Showing posts with label Ajali. Car Accident. Show all posts
Showing posts with label Ajali. Car Accident. Show all posts

Saturday, March 27, 2021

Concussion Awareness - Habari Zaidi - Ubongo ukiumia




Wangapi mmeanguka na kupoteza fahamu kwa muda?  Au baada ya kuanguka unajiona unazimia zimia

Ni kutokana na kitu kinaitwa Concusssion. Yaani ubongo  unapata shot vile.  Mara nyingi wana michezo waanaathirika, na wanaopata ajali wanaathirika.

Mnaweza kusoma kuhusu Concussion  KWA KUBOFYA HAPA:

Snowboarding Concussion (Everything You Need to Know) (snowboardhow.com)



Kumbuka msanii Steven Kanumba alikufa kwa Concussion baada ya kuanguka na kugonga kichwa nyumbani kwake.  Mnaweza kusoma kuhusu kifo cha Kanumba  KWA KUBOFYA HAPA:

http://swahilitime.blogspot.com/2012/04/kanumba-alikufa-kwa-brain-concussion.html


Saturday, February 27, 2016

Taarifa Zaidi Kuhusu Msiba wa Dada Jessie Chiume USA

The Late Jessie Chiume (1960-2016)
Jumuiya ya Watanzania New York pamoja na familia ya Marehemu Mzee Kanyama Chiume inasikitika kuwataarifu Msiba wa Dada yetu mpenzi Jessie Wayasa Chiume (maarufu kama Da Mgeni) uliotokea ghafla asubuhi ya Jumatano February 24/2016 kwa ajali ya gari huko Mt. Vernon, NY. 


Jumuiya  ya Watanzania wa New York tunasisitiza ushirikiano katika kufanikisha Msiba huu mzito. Tuungane kuwafariji wanafamilia pamoja na kutoa rambirambi zitakazosaidia gharama za kumpumzisha Dada yetu kama ilivyo desturi yetu. 


Leo hii Ijumaa familia itaendelea kuwapo 44 Fleetwood Ave, Apt 3B, Mt Vernon NY 10552). Kuanzia kesho Jumamosi February 27 msiba utakwenda Poconos, PA nyumbani kwa Kaka mkubwa wa marehemu, Ndugu Michael Kwacha Chiume 
(Address : 359 Saunders Drive,Bushkill,
PA,18324) 
ambako ndipo pia alipo Mama Mzazi wa Marehemu hadi hapo taarifa zaidi za lini na wapi taratibu za mwisho zitakapoelekezwa.


Link ya kutoa rambirambi ni : 


Kwa taarifa zaidi wasiliana na:


Michael Chiume:#  646-662-6999
Chris Lutinwa :# 614-592-6231
Nathan Chiume:#  646-552-6347



Dada Jessie atakumbukwa na wengi kwa upole, ukarimu, ucheshi na mapenzi yake kwa Watanzania na wote waliobahatika kumjua. Da Jessie ametuachia pengo kubwa mno. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi. AMEEN.
Mungu ametoa, Mungu ametwaa. 

R.I.P Jessica Chiume. We love you, we will miss you.

Thursday, December 25, 2014

Ajali Yaua Watu Wawili Nzega Chanza Mwendo Kasi na Mvua

 
Gari ndogo ya binafsi ikiwa nyang'a nyang'a na kusababisha watu wawili kupoteza maisha.

Tukio hilo limetokea  karibu na Ziba,ambapo tunaelezwa kuwa gari ndogo imechakazwa vibaya na inadaiwa kuwa inaelekea Burundi.
Taarifa za awali zinasema chanzo cha ajali hiyo ni pamoja na speed ya gari dogo lakini mvua ilikuwa kubwa kiasi cha barabara kujaa maji na kusababisha gari ndogo kugongana na lori la miziogo.
 Ajali iliyohusisha magari mawili imesababisha waliokuwa kwenye gari dogo kupoteza maisha maeneo ya Nzega mkoani Tabora
Taswira ya Lori la mizigo lililogongana na gari ndogo ya abiria.
 

Saturday, December 20, 2014

Mbunge Ishungisa Afariki na Mjukuu Wake

MBUNGE ISHUNGISA AFARIKI NA MJUKUU WAKE

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Mbunge wa Pili , wa Jimbo la Karagwe ambaye alifariki Jana jioni, Laurent Ishungisa , mjukuu wake ambaye ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TIGO, Gody Tibyampasha naye amefariki alfajiri ya kuamkia Leo  Katika eneo la Skansaka karibu na Mitambo ya IPTL Wilaya ya Kinondoni  kwa ajali ya Gari.

Kwa mujibu wa Msemaji wa msiba wa Inshungisa, Medard Birusya  alisema Gody alikutwa na umauti huo wakati akiendesha gari lake wakati akitokea kwenye msiba wa Babu yake Mabibo Hosteli kurudi nyumbani wake Tegeta kupumzika.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa Katika Hospitali ya Mwananyamala.

Birusya akitangaza Ratiba ya misiba hiyo miwili jinsi watakavyoiendesha hivi punde nyumbani kwa Mtoto wa marehemu Ishungisa, Grace Byampanju eneo la Mabibo Hosteli, alisema msiba wa mbunge Ishungisa uliokuwa ukifanyika Mabibo Hosteli kuanzia Kesho asubuhi utaamishiwa nyumbani kwa wazazi wa marehemu Gody eneo la Tegeta kwasababu Mama Mzazi wa Gody ni Mtoto pia wa marehemu Ishungisa.Baba wa Gody ni Daktari Mstaafu  Dk. Dominic  Tibyampasha.

Birusya alisema , Jumatatu miili ya marehemu ambao ni Babu na Mjukuu wake itaagwa Tegeta na Kisha itasafirishwa kupelekwa Wilayani Karagwe kwa ajili ya kuzikwa.

Birusya alisema Mbunge Ishungisa atazikwa Disemba 24 Mwaka huu ,Katika Kijiji Cha Nyakaiga na mjukuu wake marehemu Gody ambaye ameacha Mke na Mtoto wa Miezi mitatu atazikwa Disemba 25 Mwaka huu  Katika Kijiji Cha Kiruruma. Ni masikitiko makubwa.Mungu tunaomba utupe moyo wa subira na uvumilivu maana huyu Israel Mtoa roho za watu anafanyakazi yake bila huruma.

Ishungisa alifariki Disemba 19 mwaka huu, nyumbani kwa mwanae Grace, Mabibo Hosteli baada ya kuugua kwa muda mrefu.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa Katika Hospitali ya Mwananyamala Dar Es Salaam.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 20 Mwaka 2014.

Thursday, August 14, 2014

SUMATRA Mko Wapi? Abiria Wanateseka

 Abiria wakwama njiani zaidi ya masaa 6  abiria ambao walikuwa wanaelekea mwanza na gari la princes shabaha  wamezidi teseka  huku  hawajui hatima yao ya safari
 Gari hilo lenyenamba za usajili T102 AVX  Wamekwama maeneo ya kibamba jiji dar es salamu  huku kina mama na watoto wakizidi teseka



 Mama Huyu Akiteseka na mtoto mdogo
 Abiria wakiwa nje ya basi

Saturday, July 26, 2014

Mwimba Injili Bahati Bukuku Apata Ajali ya Gari!


 
 
 
 
Msanii wa Injili Bahati Bukuku (40) ni miongoni mwa majeruhi watatu wa ajali ya gari iliyotokea iliyotokea leo katika barabara ya Morogoro – Dodoma eneo la ranchi ya Narco Wilaya ya Kongwa .

Majeruhi wengine ni Edson Mwakabungu (31) ambaye alikuwa dereva na Frank Christopher (20).
 
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma David Misime  ajali hiyo ilitokea saa tisa alfajiri.
 
Alisema taarifa za wahusika zinasema kwamba gari walilokuwa wakisafiria Bukuku, IT 7945 aina ya Toyota Nadia likiendeshwa na Edson Mwakabungu mkazi wa Tabata Dar es salaam liliacha njia na kugonga gema baada ya kugongwa na gari inayodaiwa kuwa ni Fuso.
 
Kamanda Misime amesema kwamba Bukuku analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili huku Frank akiwa na michubuko usoni na mkono wa Kulia.
Aidha amesema kwamba watu wote hao wamelazwa  katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
 
 Kwa mujibu wa Kamanda Misime mwimbaji huyo na wenzake walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, huku Bahati Bukuku na Frank Christopher walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la injili.
 
Source: Sifa Lubasi, Dodoma

Thursday, July 17, 2014

Mwanamke Kutoka Kenya Agongwa na Gari na Kufariki Boston

  Wikiendi iliyopita, mwanamke kutok Kenya aligongwa na gari aina ya Pick-Up na Kufariki papo hapo! Tunachijua ni kuwa anaitwa Nancy na alikuwa na miaka 32.

Kutoka WHDH.com 

DORCHESTER, Mass. (WHDH) - A woman was hit and killed by a motor vehicle in Dorchester early Saturday morning.

Officers arrived at the intersection of River Street and Washington Street at around 5 a.m. for reports of a collision where they found the 32-year-old victim with life threatening injuries.

She was transported to Carney Hospital where she later succumbed to her injuries.

Neighbors said she was on her way to work, the first of two jobs, when she was struck. Everyone who knew her raved about her work ethic.

"She worked two jobs," said Carl Cahoon. "She got up at five in the morning went down and got the bus and did her first job."

Cahoon added that there was a purpose behind that work.

"I know she was saving her money to get her son to come back  from Kenya...8-year-old child," Cahoon said. ""Always working, always talking about 'I can't wait to get my son'...she was saving the money to have her son fly here and unfortunately it's not happening now."

Police have not identified the vehicle involved in the crash. Anyone with information is strongly urged to contact the Boston Police Homicide Unit at (617) 343-4470 or leave an anonymous tip at (800) 494-TIPS.

Tuesday, July 16, 2013

Daladala laparamia na kugonga ukuta wa Kanisa la St. Joseph mjini Dar!



Kutoka Wavuti.com


Walemavu wa miguu walijikuta wakiangalia mabaki ya baiskeli zao zilizoharibiwa baada ya kunusurika kugongwa na daladala namba T 989 BCN linalofanya safari zake kati ya Mabibo na Kivukoni lililoacha njia na kuparamia ukuta wa mlango wa kuingilia Kanisa la Mtakatifu Yosefu (St. Joseph) jijini Dar es Salaam leo.

Daladala hilo lilipata ajali wakati likijaribu kukwepa gari jingine dogo lililokata kona bila ya kuchukua tahadhari wakati likiingia katika Kanisa hilo.

Gari lingine dogo lenye namba za usajili T 674 BRL lililokuwa limeegeshwa nje ya Kanisa hilo liliharibiwa baada ya kuangukiwa na ukuta.

Picha, Maelezo: Dotto Mwaibale

KWA HABARI NA PICHA ZAIDI TEMBELEA DA SUBI
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2ZE38gx6S

Thursday, July 11, 2013

Mama Mzazi wa Profesa J Afariki Dunia! Aligongwa na Gari!





PictureBlack Rhyno aliandika haya maneno kupitia ukurasa wake wa facebook

HABARI ZILIZOPOKEWA USIKU HUU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU BAADA YA KUGONGWA NA GARI  MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.

PROFESA J AMETHIBITISHA  HILO MUDA MFUPI ULIOPITA, NA KUSEMA INAMUIA VIGUMU KUAMINI IMETOKEA KWANI ANASEMA MAREHEMU MNAMO SAA MBILI HIVI ALIMPIGIA SIMU NA KUMWELEZA KUWA AMEPATA AJALI NA KWAMBA WAKATI HUO YUKO KITUO CHA POLISI, BILA SHAKA KUPATA FOMU YA PF 3 YA KUMUWEZESHA KWENDA KUTIBIWA HOSPITALI.

"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NA GARI....NJOO NIKO POLISI NAANDIKISHA....MWANANGU NAKUFA....ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU.

ANASEMA WAKATI ANAPIGIWA SIMU NA MAMA YAKE YEYE ALIKUWA KATIKA MGAHAWA WA NYUMBANI LOUNGE, NAMANGA, DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA KATIKA KIKAO NA LADY JAY DEE NA MUMEWE GADNA G. HABASH, AMBAO BAADA YA TAARIFA HIYO WALIMSINDIKIZA HADI HOSPITALI YA TUMBI.

"TULIPOFIKA HOSPITALI SIKUAMINI KUONA BADALA YA KUPELEKWA WODINI AMBAKO NILIDHANI MAMA ATAKUWA AMELAZWA NIKAPELEKWA CHUMBA CHA MAITI AMBAKO NILIMKUTA MAMA AKIWA MAREHEMU", ALISEMA PROFESA J KWA MAJONZI.

GLOBU YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA PROFESA J KWA MSIBA HUU MZITO NA WA KUSIKITISHA. TUNAMWOMBA MOLA AMPE NGUVU YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. 

TUTAENDELEA KUWAPASHA KINACHOJIRI KADRI HABARI  ZAIDI ZITAPOPATIKANA. KWA SASA PROFESA J NA WADAU WENGINE WAKO NYUMBANI KWAKE MBEZI JUU.
source-tzdailyeye 
 
Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake.  Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'
 

Wednesday, November 28, 2012

Sharo Milionea Azikwa Tanga

Bongo Staa, Sharo Milionea aka. Hussein Ramadhani Mkieti (27) amezikwa leo, Muheza, Tanga.  Sharo alipoteza maisha yake juzi katika ajali ya gari mkoani Tanga. Alikuwa anakwenda kuona wazazi wake.  Kabla ya kifo chake, Sharo Milionea alikuwa anapanda kwa kasi katika chati ya Bongo Stars. 

REST IN PEACE SHARO MILIONEA!


Shekhe akimwombea mwili wa marehemu Bongo Staa, Sharo Milionea


Umati walitokea kwenye mazishi ya marehemu  Bongo Staa, Sharo Milionea

Sharo Milionea aka. Hussein Ramadhani Mkieti (1985 -2012)

Sharo Milionea alipoteza maisha yake katika ajali ya gari mkoani Tanga. Alikuwa anaendesha mwenyewe, alikuwa anaeelekea Muheza, Tanga kwenda kuona wazazi wake.

Mnaweza kuona picha zaidi za Mazishi ya Sharo Milionea katika KAJUNA BLOG:

Tuesday, November 27, 2012

Maelezo Juu ya Kifo cha Sharo Milionea


Kutoka: UNIQEENTERTZ  BLOG:


The Late Sharo Milionea aka. Hussein Ramadhan


Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.
Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo. 
 

Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi.

Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.


Baada ya kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika hapakuwa na mwili wa marehemu katika  eneo la tukio,ndipo mama mmoja aligundua mwili wa msanii huyo mita chache kutoka gari ilipogonga mti na kuharibika vibaya.

Mganga mkuu wa hospitali teule ya Muheza amesema kuwa chanzo cha kifo cha Sharo ni kubonyea kwa kichwa ikiambatana na majeraha yaliopo kichwani na sehemu ya mabega ndiyo yalipelekea msanii huyo kupoteza maisha papo hapo.

Hata hivyo jeshi la polisi lilikuja masaa mawili baada ya kutokea ajali hiyo,ambapo gari la Tanesco ndilo lililotumika kuvuta gari hiyo hadi kituo cha polisi wilayani humo.
habari zaidi endelea kuchungulia hapahapa .


Mwili wa Sharo utazikwa kesho saa saba mchana