Saturday, August 27, 2016

Kanisa la EAGT Lumala Mpya jijini Mwanza Kufanya Harambee ya Kanisa Jipya la Kisasa

Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji kiongozi, Dkt.Daniel Moses Kulola, linapenda kuwakaribisha watu wote kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa jipya na la kisasa linalotarajiwa kujengwa katika viwanja vya kanisa hilo.

Harambee hiyo inatarajiwa kufanyika kesho jumapili Agosti 28,2016 kanisani hapo ambapo watu wote wakiwemo waumini na viongozi wa Madhehebu mbalimbali, Viongozi wa Serikali na Taasisi binafsi, wanakaribishwa ili kuungana na viongozi na waumini wa Kanisa hilo katika kushiriki kwenye harambee hiyo.

Kumbuka "Bwana Hufurahi  Anapojengewa Hekalu Lenye Kufana" hivyo utabarikiwa ikiwa utashiriki katika harambee hiyo. Kwa mawasiliano zaidi, tumia nambari za simu; 076774 90 40 AU 0787 74 90 40.

Saturday, August 20, 2016

Mama Bishanga Ndani ya White Party ya Birthday ya Rukia Hussein

Kwa Hisani ya Christina Marolen aka Mama Bishanga


            MAMA BISHANGA NDANI YA WHITE PARTY YA BIRTHDAY YA RUKIA HUSSEIN

Rukia mtoto wa marehemu Sheihk Yahya Hussein aliangusha bonge ya white party kusherehekea miaka 50 ya birthday yake kwenye hoteli babu kubwa ya Marrioti, jijini Cleveland Ohio. Mambo yalikuwa mambo haswaaa!

Rumba lilinoga kwa nyimbo za nchi mbali mbali za Africa na hasa za maarufu home TZ za Bado, number one, bora uende, colors of African, na nasema nae taarabu ambao mume wa Rukia ilibidi awekwe kitini na kukatiwa mauno kisawasawa na mkewe na waalikwa akina Mama Bishanga, Prisca Zenda, Michelle Mujuni nk walipotupia mduara wa nguvu! Wapendwa angalieni picha mpate picha ya mambo yalivyokuwa bam bam! 
        
          HAPPY BIRTHDAY RUKIA MUNGU AKUONGEZEE UMRI, MAFANIKIO, NA
                              FURAHA YA MAISHA YAKO NA NDOA NA FAMILIA YAKO!
Birthday Girl Dada Rukia Hussein Awasili

Mama Bishanga (Kulia) na Birthday Girl



Mashindano ya Miss Mwanza 2016

Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,2016, kulikuwa na mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa taji la MISS MWANZA 2016 ambapo warembo 16 kutoka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza walijitosa kusaka taji hilo.

Ilikuwa ni furaha kubwa kwa mrembo, Mary Peter (katikati), pale alipotangazwa kuwa MISS MWANZA 2016. Pia mwendelezo wa furaha uliwaendea warembo, Victoria Boniphace (kushoto) aliyetangazwa Miss Mwanza nambari mbili na Winnie Shayo (kulia), aliyetangazwa Miss Mwanza nambari tatu.

Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza 2016, kiliandaliwa na Kampuni ya "Big D Entertainment" na baada ya kinyang'anyiro hicho, unafuata mtifuano wa MISS LAKE ZONE 2016 utakaofanyika Septemba 10,2016 ambapo washiriki wa Miss Mwanza 2016 waliongia nafasi tano bora, wanashiriki moja kwa moja kwenye shindano hilo.
Na BMG
Miss Mwanza 2015, Donny Roberty (kushoto), akimkabidhi taji Miss Mwanza 2016, Mary Peter (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.
Washiriki wa Miss Mwanza, walioingia nafasi tano bora
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016.
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Majaji walikuwa na Kazi pevu kuchagua mshindi
Baadhi ya waliohudhuria kwenye tukio
Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza akidondosha burudani kwenye Miss Mwanza 2016
Burudani za kiafrika pia zilikuwepo
Mkali wa Moyo Mashine, Ben Pol, alidondosha burudani poa sana
Ben Pol kazini
Kupitia BMG, Ben Pol, aliwashukuru wakazi wa Jiji la Mwanza kwa namna wanavyopenda kazi zake na kuahidi kufanya kazi nzuri zaidi.
Miss Mwanza 2016 aliiambia BMG kwamba, maandalizi yake mazuri ndiyo yaliyompa fursa ya kunyakua taji hilo na kwamba amejiandaa vyema kwa ajili ya taji la Miss Lake Zone 2016 na pia Miss Tanzania 2016.
Miss Mwanza 2016 nambari mbili akibonga na BMG. Anasema shauku yake ni kuongeza juhudi zaidi ili kunyakua taji la Miss Lake Zone 2016.

Friday, August 19, 2016

Benki ya Dunia Kuendelea Kusaidia Sekta ya Maji Nchini

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua  kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam.
KATIKA kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO). 

Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.

Aidha, Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi. 

Ameeleza kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.

Nimeridhishwa na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia wananchi huduma ya Maji alisema Bi. Bird

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji.

Changamoto ni nyingi katika utoaji wa huduma ya Maji, naamini kuwa kiasi cha fedha kilichotengwa kitasaidia kuondoa changamoto hizo alisema Mhandisi Luhemeja.

Benki ya dunia imekuwa ikifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwamo miradi mbalimbali katika sekta ya Maji, Nishati na Madini, Kilimo na Mifugo, pamoja na Uchumi na Biashara.


Sunday, August 14, 2016

Tanzia - Mh. Mzee Aboud Jumbe

Rest in peace Mh. Mzee Aboud Jumbe. (1920 - 2016)

Saturday, August 13, 2016

Paka Kichaa au Mjanja?


Huyo paka ni mjanja au kichaa? Anakubali kunyonyesha panya ambao ni chakula kikuu cha paka. Au anawanyonyesha ili wanone apate mlo safi?

Mwenyekiti Mpya wa CCM Dr. John Pombe Magufuli Apokelewa kwa Nderemo na Vifijo

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipungia wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kuwahutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifurahia burudani za aina mbalimbali wakati alipowasili Jijini Dar es salaam leo, akitokea Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga ngoma kutoka kwa moja ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi waliofika Uwanjani hapo kumlaki leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndehe wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanaCCM pindi alipowasili Ofisi Ndogo ya Chama hicho, Mchana wa leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndg. Rajab Luhwavi mara baada ya kuwasili Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisaini Kitabu cha wageni kwenye Ofisi Ndogo ya CCM, iliopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikifanya Mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhan Madabiba.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza jambo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana .
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwasalimia wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteja jambo na Wakuu wa Wilaya za Ilala (Sophia Mjema) na Kindondoni (Ally Hapi).