Saturday, September 12, 2015

Mzee Godfrey Mngodo Afariki Dunia

Wadau, nimepokea kwa huzuni habari ya kifo cha Mzee Godfrey Mngodo, aliyewahi kuwa mtangazaji Voice of America na Radio Tanzania.   Mzee Mngodo alikuwa rafiki wa marehemu baba yangu, Dr. Aleck Che-Mponda. Walikuwa wote Voice of America walipoaanzisha Idhaa ya Kiswahili.  Mzee Mngodo pia aliwahi kunifundisha Mass Communication nikiwa mwanafunzi Tanzania School of Journalism.  Mzee Mngodo alinichekesha sana aliponiambia kuhusu ziara ya Mwalimu Nyerere nchini Marekani wakati wa Uhuru mwaka 1961.  Mzee Mngodo alikuwa ni Press Secretary wa ziara.  Basi waandishi wa habari wa USA walimwandama Mwalimu. Mwalimu kachoka na kwa hasira kaanza kuongea kiswahili.  Waandishi ha wakamkimbilia Mzee Mngodo, "eti, anasemaje!'  Mzee Mngodo anasema ilibidi atunge maana  Mwalimua alikuwa anawachamba hao waandishi. 

Poleni sana wanafamilia kwa msiba wa kufiwa na mzee wenu. 

Rest in eternal peace, Mzee Godfrey Mngodo.


Mzee Godfrey Mngodo 1939 - 2015

 Ziara ya Mwalimu nchini Marekani mwaka 1963 akiwa ni Rais wa Tanganyika






 Kutoka Voice of America


Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika inamkumbuka aliyewahi kuwa mtangazji wake Mzee Godfrey Mngodo aliyefariki dunia Ijumaa  Septemba 11.
Godfrey Mngodo alikuwa mtangazaji wa kwanza wa  idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Amerika ilipoanzishwa mwaka 1962 .
Kwa mujibu wa taarifa za mtoto wa marehemu, Kinyemi Mngodo, Marehemu Mzee Godfrey Mngodo amefariki katika hospitali ya Dar Group jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda maradhi ya figo.
Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa mtoto wa marehemu Yombo Vituka jijini Dar es salaam lakini taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Muheza mkoani Tanga.
Mzee Godfrey Mngodo aliyezaliwa Februari 7 mwaka 1939 pia alikuwa miongoni mwa watangazaji wa mwanzo wa iliyokuwa Tanganyika Broadcasting Corporation kabla ya kubadilishwa na kuwa Redio Tanzania Dar es salaam.
Atakumbukwa pia kama mwanzilishi wa chumba cha habari mara kilipoanzishwa kituo cha utangazaji cha Dar es salaam Televisheni , DTV mwaka 1994 na aliendelea kutumikia kituo hicho baada ya kuanzishwa pia kituo cha CHANNEL TEN kama Msimamizi wa habari na baadaye Meneja rasilimali watu mpaka alipostaafu mwishoni mwa mwaka 2008.
Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika inatoa pole kwa ndugu na jamaa na Marafiki wa Marehemu Godfrey Mngodo.

No comments: