Saturday, November 12, 2016
Wananchi Wajeruhiwa Katika Ajali Iliyohusisha Magari Manne Kongowe Temeke jijini Dar es Salaam Leo
Wananchi wakiangalia ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe, Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana. Katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa.
Wananchi wakiangali basi dogo aina ya Coster ya abiria namba T 415 DCC ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa.
Wananchi wakiwa eneo la ajali
Wananchi wakiwa eneo la ajali.
Ofisa wa Jeshi la Polisi akiwa eneo la ajali akichukua taarifa.
Prado yenye namba T 177 AHH iliyohusika katika ajali hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATU kadhaa wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea saa sita mchana na kuhusisha magari hayo lori la mafuta aina ya Scania lenye namba T 617 AQQ, Coster ya abiria namba T 415 DCC inayofanya safari zake kati ya Kilwa Masoko na Mbagala, Prado yenye namba T 177 AHH, pikipiki na lori jingine.
Ofisa wa Polisi aliyekuwepo eneo la ajali ambaye alitambulika kwa jina moja la Emanuel alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
"Nimefika sasa hivi bado hatujajua chanzo cha ajali wala watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa" alisema ofisa huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alipopigiwa simu ili kuthibitisha ajali hiyo alikiri kutokea hata hivyo alisema alikuwa hajapata taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Wilaya hiyo ambaye alikuwepo eneo la tukio.
Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Manispaa ya Temeke kwa matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment