Showing posts with label VOA. Show all posts
Showing posts with label VOA. Show all posts

Saturday, August 22, 2020

Waandishi wa Habari wa Voice of America Walazimishwa Kuondoka Marekani!

 


Rais Trump amebadilisha Uongozi Voice of America.  Ni wabaguzi na hawajali watu bali wanalinda maslahi ya Rais  Trump!  Leo tunaambiwa kuwa baadhi ya waandish wa habari VOA watalazimishwa kuondoka nchini kwa vile uongozi wamekataa kushughulikia visa zao za kukaa nchini.

VOA inaajiri waandishi wa habari wengi kutoka nchi mbalmbali ikiwemo Tanzania. Inamilikiwa na Serikali ya Marekani.

**************

Some VOA Journalists Forced to Leave US soon as Visas Expire

WASHINGTON (AP) - More than a dozen journalists with the U.S. government's premier international broadcaster may soon have to leave the United States as their visas expire with no action from the agency's new leadership. Congressional aides say some 16 Voice of America journalists will be forced to return to their native countries in the coming weeks unless the government agrees to either renew their visas or extend grace periods for them to depart. Several of them could face difficulties at home because of their work for VOA, the aides said. The agency has said it's conducting a review of its visa practices but has offered no other details. 

Saturday, September 12, 2015

Mzee Godfrey Mngodo Afariki Dunia

Wadau, nimepokea kwa huzuni habari ya kifo cha Mzee Godfrey Mngodo, aliyewahi kuwa mtangazaji Voice of America na Radio Tanzania.   Mzee Mngodo alikuwa rafiki wa marehemu baba yangu, Dr. Aleck Che-Mponda. Walikuwa wote Voice of America walipoaanzisha Idhaa ya Kiswahili.  Mzee Mngodo pia aliwahi kunifundisha Mass Communication nikiwa mwanafunzi Tanzania School of Journalism.  Mzee Mngodo alinichekesha sana aliponiambia kuhusu ziara ya Mwalimu Nyerere nchini Marekani wakati wa Uhuru mwaka 1961.  Mzee Mngodo alikuwa ni Press Secretary wa ziara.  Basi waandishi wa habari wa USA walimwandama Mwalimu. Mwalimu kachoka na kwa hasira kaanza kuongea kiswahili.  Waandishi ha wakamkimbilia Mzee Mngodo, "eti, anasemaje!'  Mzee Mngodo anasema ilibidi atunge maana  Mwalimua alikuwa anawachamba hao waandishi. 

Poleni sana wanafamilia kwa msiba wa kufiwa na mzee wenu. 

Rest in eternal peace, Mzee Godfrey Mngodo.


Mzee Godfrey Mngodo 1939 - 2015

 Ziara ya Mwalimu nchini Marekani mwaka 1963 akiwa ni Rais wa Tanganyika






 Kutoka Voice of America


Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika inamkumbuka aliyewahi kuwa mtangazji wake Mzee Godfrey Mngodo aliyefariki dunia Ijumaa  Septemba 11.
Godfrey Mngodo alikuwa mtangazaji wa kwanza wa  idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Amerika ilipoanzishwa mwaka 1962 .
Kwa mujibu wa taarifa za mtoto wa marehemu, Kinyemi Mngodo, Marehemu Mzee Godfrey Mngodo amefariki katika hospitali ya Dar Group jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda maradhi ya figo.
Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa mtoto wa marehemu Yombo Vituka jijini Dar es salaam lakini taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Muheza mkoani Tanga.
Mzee Godfrey Mngodo aliyezaliwa Februari 7 mwaka 1939 pia alikuwa miongoni mwa watangazaji wa mwanzo wa iliyokuwa Tanganyika Broadcasting Corporation kabla ya kubadilishwa na kuwa Redio Tanzania Dar es salaam.
Atakumbukwa pia kama mwanzilishi wa chumba cha habari mara kilipoanzishwa kituo cha utangazaji cha Dar es salaam Televisheni , DTV mwaka 1994 na aliendelea kutumikia kituo hicho baada ya kuanzishwa pia kituo cha CHANNEL TEN kama Msimamizi wa habari na baadaye Meneja rasilimali watu mpaka alipostaafu mwishoni mwa mwaka 2008.
Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika inatoa pole kwa ndugu na jamaa na Marafiki wa Marehemu Godfrey Mngodo.

Wednesday, January 27, 2010

Bibi Titi Alivyotutembelea Mwaka 1965


Wadau, nilivyokuwa Tanzania mwaka jana, nilichukua hii picha kutoka nyumbani. Ni wazazi wangu Dr. Aleck & Rita Che-Mponda na marehemu Bibi Titi Mohamed. Naona alikuwa kwenye ziara Marekani. Picha ilipigwa Washington D.C., wakati huo baba alikuwa Mtangazaji wa Voice of America Swahili Service na pia mwanafunzi Howard University. Picha naona ilipigwa 1965, baba anamhoji kwa ajili ya kipindi chake. Nakumbuka kulikuwa na picha Bibi Titi amenipakata lakini sikuiona. Nikiipata mbona nitafurahi mno.

Thursday, January 17, 2008

Msikie mahojiano na Kanumba 1-27-08



Kutoka http://abdallahmrisho.blogspot.com/



Kanumba akihojiwa na mtangazaji wa kituo cha redio cha Voice of America (VOA) na kipindi chake kitarushwa hewani Jumapili ya tarehe 27 mwezi huu jioni saa moja na nusu, kwa wabongo wanaweza kunasa kupindi hicho Radio Tumaini au Radio Free Africa........kazi kwenu!