The Late Jessie Chiume (1960-2016) |
Jumuiya ya Watanzania New York pamoja na
familia ya Marehemu Mzee Kanyama Chiume inasikitika kuwataarifu Msiba wa
Dada yetu mpenzi Jessie Wayasa Chiume (maarufu kama Da Mgeni) uliotokea
ghafla asubuhi ya Jumatano February 24/2016 kwa ajali ya gari huko Mt.
Vernon, NY.
Jumuiya ya Watanzania wa New York
tunasisitiza ushirikiano katika kufanikisha Msiba huu mzito. Tuungane
kuwafariji wanafamilia pamoja na kutoa rambirambi zitakazosaidia gharama
za kumpumzisha Dada yetu kama ilivyo desturi yetu.
Leo hii Ijumaa familia itaendelea kuwapo 44
Fleetwood Ave, Apt 3B, Mt Vernon NY 10552). Kuanzia kesho Jumamosi
February 27 msiba utakwenda Poconos, PA nyumbani kwa Kaka mkubwa wa
marehemu, Ndugu Michael Kwacha Chiume
(Address : 359 Saunders Drive,Bushkill,
PA,18324)
ambako ndipo pia alipo Mama Mzazi wa Marehemu hadi hapo taarifa zaidi za lini na wapi taratibu za mwisho zitakapoelekezwa.
Link ya kutoa rambirambi ni :
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Michael Chiume:# 646-662-6999
Chris Lutinwa :# 614-592-6231
Nathan Chiume:# 646-552-6347
Dada Jessie atakumbukwa na wengi kwa upole,
ukarimu, ucheshi na mapenzi yake kwa Watanzania na wote waliobahatika
kumjua. Da Jessie ametuachia pengo kubwa mno. Mwenyezi Mungu amlaze
mahala pema Peponi. AMEEN.
Mungu ametoa, Mungu ametwaa.
R.I.P Jessica Chiume. We love you, we will miss you.
2 comments:
Rest in peace.
Rest in peace, DADA JESSIE...
Post a Comment