0180

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) Tanzania, Sawiche Wamunza (wa kwanza kulia) akishiriki kwenye maandamano hayo.

DSC_0185

DSC_0222

Mpiga picha wa Clouds TV Ntibashima Edward akiwa amepanda juu ya gari aina ya canter kwa ajili ya kuchukia matukio ya maandanamano hayo.

DSC_0289

Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) wakipokea maandamano kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mjini Musoma, Mkoani Mara. Kutoka kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikali, Dk. Ama Kasangala, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magese Mulongo, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Musoma, Stephen Zelote pamoja na Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Bi. Feddy Mwanga.

DSC_0275

Maandamano kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yakiwasili kwenye viwanja vya Mkendo na kupokea na mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) yakitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma.

DSC_0285

DSC_0293

DSC_0300

DSC_0304

DSC_0307

No comments: