Showing posts with label Mwanza. Show all posts
Showing posts with label Mwanza. Show all posts
Saturday, December 02, 2017
Mwanza Wazindua Mwongozo Kuhusu Uwekezaji wa Mkoa
MKOA wa Mwanza umefanya Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji ambao umeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Mwongozo huo ni sehemu ya ripoti tatu zilizotokana na agizo la mkoa wa Mwanza la kutaka kuwekewa pamoja taarifa sahihi zinazogusa uwekezaji mkoani humo ili kurahisisha na kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
Ripoti nyingine ni Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials Report), na Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report) .
Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, Mashirika ya Umma, Sekta binafsi na mashirika ya kimataifa, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella, alisema walilazimika kuwatafuta wataalamu wa ESRF, kuwasaidia kuweka pamoja fursa zote za mkoa katika mpangilio mmoja unaobainisha fursa zilipo.
[caption id="attachment_3212" align="aligncenter" width="1404"]
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa chini ya ufadhili wa UNDP katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.[/caption]
kwenye viwanja vya ofisi za Mkuu wa Mkoa huo jijini Mwanza.[/caption]
Saturday, October 21, 2017
Mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Eden Jijini Mwanza hii leo
Wahitimu wa kidato cha nne 2017, shule ya sekondari Eden iliyopo Mahango Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza wakisoma shairi kwenye Mahafali ya saba ya shule hii leo jumamosi Oktoba 21,2017 shuleni hapo.
Shule za Eden zinajumuisha ni shule za Nursery, Primary & Secondary za kutwa na bweni zenye kutoa elimu bora na ufaulu wa juu ambapo wanazo pia nafasi za masomo kwa ajili ya mwanao hivyo wasiliana na uongozi kwa nambari za simu 0759 81 95 23.
Binagi Media Group
Meneja wa shule za Aden, Charlotte Mbabazi, akizungumza kwenye Mahafali ya saba, shule ya sekondari Eden iliyopo Mahango Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza
Mkurugenzi wa shule za Eden, Joseph Mbabazi (katikati), akifurahia jambo kwenye Mahafali ya Saba ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden. Kushoto ni mgeni rasmi ambaye ni Mkaguzi wa Elimu
Meneja wa shule za Aden, Charlotte Mbabazi (katikati), akifurahia jambo kwenye Mahafali ya Saba ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo na kulia ni mgeni rasmi ambaye ni Mkaguzi wa Elimu
Wahitimu wa kidato cha nne, shule ya Sekondari Eden iliyopo Mahango Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea kwenye mahafali yao ya saba mwaka huu 2017 shuleni hapo
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne, shule ya Sekondari Eden iliyopo Mahango Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, wakiimba wimbo wa kuwashukuru akina mama kwa malezi bora
Pongezi kwa mmoja wa wahitimu kwa kuimba vyema wimbo wa kuwashukuru akina mama kwa malezi bora
Wahitimu wa kidato cha nne 2017, shule ya sekondari Eden wakitumbuiza kwa wimbo wa kuvutia wa kuwapongeza akina mama kwa malezi bora
Wazazi na waalimu wakifuatilia matukio yanayoendelea kwenye mahafali
Meneja wa shule za Aden, Charlotte Mbabazi, akisimama kuwalaki wahitimu wa kidato cha nne baada ya kuimba vyema wimbo wa kuwashukuru na kuwapongeza akina mama kwa malezi bora
Meneja wa shule za Aden, Charlotte Mbabazi, akiwapongeza wahitimu wa kidato cha nne baada ya kuimba vyema wimbo wa kuwashukuru na kuwapongeza akina mama kwa malezi bora
Meneja wa shule za Aden, Charlotte Mbabazi (mwenye miwani) akifurahia wimbo pamoja na wahitimu wa kidato cha nne mwaka huu
Wageni waalikwa wakifurahia jambo kwenye mahafali hayo
Wahitimu wa shule ya sekondari Eden wakitoa burudani
Wanafunzi 66 wa shule ya Sekondari Eden iliyopo Mahangu Ilemela Jijini Mwanza wanahitimu masomo yao mwaka huu 2017
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Eden iliyopo Mahangu Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza wakifuatilia mahafali hayo
Salamu kutoka kwa waalikwa meza kuu
Salamu kutoka meza kuu
Miongoni mwa wageni waalikwa akisalimia
Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye mahafali hayo katika viunga vya shule ya Eden Sekondari, Mahango Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza
Shughuli inasimamiwa na mshereheshaji maarufu Jijini Mwanza, Mc Katumba ambaye pia ni mtangazaji wa Metro Fm Mwanza
Mandhari safi na bora ya shule ya Sekondari Eden iliyopo Mahango kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza. Bonyeza HAPA Mahafali ya kidato cha saba 2017.
Saturday, January 07, 2017
Mchungaji Kulola wa EAGT Lumala Jijini Mwanza
Usikose kufuatilia maombezi na ibada ya neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, mubashara (live) kupitia ukurasa wake wa facebook.
Ni kila siku ya alhamisi kuanzia saa nane kamili mchana kupitia ukurasa wake wa facebook wa DANIEL KULOLA ambapo mahubiri na maombezi yatarushwa moja kwa moja (mubashara) kwa njia ya video.
Saturday, November 19, 2016
Makamu wa Rais Kuzindua Kampeni ya Uchunguzi wa Bure wa Saratani ya Matiti
Rais wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA), Dkt.Serafina Mkuwa (kulia), akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya Matiti na mlango wa kizazi mkoani Mwanza.
Kampeni hiyo itazinduliwa kesho katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan na baadaye kufanyika kwa siku mbili bure.
Na BMG
Kutoka kushoto ni Dkt.Mary Charles ambaye ni Makamu wa Rais MEWATA, Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, Rais wa MEWATI, Dkt.Serafina Mkuwa, Mwenyekiti Kamati ya Kampeni na Mjumbe kamati tendaji MEWATA, Dkt.Magdalena Lyimo pamoja na Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mwanza, Secilia Mrema.
Pia watumishi wa afya mkoani Mwanza wamepatiwa mafunzo kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi
Na George Binagi-GB Pazzo
Makamu wa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu, kesho
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kampeni ya uchunguzi na
matibabu ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi bila malipo mkaoni Mwanza.
Rais wa
Chama cha Madaktari Wanawake nchini MEWATA, Dkt.Serafina Mkuwa, ameyasema hayo
hii leo Jijini Mwanza wakati akitoa taarifa ya kampeni hiyo kwa wanahabari.
Amesema
baada ya ufunguzi wa kampeni hiyo, akinamama na wasichana mkoani Mwanza,
watapata fursa ya kufanya uchunguzi na matibabu ya Saratani ya matiti na mlango
wa kizazi kwa muda wa siku mbili ambazo ni kesho na kesho kutwa katika vituo
vinne ambavyo ni Uwanja wa Furahisha, Vituo vya Afya Makongoro, Karume pamoja
na Igoma Jijini Mwanza ambapo huduma zitakuwa zikitolewa kuanzia majira ya saa
moja asubuhi.
Tatizo la
saratani ya matiti na mlango wa kizazi bado ni changamoto kubwa mkoani Mwanza ambapo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, anabainisha kwamba takwimu zilizopatikana katika halmashauri za Ukerewe, Buchosa pamoja na
Kwimba, zinaonesha kwamba kati ya wanawake 1,294 waliochunguzwa, 58 wanamabadiliko ya awali ya saratani na 18 wanamabadiliko makubwa ya saratani na wamepewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata hivyo
Dkt.Subi amewahimiza wananchi kuepuka matumizi ya tumbaku, sigara pamoja na
pombe kali ambayo huchangia ongezeko la magonjwa ya saratani ya matiti na
mlango wa uzazi kwa akinamama huku akiwahimiza kufanya uchunguzi angalau mara
moja kwa mwaka ili kubaini tatizo mapema kwani tiba ya mapema husaidia
kupambana na magonjwa hayo.
Chama cha Madaktari Wanawake nchini kimeshirikiana na Wizara
ya Afya, Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza pamoja na wadau wengine wakiwemo
Gender Health, PSI pamoja na Tayoa katika kufanikisha huduma hiyo ya uchunguzi
na matibabu ya saratani ya matiti na mlango wa kizazi bila malipo mkoani
Mwanza.
Labels:
Breast Cancer,
Mh,
Mh. Samia Suluhu,
Mwanza,
Tiba,
Treatment
Sunday, November 13, 2016
Mafunzo Kwa Wasanii wa Filamu Mkoani Mwanza Yazaa Matunda
Kulia ni Mohamed Nyengi ambaye pia ni Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Shirika la Pensheni la PPF Kanda ya Ziwa, akifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Na BMG
Na George Binagi-GB Pazzo
Mafunzo kwa wasanii wa Filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini mkoani Mwanza, yamefungua milango mipya ya mafanikio katika soko la filamu mkoani Mwanza, baada ya Shirika la Pensheni la PPF kuahidi kuwajengea studio ya kisasa wasanii hao ikiwa watajiunga kwa wingi na shirika hilo.
Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa wasanii hao kujiunga na huduma za PPF, Afisa Uendeshaji na Masoko wa shirika hilo Kanda ya Ziwa, Khatibu Mussa, amesema mbali na wasanii hao kunufaika na mafao yanayotolewa na shirika hilo, pia wanaweza kunufaika zaidi kwa kujengewa studio ya kisasa kwa ajili kurekodia kazi zao ambapo ameahidi kufikisha suala hilo mbele ya uongozi kwa ajili ya utekelezaji.
Baada ya kauli hiyo, Mzee Fumbuki Lubasa ambaye ni Mkufunzi Mstaafu kutoka Chuo cha Ualimu Butimba, idara ya Fasihi kwa Kiingereza na Sanaa, alisimama na kuahidi kutoa bure kiwanja chenye thamani ya takribani shilingi Milioni 20 ili ikiwa PPF itakubali kujenga nyumba kwa ajili ya studio ya wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Hayo yanajiri ikiwa ni juhudi za Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, aliyewataka wasanii wa filamu mkoani Mwanza kuboresha soko la filamu kwa kuwa na studio bora na ya kisasa kwa ajili ya kurekodia kazi zao pamoja na kazi nyingine ikiwemo utengenezaji wa vipindi bora na vyenye maudhui ya mtanzania kwa ajili ya kuoneshwa kwenye runinga mbalimbali nchini.
Mohamed Nyengi ambaye pia ni Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Shirika la Pensheni la PPF Kanda ya Ziwa, akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga na mfuko wa PPF. Kulia pia ni Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka Shirika la Pensheni la PPF Kanda ya Ziwa, Khatibu Mussa Khatibu.
Mzee Fumbuki Lubasa (kulia) ambaye ni Mkufunzi Mstaafu kutoka Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza, idara ya Fasihi kwa Kiingereza na Sanaa. Pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Sanaa Asilia.
Alikuwa akizungumza wakati wa warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza ambapo ametoa kiwanja chenye thamani ya takribani shilingi Milioni 20 ili wasanii wa filamu Mwanza wajengewe studio ya kisasa ya kurekodi kazi za sanaa ikiwemo filamu.
Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, baada ya kujitokeza na kutoa kiwanja kwa ajili ya wasanii wa filamu Mwanza kujengewa studio ya kisaa ya kurekodia kazi za sanaa.
Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto) akisalimiana na Afisa Uendeshaji kutoka PPF Kanda ya Ziwa, Mohamed Nyengi, baada ya kujitokeza na kutoa kiwanja kwa ajili ya wasanii wa filamu Mwanza kujengewa studio ya kisaa ya kurekodia kazi za sanaa.
Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto) akisalimiana na Afisa Uendeshaji na Masoko kutoka PPF Kanda ya Ziwa, Khatibu Mussa Khatibu, baada ya kujitokeza na kutoa kiwanja kwa ajili ya wasanii wa filamu Mwanza kujengewa studio ya kisaa ya kurekodia kazi za sanaa.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akiwahamasisha wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga katika vyama vyao na kuanza kunufaika kupitia kutokana na kazi zao.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akizungumza kwenye warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Mkufunzo kutoka Chuo Kikuu Dodoma, Idara ya Habari na Ubunifu, Deodracias Nduguru, akiwafunza wasanii wa filamu mkoani Mwanza namna bora ya kujitangaza na kutangaza kazi zao ili kujulikana zaidi.
Wasanii wa filamu akiwemo Mjumbe wa Shirikisho la Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu (kulia) akiwa pamoja na Myovela Mfwaisa (kushoto).
Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy, akiwasilisha mada kuhusu namna bora ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii kwenye warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Amesema wasanii hao wakiitumia vyema mitandao ya kijamii wataweza kukuza soko lao la filamu ikiwemo kutangaza kazi zao na hivyo kuongeza mauzo ya kazi zao na kujiongezea kipato kupitia matangazo mbalimbali.
Wasanii wa filamu zaidi ya 300 mkoani Mwanza wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy, ambaye amewasilisha mada kuhusu namna bora ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii.
Bonyeza HAPA Kuhusu Mafunzo Hayo.
Saturday, October 29, 2016
Khadija Omar Kopa Adunda Mjini Mwanza na Show Kabambe!
Malikia wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omar Kopa, akitoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Mwanza usiku wa kuamkia leo ndani ya Villa Park Resort kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.
Na BMG
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.
Wananzengo wakifurahia burudani iliyotolewa kwenye Usiku wa Mshike Mshike na 102.5 Lake Fm
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Wananzengo kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza
Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ikijitambulisha kwa Wananzengo kwenye show hiyo
Madjz wa 102.5 Lake Fm, Dj Hcue (katikati), Dj KFlip (kushoto) na Dj Dhifa (kulia)
Dj Dhifa
Dj KFlip (kushoto) na Dj Hcue
Khadija Omar Kopa akihojiwa na wanahabari baada ya show
Hakika 102.5 Lake Fm Mwanza ni Raha ya Rock City na ni Redio ya Wananzengo. Kaa tayari kwa show ijayo.
Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi
Subscribe to:
Posts (Atom)

