Na Henry Mdimu
PICHANI JUU: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI.
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) ameiagiza
Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI kuwachukulia hatua watumishi waliobainika
kutumia vyeti visivyo vyao kupata ajira Serikalini.
Mhe. Kairuki aliyasema hayo
jana alipotembelea Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu–UTUMISHI ikiwa ni
muendelezo wa ratiba yake ya kutembelea Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais-Menejimenti
ya Utumishi wa Umma.
“Watumishi wote waliobainika
kupitia Mfumo Shirikishi wa Malipo ya Mishahara ya Watumishi wa Umma (Payroll)
kutumia vyeti visivyo halali kwao wachukuliwe hatua stahiki” Mhe. Kairuki
amesema.
Aidha, Mhe. Kairuki amemtaka Mkurugenzi wa
Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Emmanuel Mlay kutafuta Ufumbuzi
wa kumalizana na tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya kughushi.
“Muwasilishe vyeti vyao Baraza
la Mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki
watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao” Mhe. Waziri alisisitiza.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Leonard Mchau alisema kuwa Ofisi
ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma imehakiki jumla ya watumishi 704 ambao
kati ya hao watumishi 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani wamegundulika
kuwa waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.
Bw. Mchau aliongeza kuwa
baadhi ya watumishi hao walioonekana kughushi vyeti ili kujipatia ajira
Serikalini wamekimbia vituo vyao vya kazi.
Bw. Mchau aliwaasa wananchi
kuepuka mchezo wa kughushi vyeti ili kujipatia ajira Serikalini.
“Ni kosa la jinai kughushi
vyeti kwa lengo la kujipatia kazi hivyo endapo utagundulika umeghushi vyeti
utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.” Bw. Mchau alifafanua.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma inaendelea na zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wote wa
Umma nchini na matarajio ni kuwahakiki watumishi wote.
***************************************************
KUTOKA HABARI LEO
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, ameiagiza Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu (Utumishi) kuwachukulia hatua watumishi waliobainika kutumia vyeti visivyo vyao, kupata ajira serikalini.
Kairuki amesema hayo jana alipotembelea idara hiyo katika muendelezo wa ratiba yake ya kutembelea Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
“Watumishi wote waliobainika kupitia Mfumo Shirikishi wa Malipo ya Mishahara ya Watumishi wa Umma (Payroll), kwamba wametumia vyeti visivyo halali wachukuliwe hatua stahiki,” amesema Kairuki.
Amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu Utumishi, Emmanuel Mlay kutafuta ufumbuzi wa kumaliza tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya kughushi.
“Muwasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao,” alisisitiza.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa RasilimaliwatuUtumishi, Leonard Mchau, alisema kuwa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imehakiki watumishi 704 na kati ya hao, watumishi 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani, waligundulika waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.
Hata hivyo, Mchau aliongeza kuwa baadhi ya watumishi hao waliobainika kughushi vyeti ili kujipatia ajira serikalini, wamekimbia vituo vyao vya kazi. Mchau aliwaasa wananchi kuepuka mchezo wa kughushi vyeti, ili kujipatia ajira Serikalini.
“Ni kosa la jinai kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia kazi, sasa endapo utagundulika umeghushi vyeti, utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,” alifafanua Mchau. Kwa sasa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inaendelea na uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma nchini mpaka kila mmoja atakapohakikiwa.
No comments:
Post a Comment